Naona ndugu Lissu anataka kupotosha watu na kutoa taarifa mbaya juu ya Tanzania.
Nataka Lisu atuambie kuwa wapi amekuta mgonjwa wa Covid-19 au wapi ameshuhudia mazishi ya mtu aliekufa na Corona. Toka amekuja TZ amekuwa akiisema vibaya sana nchi yetu. Ila amesahau wale walio mlaki pale Airport wote ni watanzania na hawakuwa na Corona.
Na wale wote walio kuwa kwenye mkutano wa Chadema na walikuwa hawana hata barakoa wote ni watanzania na hawana Corona. Wali walio mpokea singida jana pia ni Watanzania na hawana Corona. Au unataka kutuambia kuwa Covid-19 ina bagua watu wako unaotaka kukutana nao ndio wanakuwa hawana?
LISU, LISU, LISU watanzania sio wajinga kumbuka hao unaosema wana kufa kwa Covid-19 ndio unao kwenda kuwaomba kura kesho kutwa.
Kama unaipenda sana Covid-19 hamia Kenya ambapo kila siku ndio wanaitukuza. Hata ukiondoka sisi watanzania hatuta pungukiwa kitu. Ulikaa Ubeligiji hakuna alie kufuata ukaona urudishe miguu yako mwenyewe sasa usituchafulie nchi.