Pre GE2025 Tundu Lissu: Tuhuma za Msigwa kwa CHADEMA zichunguzwe, sisi si Malaika

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hapana.
Tundu Lissu kuwa muwazi ni sahihi kabisa. Ndiyo, mtuhumiwa mkuu, sasa ni wazi ni Mbowe mwenyewe. Acha maji yafuate mkondo wake.
Mbowe anaonekana tu kuwa si mpinzani wala mwanasiasa wa kweli na hayuko serious kwenye siasa zaidi ya kuichukulia siasa kama mradi wa biashara. Anakwamisha sana harakati za upinzani.
 
hawezi kupokelewa ccm, na hata akienda huko hawez kupata platfom.
lisu ni kigeugeu hata akienda ccm kuna siku atamgeuka mwenyekiti
Sema "Lissu siyo MNAFIKI"..., huo "ukigeugeu ni kuhusu nini? Ni lini ulimsikia akiwa kigeugeu?"
 
of course yeye kama makamu mwenyekiti, aliyepo juu yake ni mmoja tu, Mwenyekiti. ukiona anachelea kusema hivi jua anawaambia watz kuwa mwenyekiti hachukui hatua, azichukue haraka au anawaambia pccb kuwa mwenyekiti na wenzake wanalamba asali waende wawachunguze. maana yake yeye angekuwa mwenyekiti angeshachukua hatua.
 
Mimi sina chama au itikadi lakini Nimekuwa nikifuatilia kwa umakini hojaji zao kuhusu masuala ya chadema au kupitia Lissu au Dr Slaa au mwingine yeyote. Inaonekana kuwa wanaibua issues zenye mwelekeo wa kuibomoa chadema. Mara kadhaa Dr Slaa amekuwa akiwakwepa sana katika kuwajibu. Na pia Tundu Lissu mpaka kufikia kuwaambia" wanataka aseme yajayo wanavyotaka wao" kwa kujaribu kumwekea maneno mdomoni ili hali ya kisiasa ichafuke.Chukueni tahadhari na mijadala yao.
 
Mbona ukikaribia uchaguzi tuhuma kama hizi hutolewa ndiyo kauli ya Lissu.He is not principled in mind. leo tena anataka haya yajibiwe wakati alisema kipindi cha kuelekea uchaguzi haya hujitokeza yapuuzwe.
 
Kwa kauli hii Lisu anatoa ujumbe kwamba umakamu mwenyekiti wake ni ceremonial (hauna meno), hivyo chama kinaongozwa na Mbowe tu.

Lisu kama kiongozi wa juu kabisa wa chama, kwanini hayo anataka yafanyike hajayafanya?
Nafikiri lissu ajiuzulu umakamu mwenyekiti awe mwachama wa kawaida kama anaona collective responsibility Ina muinflunce naye hapendi. Hii hali vinginevyo aendelee kuwa mnafikifi
 
Sema Yuko straight kuwa chama kinatakiwa kujibu yeye ndie kiongozi Namba mbili kitaifa kuwa yeye hawezi jibu ni direct message Kwa Mwenyekiti taifa kuwa ajibu Tuhuma Ake zinazohusu ufisadi wake wa Mali za chama kama Tuhuma za Msigwa zisemavyo
Kweli si vizuri myenyekiti kuacha kukujibu tuhuma inabidi aji u hiyo ni mojawapo ya damage control dhid ya tuhuma za msigwa
 
Kwa ufupi kwa Sasa ndani ya CHADEMA kuna ufa mkubwa. Na kwa yule asielewa maana utaona ni kwa nini juzi Ezekiah Wenje (Mmwenyekiti wa CHADEMA, kanda ya Ziwa) ametangaza rasmi kuwania nafasi ya Tundu Lissu (U-Makamu Mwenyeki Taifa).

Haya na tuendelee kuisoma picha🙂
 
Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa nje wana kazi gani wajibu kwa niaba ya Mwenyekiti kama wanavyofanya wenzao CCM. kumbukeni kelele zote hizi ni kwa vile chadema kinaisumbua Chama Tawala, jipangeni uchaguzi ni keshokutwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…