Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Tundu Lissu: Ninampinga Magufuli hadharani. Sio mnafiki na sijahongwa

Jamani, kuna watu walikuwa wanapiga mishe haya makontena na wanachemsha huo mchanga maana dhahabu yake hauwezi kushika bila kuchemsha.
Hayana dhahabu kiivyo!
Ni hizohizo kilo tatu au pungufu wanazosema Acacia .
Sasa bakini na Mruma wenu, sisi ndio tuko kitaa .
Mruma amechunguza kitaalam wewe umejuaje?
 
ukitaka kujua Tundu Lissu ni tahira hebu angalia anacho kiongea na sisi tunacho kiongea ni tofauti.
Yeye anafikiri watu wengi wana kataa kusafirishwa kwa mchnaga kumbe kikubwa kinachopingwa ni udanganyifu kwenye kilichomo kwenye mchanga... yeye alishawai kusema mikataba hii ni ya usiri sasa anaongelea nini kitu ambacho hajawai kukiona? hivi hiyo mikataba ndio inasema kuwa wawe wanadanganya kuna kiasi fulani cha dhahabu?
Hivi Tundu Lissu utahira atapona lini? Hata ACCACIA wanajua concern ya serikali ni kuhusu kiasi kilichomo kwenye mchanga au makanika na wao wanataka upimwe tena...
Lakini Tahira Lissu anapinga utafiti kwa tumbo na mdomo tuuu...
Mwenzie Zitto amenyamaza na kusema wazi kuwa utafiti hupingwa kwa utafiti..
 
Magufuri chonde angalia kwanza mikataba hii kijinga inasemaje pamoja na nia nzuri utatuingiza kwenye majanga tafadhali
Mikataba ni mibovu hata magufuli amewahi kutamka lkn umeshasainiwa hivyo anahakikisha for time being inatekelezwe ipasavyo.
 
Mimi na wewe tunamaana moja ila tofauti miandiko tu,haihitaji cheti cha chekechea kujua ni kina nani waliotufikisha hapa ovious ni CCM asiye jua hilo akizaliwa tutamsimulia
Pamoja na lowassa
 
I'm waiting anxiously for Tundu Lissu to be next President of Tz come 2020
Hahahaha
Magufuli ni koboko walahi! Watanyooka wabaya wote! Hamna jiwe litakalosalia bila kupinduliwa, MAGUFULI FOREVER MAY HE REIGN!
 
Mkuu kweli umefanya mengi katika kupambana na hawa majizi ya madini yetu.
Huu ndio wakati muafaka kwa wewe kumuunga mkono Rais Magufuli badala ya kuponda harakati zake, mhe. Tundu Lissu elewa Rais Magufuli ni Presidential material ambayo unaweza kufanya naye kazi. Inapokuja masuala ya kitaifa tunatakiwa tuwe kitu kimoja. Sasa sio wakati wa kutafuta mchawi.
 
Naona vijana wa Lumumba kama kawaida yenu mnajaa povu..... Acheni hisia nendeni kwa hoja. Mikataba mibovu ya madini ndo iliyotufikisha hapa, na ni mikataba hii hii iliyoingiwa na serikali hii hii ya CCM.

Kila nikikumbuka sakata la samaki na gharama tulizoamriwa kulipa, nakata tamaa kabisa. Mahakamani hatutakatiza. Hawa hawa tunaoshangilia leo, hukumu zikishatoka sijui tutajificha wapi! Katika hili, tuache ushabiki wa mazoea!!!
 
Kwahiyo kama tulikaa kimya kwa sab yoyote ile hatustahili kuamka?
Wakati mnatahadhalishwa na kuonywa, na kupigwa kelele kabla ya kufanywa mlivyofanywa, mlikuwa hamsikii au ni nini hasa kilifanya mpuuzi na kukaa kimya kipindi mnaonywa?
 
huyu ni chizi tuu aseme kama mikataba iliyo sainiwa ina halalisha kudanganya kiasi cha madini kilichomo ndani ya mchanga....
Tahira huyu
Yeye anaweza kuwa chizi ila ujuaji wako utacost nchi yote kama ilivyo tanesco na mikataba nyingine. Siasa na mihemko yake isiwatoe kujua kuwa once you have penned down something ndo hivyo otherwise mipaka tuliyo nayo sasa iliyosigniwa 1884 tusingeiheshimu. Jiulize kwa nini??? Think, read, research then come back. Kwa nini hutumii maji ya Victoria kwa Irrigation wakati Misri inayatumia? Mbona hilo hupingi?
 
