Akilindogosana
JF-Expert Member
- Jan 12, 2020
- 4,303
- 12,679
Vijana bhana walio CCM nawaonea huruma sanaBinafsi nshindwa kuelewa kwanini mgombea wa chama cha Demokrasia na Maendeleo kila akipanda jukwaani ni CCM mpaka anamaliza hotuba yake.
Anatumia muda wote kuiongelea CCM na serikali yake. Tumia jukwaa kutuambia unaenda kutufanyia nini Watanzania ambacho serikali zote za CCM zilishindwa...
Mbona alisema anawajua kwa majinaHv ulishaambiwa hawajulikani wala hawafahamiki , sasa utawachukuliaje hatua wasiojulikana? Amesema amesha wasamehe
Huna ulijualo wewe, kwanza kwanini unaandika "iyo" badala ya "hiyo". Halafu eti uijue katiba ya JMT, wewe zao la kata.Iyo katiba ya Ufipa sio ya JMT
TAKUKURU HAWAMSIKII LISU?Amesema Rais Magufuli huku akiwa ameshatangazwa kuwa Mgombea Urais wa Tanzania kupitia CCM kwenye Uchaguzi wa Oktoba 2020 ametoa rushwa Wilayani Kibiti kwa mujibu wa Fomu ya Kuweka Mapingamizi dhidi ya Mgombea Urais Amesema Rais Magufuli alipokuwa akigawa fedha kwa ajili ya madawati na shule alikiuka sababu ya 16 kwenye Fomu hiyo inayosema Mgombea Urais anaweza kuwekewa pingamizi iwapo atakiuka Makatazo yaliyotatwa kwenye sheria ya gharama za Uchaguzi
Mhe. Tundu Lissu mgombea Urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CHADEMA ameendelea kusisitiza kuwa hawezi kufungwa kwa kesi alizo nazo Mahakamani na kwamba haziwezi kumzuia kugombea Urais.
“Hafungwi mtu hapa” “Nina kesi sita Kisutu na zote ni za uchochezi.” Baraza Kuu la chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA, limemchagua Tundu Lissu kuwa mgombea wake wa Urais katika Uchaguzi Mkuu 2020.
Mhe. Lissu ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa si yeye tu anayeweza kuwekewa pingamizi la kugombea Urais bali hata Mhe. Rais Magufuli pia anaweza kuwekewa pingamizi.
"Nani aliyesema kwamba CCM hawawezi kuwekewa mapingamizi? Nani aliyesema mgombea urais wa CCM, John Magufuli hawezi kuwekewa mapingamizi.? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa CHADEMA"
Kwenye fomu ya mapingamizi, kwenye sababu 16, la 16 Magufuli amekiuka Mambo yaliyokatazwa moja wapo ni rushwa maana ukishaingia kwenye uchaguzi huruhusiwi kutoa rushwa, Magufuli akiwa anatoka kumzika Mkapa Lupaso, alifanya nini Kibiti? " Tundu Lissu, Mgombea Urais wa
CHADEMA
Lissu amesema kitendo cha Rais kutoa fedha Kibiti, kununua jogoo kwa Laki Moja ni rushwa wakati wa uchaguzi.
Mhe. Lissu katika moja ya sera zake amesema iwapo atashinda basi atakuwa na jukumu kubwa la kurudisha uhusiano wa nchi kimataifa.
"Tukishinda urais wa Tanzania, mimi nitakuwa Rais wa Katiba mpya. Kama tunataka mfumo mzuri wa utawala, mahali pa kuanzia ni Katiba mpya. Hii ndilo tutaanza nalo. Haina maana hatutajenga shule, kuboresha Sekta ya Afya '
MY TAKE: Bado tutandelea kushuhudia matamko mengi kwenye Uchaguzi huu ni juu yetu watanzania kumpima kila mgombea ili tupate kiongozi bora kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Lisu ni genius hapa TanzaniaNa hapo ndipo penye mtego kwa wana kijani maana na wao mgombea wao atawekewa pingamizi zenye mashiko.
Yani ni jino kwa jino, mguu kwa mguu.
UtopoloRais ndio amekuwa nominated na CCM kugombea nafasi ya Urais.
Ila Bado hatupo kwenye Campaign process ambapo ndipo vyama huuza sera baada ya wagombea wake kuidhinishwa na NEC.
Pia hatupo kwenye Election. (Uchaguzi).
Rais yupo kwenye majukumu yake ya kawaida kabisa.
Hivyo Hawa wapiga kelele hawana hoja.
Ataingiza watu roadNEC. hawatampatia fomu maana ana kesi za kujibu lakini pia ana zuio la maadili ya utumishi wa umma. Lakini ningeshauri wampe.
Mkuu acha kuweweseka,mwaka huu mnapenda kushitaki wapi? Uchaguzi wa mwaka 2015 mlikimbilia CCJ mwaka huu MNA mawakli wa Amsterdam, hivi ni vituko.
Kila Mara twawambieni huyu lissu hafai anawapotosheni ninyi hapana kuelewa.
Lissu hafai anapaswa kupingwa na kila mtanzania mpenda amani naaendeleo.
Hayo yamesemwa na Mwanasharia nguli duniani na mgombea Urais wa Jamuhuri ya Mungano wa Tanzani kupitia Chadema ndugu Tundu Lissu!
Tundu Lissu amesema kitendo cha Rais Magufuli kupewa jogoo huko Kilwa na kulipa shilingi laki moja ni kitendo cha utoaji wa rushwa kwa wapiga kura kwani bei ya jogoo inajulikani ni shilingi elfu kumi tu.
Pamoja na malipo hayo makubwa kwa jogoo, Lissu amesema hata ile milioni tano aliyotoa Rais Magufuli kwa ajili ya shule pia ni rushwa kwani matendo hayo yamefanyika wakati rais Magufuli akijua yeye ni Mugombea!
Kwa kuwa vitendo hivyo vinakatazwa na sheria za Uchaguzi, Lissu anakusidia kumuwekea pingamizi Rais Magufuli asiteuliwe n Tume ya Uchaguzi kupeperusha bendera ya CCM.
Ushauri wa bure kwa CCM wabadili gia haraka, kwani kuna uwezekano mkubwa Rais Magufuli asiteuliwe na Tume kwa makosa aliyofanya ya kukiuka sheria za Uchaguzi!