Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Mpumbavu ni yule anaesema ndani kuna simba alafu anaingia hivyohivyo bila tahadhali!

Lisu anasema tz kuna corona lakini yeye anapuyanga bila thadhali
 
Kimzaha mzaha chadema wanaweza wasipate mbunge hata mmoja. Magufuli leo kaenda kuchukua fomu nec, kaongea vizuri sana kama mgombea urais.
Lisu ana hasira, visasi na chuki kwa watanzania. Yeye amekwenda kenya leo, amepimwa lini corona huko kenya? Amewekwa karantini?.
Kweli akili za kuambiwa changanya na zako. Naishauri serikali lissu akitua Tanzania apimwe corona lakini pia awekwe karantini maana huko alipotoka hali si shwari.
 
Yaani sisi watanzania tuliofunga siku tatu tukalia na kuomba Mungu akasikia kilio chetu akatuondolea hili balaa la corona leo hii anakuja mtu mmoja tena anayetegemea kugombea nafasi ya raia number moja hapa nchini anatunanga na kubeza juhudi zetu na huruma ya Mungu! Kwa kweli inauma sana.
 
Hata mm nimeshangaa mm binafisi napenda wapinzani wawepo ili kuleta maendeleo, maana kama hakuna upinzani serikali iliyopo madarakani italala usingizi. Lakini nashauri upinzani linapokuja swala la utaifa wetu tuwe kitu kimoja, kama tundu lisu anaamini bado korona ipo kwanini anaendelea na mikusanyiko? Sio poa inatakiwa aseme ataifnyia nini inchi iwapo atachaguliwa,sio kuendekeza porojo za kitoto eti tz kuna korona na watu wanakufa mbona anaendelea na mikutano yake bila kuchukua tahadhari yoyote.
 
Sema makonda katolewa bila ivyo tundulisu angefikia karantin
 
Ama kweli ni aibu sana kwa vyombo vyetu vya habari hapa nchini.

Mtu aliyekuwa mbunge na aliyeshambuliwa kwa risasi zaidi ya 16 kama tembo mharibifu wa mazao na tishio la maisha ya binadamu.

Anarudi nyumbani mnashindwa hata kufanya naye interview kuhabarisha wananchi!
 
kwa sababu ni mda wa kampeni wacha tu waongee, sisi tunataka aongezewe mda atake asitake
 
Wakenya hao hao walikubali kumchangia damu mh Lissu wakati yupo mahututi wakati nyie mliwakataza watu kumchangia damu, hata watu kumuombea mliwakataza!

Kabla ya kuchangia lazima uwasiliane na ubongo wako kukumbuka yaliyo pita.
 
Wapinzani wa Tanzania bwana.

Sasa kama hali ni mbaya Kwanini alikusanya watu kipindi anatoka ulaya?

Kwanini bado wanaendelea kuwakusanya watu kwenye mikutano yao?

Kuna tatizo kubwa kwenye upinzani hasa Lissu na chama chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…