Mku umesema nilichokuwa nakiwaza. Uenda Lissu anaomba huko kwa Wazungu kazi ya kuwatetea kwasababu yeye ni mwanasheria akidai kwamba anaifahamu vizuri Tz ataigalagaza. Labda hizo kesi zingine Lissu atashinda lakini kule ACCACIA alishindwa shida yeye hata mteja wake akishindwa kesi Lissu pesa harudishi. Ngoja tule pesa ya wazungu hakuna kuwaonea huruma.
..kesi za makampuni ya madini zinafunguliwa na kusikilizwa nje ya nchi.
..TL ni wakili wa kujitegemea wa hapa Tz, hana leseni ya kusimamia kesi nje ya nchi.
..kwa mfano, kesi ikifunguliwa Canada inabidi kampuni iwakilishwe na mawakili wenye leseni za kusimamia kesi ktk mahakama za Canada.
..habari kuwa TL alikuwa wakili wa acacia ni kutokufahamu vizuri historia ya TL na haya makampuni ya kigeni.
..TL alianza harakati za kupinga unyonyaji wa makampuni ya kigeni miaka ya mwisho ya 90. kulikuwa na kampuni inataka kuwadhulumu wavuvi wa eneo la Rufiji delta na TL ndiye mwanaharakati aliyesimama kidete upande wa wananchi mpaka wakaishinda kampuni hiyo.
..TL pia alitetea wachimbaji wadogo-wadogo ktk maeneo ya Bulyankhulu, Nzega, Geita, North Mara, etc. Kuna wakati serikali na jeshi la Polisi walimpiga marufuku kufika maeneo ya North Mara kwasababu TL alikuwa akiwatetea wananchi wakati serikali ilikuwa upande wa muwekezaji.
..Madai kuwa TL yuko upande wa acacia ilikuwa ni janja ya serikali na ccm wakiamini kwamba wakimchafua TL basi wao wataweza kuaminika zaidi. ukweli ni kwamba mikataba yote ya kinyonyaji ilisainiwa na watendaji wa serikali za ccm.
NB:
..Deo Mwanyika ambaye alipata kuwa ceo wa acacia na mtendaji wa ngazi za juu wa barrick ametia nia na kushinda kura za maoni za ubunge ktk chama cha mapinduzi.