Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Hali ya Corona nchini inabadilika kwa maneno ya mtu?

Kwa hiyo mkibwabwaja Corona hamna inakwisha?

Hiiiii!
 
Tangu lini Meko na serikali take wakawahitaji hao waangalizi?

Huoni kwamba hiyo ndo fursa kwa chama chake cha mbogamboga?

By the way, waangalizi wawepo au wasiwepo, mkoloni mweusi lazima aondoke.
 
Aliyekuambia waangalizi wanakuja kwa niaba ya UPINZANI nani?

Waangalizi wanakuja kw ajaili ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
 
yaani ukiamka siku ya kupiga kura ukaenda kumpigia lissu ni bora ungelala tu maana utakuwa unailetea nchi matatizo huyo hafai kuwa rais kabisa
 
Huyo jamaa hakuna kitu hapo.. Hana fikira pana huyo anajua sheria tu Mambo mengine tupa kule! Tatizo ni kuwa mpinzani hivyo ye anapinga kila kitu. Kama Kuna korona mbona hakalishi kichwa chake nyumbani akae atulie!

Huyu mtu ni walewale tu wapiga kelele, Lissu mi najua ni debater au Challenger ila sio kiongozi na hilo wengi hawaelewi.
 
Mkuu Lissu anazidiwa na Lowassa aliyekuwa ameinunua Chadema, Yaani Kila ninaposikia speech zake nazidi kuisikitikia Chadema, Hivi anajua hofu iliyokuwa imetanda kwenye jamii kutokana na janga la Covid-19?

Hivi hajui kuwa asilimia kubwa ya watanzania ili waweze kujikimu lazima wazunguke hapa na pale wakati Covid-19 inapiga vita mizunguko? Mwanzo nilifikiri Lissu wanaweza kuwa mpinzani sahihi wa Jpm, kumbe hamna kitu.
 
Ahsante sana kwa kuliona hilo mkuu
 
Lissu amekuwa hajali na hachungi mdomo wake na hajali athari za anayoongea kwake wala chama chake, wala vyombo vya habari wala nchi.

Angalieni wenyewe, uongeaji wake pana Rais hapo? Hamna kitu.
Mkuu Yehodaya, kwanza with due respect, waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi hawaji kwa ajili ya upande wote, wanakuja kuangalia hatua zote za uchaguzi huru na wa haki zimefutwa.

Kuhusu wasiwasi wako kwa Lissu, usiwe na wasiwasi kabisa, trends zangu zinaelekeza mgombea wa pamoja wa opposition ni Benard Membe na sio Tundu Lissu!, Tundu Lissu ni pace maker tu!
P
 
Hali ya Corona nchini inabadilika kwa maneno ya mtu?

Kwa hiyo mkibwabwaja Corona hamna inakwisha?

Hiiiii!
Hawa watu wanatutafutia kutuingiza kwenye tanuru la umauti kisa kutafuta sifa tu.
 
Tangu lini Meko na serikali take wakawahitaji hao waangalizi?

Huoni kwamba hiyo ndo fursa kwa chama chake cha mbogamboga?

By the way, waangalizi wawepo au wasiwepo, mkoloni mweusi lazima aondoke.
Comment bora sana asubuhi hii
 
yaani ukiamka siku ya kupiga kura ukaenda kumpigia lissu ni bora ungelala tu maana utakuwa unailetea nchi matatizo huyo hafai kuwa rais kabisa
Mamillion ya watanzania wapo na mh Lissu, nyie bakieni na Bashite wenu
 
Aliyekuambia waangalizi wanakuja kwa niaba ya UPINZANI nani?

Waangalizi wanakuja kw ajaili ya kuhakikisha uchaguzi huru na wa haki.
kwenye maeneo ya chama tawala kimoja huwa waangalizi wa kimataifa hwaendi kutizama uchaguzi unaendaje

Nchi zenye vyama vingi ndio huenda Sasa Lisu kawaambia Tanzania Kuna Corona hawatakuja kabisa kawafukuza
 
Lisuu aachane na agenda ya corona.
Itampunguzia POINT.
hata kama corona ipo Tanzania yeye angekuwa ndo rais wa Tanzania angefanya nini KUPAMBANA na corona nchini?.


Sent from my SM-G928F using JamiiForums mobile app
 
Kwa kweli Tanzania democracy inazidi kukua mkuu, kwa sababu wananchi wameshakuwa na utambuzi juu ya watu wanaotafuta madaraka kwa masirahi binafsi.

Kwa kuwa MBOWE amemuchagua LISSU kurejesha RUZUKU isipotee.

Basi mnaamini kila mtu anaamin huyo MR. ROPOROPO kwa kila jambo ni mkombozi wa masikini.

Nazani bro @Pascally mayalla kanena vyema anabaki kuwa challenger na sio KIONGOZI kwa Taifa.
 
Mkuu Yehodaya, kwanza with due respect, waangalizi wa kimataifa wa uchaguzi hawaji kwa ajili ya upande wote, wanakuja kuangalia hatua zote za uchaguzi huru na wa haki zimefutwa.
Nchi zote zenye mfumo wa chama kimoja waangalizi wa kimataifa huwa hawaendi kuangalia chaguzi Kama ni huru na haki huenda nchi zenye vyama vingi tu
 
PAZIA 3,

Hapo kwenye corona ndo atatuchefua shenzi zake. Mbona havai barako? Mbona ana mikusanyiko ya kizembe sana watu kwa maelfu anawarundika sehemu moja? Mbona vikao vyao wamefanya bila tahadhari ya corona?

Lisu ni mgombea mzuri lkn kukataa kila approach ya Magufuri akidhani atampaisha ni ujinga sana. Leo hii tungekuwa tumefungiwa kama misukule ndani, corona inawatesa wakenya na taratiibu wanaanza kuchukua hatua za Tanzania.

Hapo anaharibu. Na angejua hao watu akili zao ni faytu wanawaza kutuzidi kila kitu na kututawala asingewaambia ya Tanzania
 
Naona ndugu Lissu anataka kupotosha watu na kutoa taarifa mbaya juu ya Tanzania.

Nataka Lisu atuambie kuwa wapi amekuta mgonjwa wa Covid-19 au wapi ameshuhudia mazishi ya mtu aliekufa na Corona. Toka amekuja TZ amekuwa akiisema vibaya sana nchi yetu. Ila amesahau wale walio mlaki pale Airport wote ni watanzania na hawakuwa na Corona.

Na wale wote walio kuwa kwenye mkutano wa Chadema na walikuwa hawana hata barakoa wote ni watanzania na hawana Corona. Wali walio mpokea singida jana pia ni Watanzania na hawana Corona. Au unataka kutuambia kuwa Covid-19 ina bagua watu wako unaotaka kukutana nao ndio wanakuwa hawana?

LISU, LISU, LISU watanzania sio wajinga kumbuka hao unaosema wana kufa kwa Covid-19 ndio unao kwenda kuwaomba kura kesho kutwa.

Kama unaipenda sana Covid-19 hamia Kenya ambapo kila siku ndio wanaitukuza. Hata ukiondoka sisi watanzania hatuta pungukiwa kitu. Ulikaa Ubeligiji hakuna alie kufuata ukaona urudishe miguu yako mwenyewe sasa usituchafulie nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…