Naamini kifo cha Magufuli kitaleta muelekeo mpya kwenye masuala kadhaa ikiwemo utawala bora na haki za binadamu, ili kulileta pamoja tena taifa letu.
Lakini kwenye kufanya kazi kwa bidii itabidi tumuenzi kwa kuendeleza pale alipoishia, ameonesha kwa vitendo kuwa kiongozi mkuu wa nchi unatakiwa kuwatumikia watanzania kwa dhati, sio kukaa tu ofisini, ili kuwapelekea maendeleo ya kweli wananchi.
Na masuala mengine yakiwemo kulinda mali za umma, na uwajibikaji, watu wasifanye kazi kwa mazoea ukikosea mahali pako pa kazi uwe tayari kuwajibika/wajibishwa, pia uthubutu wake kwenye utendaji ikiwemo ujenzi wa miradi mikubwa kama SGR, meli mpya Ziwa Victoria, na mingineyo, hakika yapo mengi mazuri yakumkumbuka.