Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anayekula rambirambi hatufai

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Rais anayekula rambirambi hatufai

Mzalendo2015

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2012
Posts
6,710
Reaction score
9,063
Mgombea wa Urais kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Tundu Antipas Lissu amewaambia wana-Kagera wazi kuwa RAIS anayekula Rambirambi hafai kuwa Rais.

Mhe. Lissu alikuwa akiwakumbusha Wana Kagera alichowafanyia Rais Magufuli baada ya janga la tetemeko la Ardhi alipobadili matumizi ya Fedha za Rambirambi kusipeleka kujenga reli na mabarabara akisema ati," SERIKALI YAKE YA CCM HAIKULETA TETEMEKO LA ARDHI".


https://www.jamiiforums.com/data/at...a_Kagera.__Wananchi_wa_Kagera__480_X_480_.mp4
 
Uongo Uongo Uongo, yani mgombea urais unathubutu kuidanganya kadamnasi. Hufaia kuiongoza Tanzania. Umeona wapi popote pale duniani ambapo maafa yanatokea halafu serikali inakimbilia kujenga nyumba za watu binafsi kabla ya kujenga miundombinu ya eneo husika liliathirika?
 
Alwatan kafikiria...Hela za maafa zinapitia kwenye mfuko maalum wa maafa na lengo lake ni kusaidia katika Huduma za kijamii za muhimu hivyo hata Hela zilizotolewa zilitumika kurekebisha miundombinu ya Huduma za kijamii zilizokua zimeharibika kama Hospital, Mashule na Mengineyo.

Niliskia hili.

Au kuna namna zilifanyiwa nini?
 
Hii tabia ya uropokaji wa Rais Magufuli kwa Sasa una mgharimu vibaya Sana!!!![/QUOTE]Tindulissu aache mambo yake kabisa.

Huduma za kijamii ni msingi Sana zile fedha walipewa waliweka kwenye huduma zaa kijamii zilizoharibika isingekua Rahisi kila mtu kupewa fedha.
 
Uongo Uongo Uongo, yani mgombea urais unathubutu kuidanganya kadamnasi. Hufaia kuiongoza Tanzania. Umeona wapi popote pale duniani ambapo maafa yanatokea halafu serikali inakimbilia kujenga nyumba za watu binafsi kabla ya kujenga miundombinu ya eneo husika liliathirika?
Hatukuchanga hela za kujenga miundombinu, kama serekali ingejenga kwa chanzo kingine cha mapato sawa.

Si bora waathirika wangeweka namba zao za simu tuwarushie moja kwa moja.
 
Kama kweli watu wameamua kukesha kwa sababu ya Lissu ni hatari. Jamani nataka niwaambie ukweli, J P M hajui uhalisia huu. Anadanganyika na watu wanaoenda kuwatazama wasanii, hawa wasanii wanapofanya mambo yao, huwa ni aghali sana, leo wanafanya mambo yao bure kwa nini watu wasikimbilie? Nyinyi CCM haki ya Mungu msipoliangalia vizuri hili tarehe 28 Octoba mnaenda kufa, nyie endeleeni kujifariji, uchaguzi huu upo tofauti na tulivyozoea.
 
Back
Top Bottom