Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Nitalipa malimbikizo ya wafanyakazi yote kuanzia 2015 - 2020

Nyerere alikuwa anakusanya kodi kiasi gan bila Tra?
Alikua anakusanya kulingana na mahitaji na idadi ya watu.
Pili Mgombea Lissu wa CHADEMA anasema Ilani yao ni kufanya reforms kwenye TRA kwani apo kuna kosa gani maana tangu ianzishwe imeishafanyiwa reforms pia nyingi ila sasa CHADEMA wanasema zilizofanyika hazina tija!
 
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
Mungu na akuongoze inshallah watumishi tuna dhalilika sana mwaka wa 7 sijapanda daraja Mie nasikia tu neno daraja sijaonja ladha yake tangu niajiriwe
 
Amelipa lini nyongeza za wafanyakazi mwaka wa 5 hawajaongezewa mishahara japo sheria iko wazi ya wafanyakazi kuongezewa mshahara kila mwaka kuendana na ugumu wa maisha
Mkuu hebu nipe kifunguncha iyo sheria na sheria husika nifanye marejeo..kuuliza sio ujinga
 
Ameshindwa kubadili mfumo wa Chadema ataweza mfumo wa Tanzania?
Haahaaa mkuuu umenifanya nicheke kwa sauti kubwa aisee...kweli kidogo unachokabidhiwa ukishindwa kuaminika ktk hilo basi ni ngumu kuaminika kwenye kubwa
 
Kupunguza rate ya HESLB ni sahihi mana wanachuo wengi hawajaajiriwa lakini mkopo unazid kupanda
 
Hakika mheshimiwa Tundu Lissu anastahili hii nafasi ya urais, tujitokeza kwa wingi Oktoba tumchagua mheshimiwa Tundu Lissu awe rais wa Tanzania.
 
Tundu Lisu hajui cho chote zaidi ya sheria.
Amesema eti atawapa watanzania wote bima ya NHIF na kwamba bima hiyo itawalipa mishahara na marupurupu mazuri watumishi wote wa afya wakiwemo madaktari na manesi! Yeye na chama chake are very ignorant. Hawajui NHIF ni kitu gani.
 
Tundu Lissu anasema atalipa malimbikizo yote ya mishahara na kupandisha vyeo vyote vilivyosimama toka mwaka 2015 mpaka leo 2020.

Anasema lazima wafanyakazi walipwe fidia na Serikali yake.

Anasema atawalipa pia fidia wote waliofukuzwa kazi na Serikali ya CCM ndani ya hii miaka 5.

Anasema atarudisha makato ya loan board kutoka 15% na kuwa 3%

Na yatakuwa kwa wale tu watakao kuwa na kazi za kueleweka ndani ya serikali yake.

Anasema atafumua mfumo wa elimu ili utoke kwenye kujibu mithihani na kuwa elimu ya maarifa na kujitegemea na kuajirika kirahisi.

Anasema ataifumua TRA na kuanzisha mfumo wa Kodi moja ili nchi zote zilizo tuzunguka zije kununua bidhaa bandarini na kwenye maduka yetu ya ndani.

View attachment 1552154View attachment 1552155
Huyu ndiye Rais Sasa. Sio huyu anayewaza kununua ndege 5.

Nadhani baada ya Mkapa, Lissu atafuatia kuwa Rais aliyebadilisha mfumo wa maisha yetu kuwa bora.
 
Huyu anataka turudi kwenye uchumi tegemezi.

Atatoa wapi hela endapo anaivunja TRA?

Haelezei atainuaje uchumi wa nchi bali anaelezea atakavyoharibu mifumo mizuri iliyojengwa
Hela za kununua ndege zinazotupatia hasara zilitoka wapi?
 
Hivi kweli katika mazingira ya nchi kama Tanzania unaweza kupanda jukwaa la kampeni za uchaguzi mkuu ukatoa ahadi lukuki na zisizotekelezeka kwa kundi lenye chini ya 20% ya watanzania wote, na kutegemea kushinda uchaguzi hata kwa kura halali za wapiga kura?? Nyie watu mmerogwa na mchawi wa dunia ipi?? Au labda hata huyo mchawi wenu naye karogwa. Achilia mbali katika kundi hilo hilo bado kuna semi group ambayo ni chama tawala damu na wengine walishasusa kujiandikisha kupiga kura. Mbona mnatia huruma kupundukia!!
 
Back
Top Bottom