Tundu Lissu: Rais wetu ni Rais wa Kifalme, hawajibiki kisheria mahali popote, anawajibika kwa Mungu wake tu

Tundu Lissu: Rais wetu ni Rais wa Kifalme, hawajibiki kisheria mahali popote, anawajibika kwa Mungu wake tu

Kwanza umedeclare kua wewe ni shabiki namba moja wa Magu, hivyo si rahisi wewe kukubali kua huyo raisi wako alikosea mahala. Ni mbaya sana hii kumuelimisha mtu ambaye tayari ana majibu yake asiyotaka yabadilishwe.

Hoja sio dhaifu mkuu na hapo hao nimetaja wachache mno, kiufupi uongozi uliopita ulikua unafanya kazi kwa mihemko kupita kiasi. PM aliepita ambaye ndo huyuhuyu ila ni kama tofauti(sijui umeelewa).

Kubali kataa Magu kuna mambo alikua anafanya nje ya katiba, hakuacha wizara zifanye kazi yake( huku kwetu tunawaita kina kajua yote). Ila kwakua wewe ni shabiki huwezi kuona hayo, utatetea hata madudu.
Ni kweli ndiyo maana nkatangulia mapema kutoa angalizo kwamba kwa Magu pengine hatutaweza kukubaliana.

Hata hivyo naheshimu mtazamo wako na najua kuwa hakuna Rais, si Nyerere hadi Samia, atakayeweza kuwaridhisha watu wote. Na ndio mantiki ya Rais kupewa kinga ya kutoshtakiwa kwa yale aliyoyatekeleza akiwa madarakani.
 
Ww nguchiro hakuna aliyetukuka zaid ya Mungu,ucwe zumbukuku hvyo
Lissu bana!

Kila nchi na utaratibu wake -- kuna nchi nyingine viongozi wao ni wafalme kabisa na wakifa watoto wao wanasimikwa kuwa wafalme. Na mambo ya nchi zao yanaenda.

Na sisi utaratibu wetu ni kwamba Rais wetu awe na mamlaka yale -- waasisi wa Tanzania waliowaza na kuisuka hiyo katiba iliyompa Rais hayo madaraka hawakuwa wajinga. Nachukia sana kuona watu ambao hawajaifanyia Tanzania kitu chochote cha maana zaidi ya ulalamishi na kutafuna kodi zetu kupitia ulalamishi tu na kuquestion wisdom ya waasisi wetu waliotukuka. Who is Lissu katika nchi ya mamilioni ya watanzania wanaoona ni sahihi Rais kuwa na madaraka aliyo nayo?

Awkward!
 
Ni kweli ndiyo maana nkatangulia mapema kutoa angalizo kwamba kwa Magu pengine hatutaweza kukubaliana.

Hata hivyo naheshimu mtazamo wako na najua kuwa hakuna Rais, si Nyerere hadi Samia, atakayeweza kuwaridhisha watu wote. Na ndio mantiki ya Rais kupewa kinga ya kutoshtakiwa kwa yale aliyoyatekeleza akiwa madarakani.
Daah yani mkuu na hiyo kinga pia unaiona ni sawa??

Sawa mkuu. Acha tuishie hapa.
 
"Kulazimishwa kwa Spika Ndugai kujiuzulu kunathibitisha wazi kabisa kile ambacho tumekisema kwa miaka mingi, kwamba kwa mfumo wetu wa kikatiba na kiutawala tuna muhimili mmoja tu wa dola na muhimili huo unaitwa Rais." Mhe. @TunduALissu.

"Kwa miaka 60 ya uhuru tangu 1962 utaratibu wa Mihimili mikuu 3 inayothibitiana imevurugwa kwa maana kwamba Rais amekuwa na madaraka makubwa sana. Rais wetu ni Rais wa kifalme, mamlaka yake hayana udhibiti, hawajibiki kisheria mahali popote, anawajibika kwa Mungu wake tu." Lissu
Acha uongo.. TL ameyasema hayo lini na wapi? Watu mnaandika uongo kabisa wa kujitungia wenyewe. Hapa ndio TL akisema kuhusu hili
 
"Kulazimishwa kwa Spika Ndugai kujiuzulu kunathibitisha wazi kabisa kile ambacho tumekisema kwa miaka mingi, kwamba kwa mfumo wetu wa kikatiba na kiutawala tuna muhimili mmoja tu wa dola na muhimili huo unaitwa Rais." Mhe. @TunduALissu.

"Kwa miaka 60 ya uhuru tangu 1962 utaratibu wa Mihimili mikuu 3 inayothibitiana imevurugwa kwa maana kwamba Rais amekuwa na madaraka makubwa sana. Rais wetu ni Rais wa kifalme, mamlaka yake hayana udhibiti, hawajibiki kisheria mahali popote, anawajibika kwa Mungu wake tu." Lissu

Of course, yes! Lissu hakuwepo tu wakati wa kusimikwa kwa Paramount Chief Hangaya.
 
Back
Top Bottom