Uchaguzi 2020 Tundu Lissu rasmi kupambana na Rais Magufuli

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu rasmi kupambana na Rais Magufuli

Watu wengi tulidhani Magufuli angekuwa rais bora, kutokana na uchapa kazi na misimamo yake. Sasa hivi nimejifunza, watu wenye misimamo mikali hawafai kuwa ma Rais, ni watu wenye viburi, kujiamini kuliko pitiliza na wasio penda kusikiliza watu wengine. Tundu Lissu hana tofauti na Magufuli, tabia zao zinafanana sana. Tindu Lisu hafai kuwa Rais.
Basi wewe tuambie nani anafaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe unaamini hata kama kuna tume huru Chadema anaweza akashinda?

Weka tume huru ya uchaguzi kisha uone, hata kama ccm itashinda sio kwa majority tena, na uchaguzi utakaofuata ndio inamaliziwa jumla. Binadamu wana tabia ya kuchoka kitu, hivyo ccm haya ifanye mazuri gani, watu wameichoka, hivyo kugomea tume huru na kutumia vyombo vya dola sio kwamba wanapenda, bali hakuna jinsi. Na kwa taarifa yako ccm ikiendelea kuwa madarakani, haitokaa itawale kwa ridhaa ya wananchi walio wengi, hivyo mara zote itabidi itawale kwa mabavu tu.
 
Eti tume huru! Kwani tume ndo inapiga kura? Nyie hazimo kabisa! Huyo mhanga utampambanisha na JPM? Hizo hela za kampeni CHADEMA kajengee ofisi

Tena hakuna mtu mrahisi kama JPM, ukitaka kujua ni mwepesi, uitishwe mdahalo wagombea wa urais uone kati yake na Lissu nani atageuka kuwa kituko. Yeye kugomea vyama vya upinzani kufanya siasa ni kwakuwa anajua yeye hana uwezo wa ushawishi, hivyo anajua atafunikwa.
 
Kweli tunahitaji mabadilkko, utawala wa kisheria, mabadilkko ya katiba , kiongozi atakaye jali utu na haki za binaadamu, tunahitaji kuimarish hii miimili mi3, kumpunguzia raisi nguvu aliyonayo (ufalme Juha) tunaamini hayo yote ,kutokana na sera za chadema yanawezekana kabisa, hivyo Tundu lissu ni chaguo sahii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa atawezaje kukagwaride mmh nauliza tu ataweza kweli kumatch mwendo na kamanda 😁😁😁

Ukiwa rais hata ukitaka hao makamanda wakubebe mgongoni wakati unakagua gwaride wala hamna shida. Ukitaka kujua ukishakua rais jeshi ni kitu kidogo sana na unaweza kufanya lolote na wala wasibishe, rejea siku Magufuli kapokea makada wa ccm kwenye kamisheni ya jeshi, huku jeshi likiwa limetengwa kabisa kikatiba na siasa.
 
Chadema wataangukia pua kama wata msimamisha Tundu Lissu. Kwa sababu Tundu Lisu siyo presidential material. Kwangu mimi Mbowe ndo presidential material pekee Chadema. Wengine wote bado wana mihemuko mingi

Kama JK na Magufuli wameweza kuwa marais wa Tanzania, basi hakuna mtu yoyote mwenye akili timamu atashindwa kazi hiyo. Kazi ambayo unafanya lolote utakalo, na wala hushitakiwi ukiwa madarakani au ukiwa umetoka kuna mtu atashindwa kazi hiyo kweli?
 
Chadema wataangukia pua kama wata msimamisha Tundu Lissu. Kwa sababu Tundu Lisu siyo presidential material. Kwangu mimi Mbowe ndo presidential material pekee Chadema. Wengine wote bado wana mihemuko mingi
Wewe unataka kuanzisha mjadala mgumu sana ambao muda na nafasi ya kuujadili na hata kufikia maafikiano hakuna.

"Presidential Material" ina maana nyingi kwa watu mbalimbali. Vipimo vyake ni vya aina mbalimbali kwa kila mtu.

Kwa hiyo, kusema tu kuwa mtu sio 'Presidential Material' na kuishia hapo kwa kweli haitoshi kabisa.

Tuchukulie aliyepo sasa, sijui kama kwako ndie 'Presidential Material' au hapana? Ni kipi kinachokufanya uone anazo sifa hizo?

Na mtu kuwa 'Presidential Material', ni lazima awe na sifa zote unazozitaka wewe, au hata akiwa na baadhi ya sifa hizo na kukosa zingine, na ukapima kati ya pande mbili hizo, si unaweza ukaamua kwa kupima hivyo?

Utampata wapi mtu kamilifu kabisa anayekidhi kila aina ya sifa unayotaka awe nayo president?

Kuna mambo nisiyoyataka aliyo nayo Tundu Lissu, lakini Magufuli anayo.

Mambo aliyonayo Magufuli, na nisiyokubaliana naye kabisa, kwa sababu ni ya 'msingi' kabisa katika uongozi; mambo hayo siyaoni kwa Tundu Lissu; na kwa kuwa ndiyo ya 'msingi' katika vipimo vyangu, namwona pia kwamba anakidhi kuwa kiongozi kulikoMagufuli.

Sasa sijui kama utanielewa nilichoandika hapa.
 
Anakuja ndiyo maana Chadema wameanza kumtambulisha kwa Wananchi.
Mara ngapi uliambiwa anarudi nchini na hajarudi hadi leo?
Mwenyewe alisema nikimaliza matibabu na daktari wangu akinirugusu nitarudi nyumbani na mwishowe kasema amemaliza matibabu lakini bado hajarudi.

Hiyo kuwekwa kwenyemagazeti ni propaganda tu za kisiasa hata ile habari ya kurudi September 2019 iliwekwa kwenye magazeti hayo hayo.
 
Labda kama ni uraisa wa ubelgiji
Fomu ya chadema tu amejaza akiwa kenya
Fomu ya urais wa Tanzania kwa mujibu wa sheria ni lazima mgombea achukue na kuirudisha mwenyewe
 
Back
Top Bottom