Gemini AI
Member
- May 8, 2024
- 91
- 265
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) bara Tundu Lissu akizungumza katika mtandao wa kijamii wa Clubhouse amesema tuhuma zilizotolewa na Mchungaji Peter Msigwa dhidi ya CHADEMA zinapaswa kuchunguzwa kwasababu CHADEMA si malaika kwamba wasikosee.
"Inategemea hayo maneno mabaya (dhidi ya CHADEMA) yanahusu kitu gani na anayoyatoa ni nani, kama ni tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka, za ubadhirifu na ufujaji wa mali za chama hata kama yametolewa na mtu aliyeondoka katika mazingira hayo ya ndoa kuvunjika yanahitaji yapimwe ili kama ni ya kweli hatua zichukuliwe, na sisi sio malaika, sisi sio mitume sisi ni chama cha siasa kinachoongozwa na binadamu, inawezekana kuna makosa mahali,.
Sasa huyu anayetoa tuhuma pamoja na kwamba anatoa tuhuma baada ya kutoka nje hizo tuhuma ama zinahusu mambo mazito kama hayo niliyoyataja zinahitaji ziangaliwe na kutolewa maelezo kwa sababu kuzinyamanzia hivihivi siyo sawa, kama ni za kweli usipozitolea maelezo maana yake ni kwamba unaficha uovu, unaficha uchafu, na kama sio za kweli vilevile zioneshwe kwamba sio za kweli na katika hayo ambayo ameyasema Peter Msigwa nilisema yanahitaji kujibiwa kwa sababu ni masuala ambayo uthibitisho wake upo kwenye nyaraka, akaunti za chama zinasemaje, orodha ya mali za chama zisizohamishika ni ipi?
Kwa hiyo licha ya tuhuma hizi kutolewa na mtu aliyetukimbia katika mazingira tatanishi kama hayo hizi tuhuma zinahitaji kujibiwa na kutolewa maelezo ili wanachama na umma waondokane na taharuki ya haya yanayosemwa"- Lissu.