Chadema wataangukia pua kama wata msimamisha Tundu Lissu. Kwa sababu Tundu Lisu siyo presidential material. Kwangu mimi Mbowe ndo presidential material pekee Chadema. Wengine wote bado wana mihemuko mingi
Wewe unataka kuanzisha mjadala mgumu sana ambao muda na nafasi ya kuujadili na hata kufikia maafikiano hakuna.
"Presidential Material" ina maana nyingi kwa watu mbalimbali. Vipimo vyake ni vya aina mbalimbali kwa kila mtu.
Kwa hiyo, kusema tu kuwa mtu sio 'Presidential Material' na kuishia hapo kwa kweli haitoshi kabisa.
Tuchukulie aliyepo sasa, sijui kama kwako ndie 'Presidential Material' au hapana? Ni kipi kinachokufanya uone anazo sifa hizo?
Na mtu kuwa 'Presidential Material', ni lazima awe na sifa zote unazozitaka wewe, au hata akiwa na baadhi ya sifa hizo na kukosa zingine, na ukapima kati ya pande mbili hizo, si unaweza ukaamua kwa kupima hivyo?
Utampata wapi mtu kamilifu kabisa anayekidhi kila aina ya sifa unayotaka awe nayo president?
Kuna mambo nisiyoyataka aliyo nayo Tundu Lissu, lakini Magufuli anayo.
Mambo aliyonayo Magufuli, na nisiyokubaliana naye kabisa, kwa sababu ni ya 'msingi' kabisa katika uongozi; mambo hayo siyaoni kwa Tundu Lissu; na kwa kuwa ndiyo ya 'msingi' katika vipimo vyangu, namwona pia kwamba anakidhi kuwa kiongozi kulikoMagufuli.
Sasa sijui kama utanielewa nilichoandika hapa.