Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Ni makampuni ya madini yaliyonyang'anywa Retention Licenses huku yakiwa yametumia mamilioni ya fedha.Akiwa mjini Kahama, mgombea urais wa Jamhuriya muungano ndugu Tundu Antipas Lissu amesema kuwa makampuni makubwa matatu kwa mwaka huu pekee yameishtaki Tanzania kwenye mahakama za kimataifa.
"Si walisema hatutashtakiwa? Oooh Lissu alisema tutashtakiwa...mbona sasa hatujashtakiwa? Niwaambieni, kwa mwaka huu pekee makampuni matatu yametushtaki kwenye mahakama za kimataifa" Amesema Lissu bila kubainisha haya makampuni.
My take: Kutokana na Rais kubana uhuru wa upatikanaji habari na kutokana na mambo ya ajabu tunayoelezwa na serikali huku mengine yakiwa waziwazi ya uongo, naamini alichosema Lissu.
Mabadiliko yale ya Sheria ya madini yaliyofanywa na Kabudi yana upuuzi mwingi sana.
Hebu fikiria Serikali yenyewe ndiyo iliyowapa retention licenses wawekezaji. Wawekezaji hawajakiuka sheria yoyote ile wala masharti ya leseni. Unalala unaamka unasema nimefuta retention licenses zote. Na waliokuwa wanamiliki retention licenses hawana maeneo! Lazima uwe mwendawazimu hasa kufanya kitu kama hicho halafu uamini kuwa huyo aliyeonewa hatakushtaki.
Tumeshtakiwa, hatuwezi kushinda hata tungepeleka wanasheria wa kutoka sayari ya Jupiter. Tutalipa. Tusipolipa, mnajua kitachotupata. Aheri anayetembea umbali wa km 20 kwa siku, kuna siku atamaliza km 200, kuliko anayeenda kilometer 40 kwa siku halafu anarudi nyuma km 50.
Sent using Jamii Forums mobile app