Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anasema hatutashitakiwa, kwa mwaka 2020 pekee makampuni matatu yametushitaki kwenye mahakama za kimataifa

Ni makampuni ya madini yaliyonyang'anywa Retention Licenses huku yakiwa yametumia mamilioni ya fedha.

Mabadiliko yale ya Sheria ya madini yaliyofanywa na Kabudi yana upuuzi mwingi sana.

Hebu fikiria Serikali yenyewe ndiyo iliyowapa retention licenses wawekezaji. Wawekezaji hawajakiuka sheria yoyote ile wala masharti ya leseni. Unalala unaamka unasema nimefuta retention licenses zote. Na waliokuwa wanamiliki retention licenses hawana maeneo! Lazima uwe mwendawazimu hasa kufanya kitu kama hicho halafu uamini kuwa huyo aliyeonewa hatakushtaki.

Tumeshtakiwa, hatuwezi kushinda hata tungepeleka wanasheria wa kutoka sayari ya Jupiter. Tutalipa. Tusipolipa, mnajua kitachotupata. Aheri anayetembea umbali wa km 20 kwa siku, kuna siku atamaliza km 200, kuliko anayeenda kilometer 40 kwa siku halafu anarudi nyuma km 50.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama hatuogopi kushitakiwa unajua ni kwanini matokeo ya urais Tanzania hayapingwi mahakamani?
Lakini hapa mada ni serikali kushitakiwa.

BTW:Ungetuambia kwanza ni kwa nini MwanaCHADEMA akipinga maamuzi yoyote ya chama mahakamani anakuwa amejifukuzisha uanachama.
 
Lakini hapa mada ni serikali kushitakiwa.

BTW:Ungetuambia kwanza ni kwa nini MwanaCHADEMA akipinga maamuzi yoyote ya chama mahakamani anakuwa amejifukuzisha uanachama.
Mkuu tafuta kujua kwanza kwenye kupinga matokeo ya urais nani anashitakiwa kabla ya kulinganisha nchi na chama cha siasa.
Chadema ilinganishe na CCM na Tanzania ilinganishe na kenya,Malawi and other countries.hope umenielewa
 
Sasa kataja hizo kampuni?

Lisu ataaibika san kwenye uchaguI huu
 
Ha Hana sera huyo hajui anaongea nini, kama anajua hakuna uhuru aliwezaje kusema tuna kesi?
Yeyebkila siku anaongea ujinga kuhusu kesi, sasa akichukua nchi atazuia hizo nchi kutushitaki?
Au hizo kesi zilizofunguliwa zitafutwabkwa kuwa zinamlenga magufuri na sio nchi?
Huyu jamaa ni poyoyo sana.
 
Mkono Nimrod ameitetea tanesco sana mkuu

..siyo yeye aliyewakilisha Tanesco huko nje.

..unaweza kwenda kwenye website ya mahakama tunayoizungumzia na utakutana na listi ya mawakili wote wenye leseni za kusimamia kesi ktk mahakama hiyo.
 
Gambia walikuwa wajamaa na yahya jammeh alitoka
 
Mwambieni tunajua..hata mkulima katushtaki zaidi ya mara moja.. ila vipi kuhusu miga?
 
wew ni bure kabisa
 
TL binafsi nilisikitika sana alipojeruhiwa. Ila sikubaliani Naye kabisa kwa jinsi anavyopenda kuona Tanzania inanyanyasika na kupata shida na mataifa ya nje. Yeye ananufaika na nini?
 
Upande mmoja wenye haki yao walisha anza tangu 2015
Hawajawahi kukoma kupiga kampeni, wanahubiri barabara na madaraja kila siku kama vile ndicho chakula kwetu.
Huo ni ushamba, hawaoni hata haya kuhubiri vitu ambavyo tulipaswa kuwa navyo tangu miaka ya 90 sawa na wakenya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…