Huyu jamaa anapendezea sana kuimba taarabu. Hawezi kupambana na ccm kwa mipasho. Saizi yake ni akina Isha mashauzi
 
Share zao zinaporomoka kwa sababu 30% ya faida ya mgodi kwa mwaka inatokea kwenye huu mchanga halafu mtu anaweza diriki kudai auna la maana.
 
huyu ni chizi tuu aseme kama mikataba iliyo sainiwa ina halalisha kudanganya kiasi cha madini kilichomo ndani ya mchanga....
Tahira huyu

Watu wakiambiwa Mungu ni wa ajabu na Mwenye haki wanabisha sana kwa kudai eti mbina Luna masikini na matajiri pia wazima na walemavu. Kama ningekuwepo kumsaidia katika uumbaji, hakika nawaambieni mjadala wa aina hiyo ungekua ni zaidi ya Sasa. Maana watu kama ninyi wala singesumbuka kuwaumba mkiwa na vichwa vizuri vyenye akili timamu bali sehemu kilipo kichwa ningewawekeeni makalai tu uti wa mgongo wenye nguvu na imara kama punda ili mtumike katika kubeba Mizigo tu na si kuchangia hoja au kutoa maoni.
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
 
18622446_1126398777465538_2060351389369899505_n.jpg



Na mimi ni Mtanzania pia.

Tofauti kati yangu mimi na wewe na Magufuli ni hii: Mimi nimepigania nchi yangu katika masuala haya tangu mwaka '99.

Wakati huo tulikuwa na mgodi mmoja tu wa dhahabu, Resolute Golden Pride Nzega. Bulyanhulu ilikuwa haijajengwa. Geita ndio kwanza walikuwa wanafukuza wanakijiji wa Mtakuja.

Nadhani nilikuwa wa kwanza katika nchi hii kupiga yowe kwamba tutaibiwa sana kwenye sekta ya madini.

Wewe sijui ulikuwa wapi wakati huo. Najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa MaCCM na wawekezaji hawa.

Nimepigana na wawekezaji hawa mahakamani, kwenye medani ya kisiasa ndani na nje ya nchi hii kwa zaidi ya miaka 15. Nimetetea wananchi completely free of charge Bulyanhulu, Tarime, Nzega, Geita, n.k.

Sijui wewe ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa upande wa nani: wa MaCCM na wanyonyaji hawa.

Soma Rai ya tarehe 17 Julai, 2001, uone tulimwambia nini Mkapa siku anaenda kuzindua Mgodi wa Bulyanhulu.

Sijui ulikuwa wapi lakini najua Magufuli alikuwa wapi: alikuwa anatetea tumbo lake na matumbo ya wanyonyaji hawa.

Nilikamatwa na kushtakiwa kwa uchochezi kwa sababu ya Bulyanhulu. Hiyo ilikuwa December 2002. Nilikaa na kesi hiyo mahakamani Kisutu kwa miaka sita.

Sijui ulikuwa wapi ila najua Magufuli alikuwa wapi: upande wa watesi wa wananchi na wanyonyaji wa rasilmali zetu.

Leo Magufuli anajifanya mzalendo na anahoji uzalendo we yeyote anayepingana nae.

Ni muongo. Anatafuta umaarufu wa kisiasa kwa wasiojua na wasiokumbuka. Ataupata. Kwa siku chache tu. Mark my words: ataumbuka na mtaumbuka.

Mimi ninampinga hadharani. Sio mnafiki, na sijahongwa. Ninampinga kwa sababu atatusababishia matatizo makubwa zaidi kuliko tuliyonayo sasa.

Huo mchanga atauachia upelekwe ambako umepelekwa kwa miaka 16 iliyopita. Kama sheria ndiyo hiyo na mikataba ndiyo hiyo hana pakwenda.

Tatizo ninaloliona ni kwamba by the time anawarudishia mchanga wao, Tanzania itakuwa imekuwa a basket case kama Zimbabwe.

Na tutakuwa tumelipishwa mapesa mengi kama fidia na arbitral tribunals za kimataifa kwa kuvunja mikataba na wawekezaji hawa.

Kama kuna anayefikiri uzalendo ni kufumbia macho masuala haya basi huyo na amuunge mkono Magufuli kwenye upofu wake wa kujitakia.

Ripoti ya Prof. Mruma haitamaliza hata nusu saa under serious scrutiny. Zaidi ya majina ya maprofesa walioiandaa, ripoti hii haina credibility yoyote. Ni kazi ya kisiasa iliyopakwa rangi ya usomi.

Kama umefuatilia taarifa za kitaalamu za Bulyanhulu hata kabla ya Barrick Gold kuingia mwaka '99 utajua ninasema nini.

Sutton Resources, Outukumpu Oy na hata STAMICO walishafanya utafiti mkubwa juu ya utajiri wa Bulyanhulu. Taarifa zipo na zimekuwepo kwa hata mbumbumbu wa jiolojia ya madini kama mimi.

Hiki alichoambiwa Magufuli ni rubbish, hata kama ni ya kiprofesa. Rubbish. Hatuibiwi kwenye mchanga, that's the rubbish fed on the unlettered.

