Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Pre GE2025 Tundu Lissu: Nimewasilisha kusudio la kugombea nafasi ya Mwenyekiti CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Wakuu,

Siku ya leo Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu atakuwa ananguruma wakati anazungumza na vyombo vya habari

Fuatilia uzi huu kujua nini kinaendelea kwenye mkutano huo.

  • Katika mkutano huo uliofanyika Mlimani City, Tundu Lissu amedokeza kuwa anagombea nafasi ya Uenyekiti wa CHADEMA ambayo kwa sasa inashikiliwa na Freeman Mobwe

  • Lissu amesema kuwa tayari ameshawasilisha maombi yake ya kugombea nafasi ya Uenyekiti kwa viongozi wa juu wa CHADEMA


Akiongea na Waandishi wa Habari, Makamu wa Rais wa CHADEMA Bara, Tundu Lissu, amesema anaaamini na Wanachama wengine wanaamini kuwa ana sifa zote za Kugombea nafasi ya juu kabisa ya Uongozi wa Chama hicho kwa ngazi ya Taifa, kama zilivyoanishwa katika Katiba ya Chama.

Lissu amesema amewasilisha taarifa rasmi kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA ya kuondoa kusudio lake la kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Tanganyika) na badala yake amewasilisha kusudio la Kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Chama taifa katika Uchaguzi Mkuu wa Chama ujao.


Amefikia tamati CHADEMA, uenyekiti ataukosa, atahama, Natabiri Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti na John Heche ni wakati sahihi kwakwe kuwa makamu mwenyekiti
 
Haya madongo ni ya Mbowe kabisa kwa namna hii inabidi tu ajiandae kisaikolojia kulipokea hili japo nae ni mkoloni sana...

Nuru mpya
Mwelekeo mpya
Mapambano mapya
 
Je hatofanyiwa visa na hila kweli ?! 🤔🤔

Kwa Maneno yake ya jana Sijui juzi ya Mboe ni wazi anataka kuwa Mwenyekiti wa kudumu,
Sasa je hapo itakuwaje ?
Sio mwanzo wa hasama huo ?!
 
Lusu amechoka kuwa mwanachama wa CHADEMA
 
Hapana mkuu. Huyu labda awe waziri mkuu. Watu wenye hulka yake hawafai kuwa wa mwisho katika maamuzi. Watu kama hawa wanafaa kuwa kama sokoine, anakuwa waziri mkuu halafu raisi anasapoti afanyayo ila inapotokea jambo lisilohitaji hulka ya watu aina yake basi anakuwepo wa kummpunguza mwendo.
Unawaza kizamani sana 😂
 
Back
Top Bottom