PreGE2025 Tundu Lissu: 'Nipo tayari kunyongwa hadi kufa, siogopi' aisisitiza No reforms, No election iendelee

PreGE2025 Tundu Lissu: 'Nipo tayari kunyongwa hadi kufa, siogopi' aisisitiza No reforms, No election iendelee

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Mb
Ingekuwa enzi za mwendazake angethubutu kusema hivyo? Ila kudos kwake kwa kuipigania haki.
MBONA HAKUNYAMAZA ENZI ZA MWENDA ZAKE? MPAKA ANAPIGWA RISASI MAMBO SI YALIKUWA HAYAHAYA TU?
 
Gentleman,
hukana haja ya kunyonga vibaka na matapeli wa kisiasa Tanzania, kama Taifa, lipo jukumu muhimu zaid la kunyorosha tabia na mienendo ya waropokaji na wachochezi chuki na uhasama miongoni mwa waTanzania waTulivu sana.

Roho ya mauti ikikulemea, kinyonge au kunywa sumu ufe, tukuzike na tukusahau na maisha ya walio hai yaendelee kusonga mbele 🐒
Kasome Riport ya CAG acha kutuchosha
 
Hakuna mtu muoga kama Mtanzania, hata mimi ni muoga sana. 🤣🤣 Hao watanzania anaowapigania ni waoga sana ataishia kuwaona mitandaoni na kwenye comments. Labda yatokee maajabu



Labda Tundu Lissu apate uungwaji mkono toka kwa watu ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama kama usalama,polisi au jeshi. Yaani unakuta kuna makapteni,makanali, mabrigedia, meja jenerali, jenerali au mkuu wa kikosi chochote, au kamandi ya jeshi au wanaanga au makao makuu ya jeshi au wanamaji au kikosi cha ardhini awe anamuunga mkono lissu. Hapo ndio uchaguzi utafanyika na nchi itanyooka. Au kamandi ipindue nchi halafu uchaguzi wa haki ufanyike au imteke bitozo asionekane mwaka mzima 🤣 angalau uchaguzi wa kueleweka utafanyika.

Nje ya hapo sisi watanzania ni waoga. Hata mimi ni muoga sana 🤣
Ila utakufa ilo ndo ulikue na uliweke kwenye akili yako Utaishi milele
 
Ukombozi wa waTanzania kutoka mikononi mwa wakoloni wapya wa CCM umeanza, na hakuna mwenye uwezo wa kuuzuia usitokee. Tundu Lissu ataongoza mapambano haya popote atakapokuwa.. Hata katika kifo ukombozi hautazuilika tena.
 
Lissu hana cha kupoteza, hana biashara kusema labda serikali itamfilisi kama ilivyofanya kwa Mbowe ndiyo maana aogopi na kisaikolojia alishajiandaa huyu, ukipona risasi 36 uwezi kuogopa kifo ten
Kabisa huyu ndiye kiongozi toka kwa Mungu maana hajawahi kumdhulumu mtu wala kuvunja sheria kwa manufaa yake binafsi.

Marekebisho ya sheria ni muhimu sana .

NI Vema Rais Samia atafakari kwa ajili yake na kujiuliza kipi kitakiunganisha taifa na kulileta pamoja kati ya kurekebisha sheria ili kura zipigwe na kuhesabiwa kwa haki au kuacha sheria zilizowaumiza wetu wengi kwenye chaguzi zote zilizopita ziendelee.
Marekebisho ya sheria za \kwa usalama wa nchi
 
Kutoka gerezani Keko, Tundu Lissu akiwa kolokoloni ametuma ujumbe kwa umma kupitia kwa Goddess Lema kuwa yeye haigopi na yupo tayari kunyongwa hadi kufa kama atakutwa na hatia. Pia amesisitiza no reforms, no election iendelelee.

Kwa kauli hizi nadhani serikali ya ccm ielewe Tundu Lissu hana cha kupoteza katika kupigania mageuzi na mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi.

View attachment 3306192
Najiuliza watawala wetu wanaishi hiihii dunia ya leo ama?Hayo mambo ya kumsweka mtu ndani kwasasa ni mbinu butu,kutunga vikesi ni mbinu za miaka ya 60!Jaman waambieni wafungue macho!
Bora wawahi kuliko wanavyojichelewesha hivyo.Ni ama wajikane na kupunguza ulafi na kutumia kidogo kinachopatikana kugawana na watz(kuleta maendeleo walau kiduchu) ama basi kugawana madaraka na wapinzani kwa kuhakikisha wanaweka at least 30% ya ushiriki kwa kuruhusu fair elections kwa asilimia hizohizo.
Kuendelea kujiona au kudhan kuwa wataendelea kutumia dola kukontroo umma ni kujidanganya.Umma utageuka kwa namna ambayo hamkuitarajia ama dola likawageuka(vyombo vya ulinzi vinaweza kubadilika na kutangukiza nchi kwanza kabla ya maslahi)!
Nnaiona HATARI sijui na wengine mnaiona!..CCM angalieni jinsi dunia inavyobadilika kuanzia Marekani,Ulaya na hata ASIA..The rise of technology ni kisu kitawachinja msipobadilka chap.Huku chini hali si hali na bahat mbaya hakuna mtu pale juu wa kuwaamsha!Mwenyekiti wenu kwa bahati mbaya amesinzia,msaidizi wake ndio kasinzia zaidi!!!!Tazameni hata vyama vinavyowasaidia kama CCP jinsi wanavyojinyima viongozi na kuhakikisha Taifa linapiga hatua.Wanatumia nguvu lakini wanajitahidi pia nchi inapiga hatua.Ninyi mko busy kununua magari kila mwaka na network ya barabara nchi nzima hakuna!!!Mko busy kutukuzwa huku chini panalegalega..yaan hakuna sekta mnaweza simama kwa uhakika mkasema tumefanya vizuri!!!You guys wake up!!!!!
 
"Hukumu ya kunyongwa mpaka kufa", hivi kuna hukumu ya kunyongwa bila kufa? Yani naona jina hilo la hukumu limekaa kisanii tu
 
TAL huku kwa ground anaeleweka kweli kila mtu na nyota yake. Lissu ni harakati na ukombozi . NOREFORMSNOELECTION
 
Back
Top Bottom