Tunaibiwa kwenye sheria. Kama hamuoni hilo then God have mercy on us.
Yaani we mtoto wa Antipus libarikiwe tumbo lililokubeba,,yaani ningekuwa na binti mwanamwali ningemtoa kwako buree,,nakumbuka yote uliyoongea ni kweli tupu,. Miaka yote hiyo nilikuwa nakusikiliza na natambua ukweli wako na umesimamia wapi. Big up keep it up,,wasioelewa ipo siku watakuelewa
 
Lissu tangu lini ulikuwa mzalendo! Uzalendo wa kutetea fisadi lowasa, au uchumia tumbo upi anausema zaidi ya huu wa kupewa kitu kidogo kumsafisha mtu aliye mchafua kwa miaka 10. Lissuu wadanganye vipofu wa vabichaa
Aisee,,hv ufisadi wa Lowasa ulithibitishwa kwenye mahakama ipi vle,,au tumsubiri Sizonje amtumbue maana mi nashindwa kuelewa kabisa pamoja na mkuu kulalamika jinsi alivyoteswa kwenye kampeni na huyu mtu lkn mbona anashindwa kumpeleka mahakamani,,?? Mbona ilikuwa rahisi kama mnavyofikiria kwa kutumia akili za kuazimwa,si DPP angemfungulia tu mashtaka akampeleka kwenye mahakama ya mafisadi,,!!? Au kwa nn nyie msiende kufungua tu kesi,? Serikali si inaongozwa na chama chenu cha kifisadi,mnaiba mpaka mchanga,!! Mawakili na wanasheria pamoja na wapelelezi ukichanganya vyombo vyote vya uchunguzi mnaviongoza sasa mnalalamika nn kuhusu mtu anayewanyima usingizi,!?
 
Wakati mnatahadhalishwa na kuonywa, na kupigwa kelele kabla ya kufanywa mlivyofanywa, mlikuwa hamsikii au ni nini hasa kilifanya mpuuzi na kukaa kimya kipindi mnaonywa?
Jibu swali ukiteleza hutakiwi kuamka bila kujali umetelezeshwa na nini?
 
..binafsi nimesikitika jinsi yule former PS alivyodhalilishwa.

..kwa kweli haipendezi kabisa mzee yule kuambiwa majibu aliyotoa ni "unyama wa ajabu" na stupid answer..na maneno hayo yanasemwa live
Mkuu kumbe uliona hilo, nilidhani nipeke yangu

Namkumbuka sana Nyerere katika leadership. Alikuwa na uwezo mkubwa sana wa 'communication'

Kumfukuza kazi PS katika sifa zake za kitaaluma ilitosha, kusema ni stupid ilikwenda mbali

Ni Mwanadamu hata kama ana makosa anabaki na reputation yake katika society
Ni mzee, ni mume ,baba mjomba n.k.

Tatizo letu kama alivyosema mbeziboy ni kudhani tunaweza kuangalia mambo kwa mtazamo mmoja
Ukiona jamii ya namna hiyo ujue 'imekufa' kifikra.

Ni lazima tujifunze kuangalia mambo kutoka kona tofauti ili tuweze kufikiri vema

CCM wamefanya hayo ya mtazamo mmoja wa 'ndiyoo' kule bungeni.
Matokeo yake mikataba ya madini ikapitishwa hovyo, CCM hao hao wanarudi na kudhani ni jambo jipya

Ni lazima tuvumiliane katika mawazo na mitazamo hata kama haitufurahishi
 
Tundu Lissu hajui hata namna ipi bora ya kushauri nchi inapokuwa vitani ....anaropoka kama vile ni ile michezo ya Chadema vs CCM ....anakuja na ngojera za kuanza kupigania issues za madini toka 99 na anatumia kigezo hicho kuponda kuwa hatuibiwi kwenye mchanga!!! ....hivi hiyo mikataba hata kama ingekuwa na ubora kiwango anachotaka yeye ....itaweza kuzuia udanganyifu kama huu ukihusisha maafisa wa serikali? Mbona anamshambulia JPM kuwa anajua alikuwa upande upi kipindi mikataba inasainiwa lakini hawataji mawaziri wakuu walioshiriki kama wakuu wa serikali ambao wapo nao huko Chadema? ....Tundu Lissu asitake kutafuta sifa kwenye issues za kitaifa ....maoni yake ni kama anatamani kuwasaidia ACACIA kuishtaki serikali .....atafute namna ya kutoa maoni yake kwa faida ya taifa na si kuropoka ovyo kama vile hii ni siasa .....Tundu Lissu amevimba kichwa inabidi aambiwe ukweli ....
 
Kwahiyo kama tulikaa kimya kwa sab yoyote ile hatustahili kuamka?

Mkiamka amkeni kwa heshima na aibu juu, sio mjifanye ni bonge ya wazalendo wakati mlitumia wingi wenu vibaya kupitisha mrahaba wa 3%, wakati watu walikuwa macho na wakipiga kelele kuwa tunaibiwa mkawa mnawabeza na kuwafunga.

Upuuzi huu pia iwe ni fundisho kwa wanaccm wote kwani hata maoni ya wananchi yaliyokusanywa na jaji Warioba mliyapindisha hivihivi. Ikitokea leo Magufuli akasema maoni ya jaji warioba ndio yafuatwe kwenye katiba usishangae ccm bila soni mkasimama na kujifanya ni wazalendo sana.
 
Back
Top Bottom