Tayari Serikali ya Tanzania ilishaondoa huduma zote za Jamii ikiwemo kulifutilia mbali eneo hilo
Historia ya makatili huishia vibaya sana, dola inabidi ijitizame maana kwa miongo na karne nyingi zijazo majina ya watawala walioongoza operesheni hizi yataabisha vizazi vyao, kwa makaburi yao kuhamishwa, sanamu zao kuondolewa, mabango na picha pia kupelekwa makumbusho sehemu maalum itakayoonesha historia ya ukweli juu ya ukatili na maafa yaliyotenda enzi ya tawala za kifashisti na kidiktekta
TOKA MAKTABA :
Habari zaidi za historia za tawala za mkono wa chuma kandamizi :
24 Apr 2018
Madrid, Spain
Mihimili ya Bunge na Mahakama za afiki kuweka historia sahihi ya dikteta Jenerali Franco wa Uhispania
Diktekta Jenerali Francisco Franco alitawala taifa hilo la Hispania kwa staili ya utawala wa 'mkono wa chuma' kwa muda wa miaka 39 hadi alipofariki dunia kwa afya dhoofu mwaka 1975.
Katika kipindi chake cha utawala wa Jenerali Franco, watu wengi walipotea ktk mazingira ya utatanishi na wengineo maelfu kufungwa jela kutokana na kuwa na itikadi tofauti za kisiasa zilizokwaza utawala wake.
Diktekta Franco alikuwa na mahusiano ya karibu viongozi wa juu wa kanisa, maana kanisa lilikuwa na ushawishi ktk maisha ya raia na pia kuunga mkono utawala wa kifalme ktk Hispania.
Jenerali Franco katika vita (1936-1939) vya wenyewe kwa wenyewe Hispania iliyoisha mwaka 1939 hakutaka kuona nchi hiyo ikiishia kumeguka ktk majimbo ya Catalonia n.k Hivyo alitumia majeshi kuhakikisha nchi inabakia bila mgawanyiko. Ushindi wa majeshi ya Franco, ulishangiliwa na kubatizwa kuwa ni ushindi dhidi ya wapiganaji wasio na imani ktk uwepo wa Mungu, Ufalme , uzalendo na umoja wa taifa.
Vita hivyo vilisababisha maelfu ya vifo na Diktekta Franco kuja na wazo la Kujenga basilica / makumbusho maalum ktk mfano wa kanisa kuwaenzi waliopoteza maisha ktk vita hivyo vya wenyewe kwa wenyewe.
Katika wosia wake Dikteta Franco, aliomba kuzikwa ktk basilica hilo na wahanga wengine wa vita ili kujibainisha na wafu wengine waliopigania au kufa kutetea taifa hilo la Hispania lisigawanyike.
Hata hivyo miaka 43 baadaye toka kifo cha diktekta huyo, wananchi, mwanaharakati wa haki za binadamu na wanasiasa wameona kuwa ukatili uliofanyika na utawala wake haustahili kusahauliwa.
Hivyo kupitia Bunge na Mahakama wameona kuweka historia sahihi kuwa ktk utawala wa Franco kuna unyama na ukatili mwingi ulitendeka ktk utawala wake uliodumu miaka 39.
Kuhitimisha hilo, hoja ya kufukuliwa mwili wake imepitishwa Bungeni na kutiliwa uzito mahakamani kisheria kuwa Diktekta huyo hastahili kulala ktk makumbusho hayo kutokana na vitendo viovu vilivyofanyika ktk utawala wake wa kiimla.
13 Sept 2018
Mwili wa dikteta Fransico Franco waondolewa kutoka makaburi ya mashujaa nchini Spain, baada ya bunge la Spain kukubaliana kuwa kwa ukatili wa diktekta Franco, mwili wake haustahili kulala ktk makaburi ya mashujaa tajwa wa Spain hivyo ufukuliwe na kwenda kuzikwa sehemu familia ya Francisco Franco itachagua kumhifadhi mtu wa familia yao
Spanish court has for the first time authorised the exhumation of bodies from the Valley of the Fallen. It is a vast mausoleum where the fascist dictator General Franco is buried with thousands of victims of Spain’s 1936 civil war
View: https://m.youtube.com/watch?v=W8IFtfhIy48
All countries have to make choices about what in their history to honor - and who. The Spanish parliament passed a vote today to exhume the body of former dictator Fransisco Franco from a place of honor in a national monument, taking a step away from their fascist past.