Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

CHADEMA punguzeni papara na haraka zisizo na msingi wakati mnaandaa mikakati yenu mnawapa CCM hoja za kuwaonesha wananchi ninyi hamuitakii mema Tanzania na mnajali maslahi yenu tu na ya nchi jirani.

Unapokwenda kwenye vyombo vya habari vya nje ukasema watu wengi wanakufa kwa COVID-19 nchini kwako unasababisha kudorora kwa uchumi wa nchi yako kupitia sekta ya ANGA na UTALII.

Tumeona ile video jirani wanalialia watalii wote wa EAC sasa wanaenda Tanzania. Jamaa kwa kauli kama zile kwa lugha ile ya watalii (kiingereza)amerudisha juhudi za nchi yake nyuma kwa hatua 100.

Lissu ametumika na adui bila kujijua, ametekeleza na kupenyeza agenda ya adui kuidhuru nchi yake ambayo anaomba kuwa kiongozi mkuu wa hiyo nchi.

Leo Lissu 'katoa boko', mlitakiwa mumuandae mtangazaji wa KTN kwamba mnaomba msimuulize maswali Lissu kuhusu hiki na hiki.

Ni mawazo tu ya mtu mwenye njaa mtaani, kama vipi yapuuzieni muendelee na mtindo wenu huu wa kufanya vitu kwa kujibu mapigo bila kujipanga.

Ndugu Humprey Polepole tumieni vizuri hili boko alilotoa Lissu. Usaliti kwa nchi yako hautakiwi kwa gharama yoyote ile.
Nimesema hapa Lissu hafai kuwa raisi hata kwa mwezi mmoja tu na papara zake na mihemko.

TAFSIRI KWA WAZEE WETU: 'Kutoa boko' ni kufanya kitendo ambacho kina igharimu vibaya timu yako.
Lissu kachemka tena hana tofauti na Chief Mangungu.Wapiga kura ni watanzania sio wazungu au wakenya.
 
Magufuli ndio kaagiza atangazwe na hizo 5%?
Tena hata hizo kashazipunguza kwa uropokaji wake wa leo, Zitto aziwahi hizo zilizopungua kwa kukemea kitendo hicho cha TL cha leo vinginevyo watajikuta wanagawana hizo 5%.
 
anatatizo kubwa na kisaikolojia ambalo huwapata watu wa aina kama yake kibaya zaidi hata watu wake wa karb hawamwambii....

fikria tu kesho tuamke tunarais anaitwa tl.. unadhani nn kitatokea???
Ilipaswa wampeleke kutibiwa tatizo la kisaikolojia badala ya kumpa nafasi ya Urais.

Hapo alipo anataka kila mtu apigwe risasi Kama yeye, ndio maana hachungi kauli zake, anataka kuona machafuko, kuona watu wakiumia ndio itakua faraja yake.
 
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)


Ina maana huyu Lissu akishika dola atatufungia ndani kwaajili ya korona,titakoma afadhali tuendelee na Magu
 
Matusi na kashifa hazijengi mkuu, but siwezi kuwalaumu maana mgombea wenu break mdomoni kwake,chochote kikija kwake ni kuropoka tu


Turudi kwenye hoja,lissu hafai kuwa rais na hata kuwa kwa vyovyote vile iwavyo,huyu mtu no mbinafsi na mlafi wa madaraka na ataigawa nchi yetu na huenda hata ikaingia kwenye machafuko sababu ya huyu lissu

Watanzania hawapendi promo,wanapendA rais mchapa kazi kama ilivyo kwa JPM,

Harafu itakuwa ni maajabu kwa chama ambacho hakina uhakika wa kupata japo five MPs kutegemea kutoa rais wa kuiongoza nchi

Ni kweli hakina uhakika wa kupata japo 5%, leo tumeona jinsi tume ya uchaguzi ilivyokuwa inamtetemekea Magufuli. Hapo unatarajia wapate hata hiyo 5%?
 
Toka mwanzo nimesema ya kuwa CHADEMA kila siku inaendelea kujipotezea sifa kwa Aina ya watu wanao Wategemea

Tundu Lissu leo katika Mahojiano yake na KTN anakiri kuwa Tanzania hali ya corona ni mbaya jambo ambalo sio kweli tena anakiri mbele ya Taifa Ambalo siku zote limekua likijaribu kutuchafua katika sura ya Dunia.

Tundu Lissu anailaumu serikal kuwa inaficha Taarifa za janga la corona na kusema kuwa serikali haijachukua hatua na kusema kipindi hiki cha Corona mpaka kufikia uchaguzi hali itakua Mbaya Sana.
Vip wao kama chadema hawato endesha kampeni? Ili kuokoa Wafuas wao wengi kama wanajua kuelekea kampen Hali itakua mbaya?

Kwanini anayasema haya wakati yeye alipotoka ubelgij hakuvaa mask kujikinga wala hawakutoa ushauri wowote wa tahadhari.

Pia Tundu Lissu anasema watanzania hatuchukui Tahadhari yoyote ya kuachiana nafasi vipi kwao CHADEMA hizo nafasi wao Wana achiana?, au wao hawaugui corona?

Na vipi wao kama viongozi mbona hata siku moja hawaamrishi wafuasi wao kuachiana nafasi bali wanawaamrisha Tena kwa Nguvu nyingi Wakusanyike.

Tundu Lissu kumbuka unavyozidi kuichafua nchi hata ukiwa Rais jua tu utakua na kazi mbili, moja kuisafisha na nyingine kuikuza kiuchumi kazi ambayo itakua ngumu kwako.

Naomba Wanasiasa tuwe makini sana wakati huu wa kampeni heshima ya Tanzania ni muhimu sana kuliko kitu chochote,
tuache kuropoka tuongee.
 
Lisu katumwa na mabeberu huyu jamaa ataleta madhara makubwa Sana kiuchumi kwa Taifa letu hakika nawaambieni.

Katumwa na nani ww, kila akiongea hapa nchini anakatiwa sauti, sasa ngoja akaongee na vyombo vya watu wasiomsujidia kiongozi wa Tanzania. Hivi mnadhania kila mtu atakubali kuongozwa kikondoo?
 
Lissu.jpg
 
Magufuli ndio kaagiza atangazwe na hizo 5%?
Mkuu itakuwa ni aibu kubwa sana kwa taifa letu kumpa urais mtu mwenye ubinafsi,mlopokaji,hana staha wala uvumilivu,kila linalomwijia kwa bichwa lake yeye ni kulopoka tu.

Huyu urais atausikia kwenye bomba tu,na nawaambieni huyu kwa uchu wake wa madaraka anao uwezo wa kuanzisha hata vikundi vya uasi ili tu kuvuruga amani ya nchi

Najua fika hawezi kushinda anachofanya ni kutaka kuvuruga amani yetu,kwa aliyoyafanya ughaibuni yatosha .
 
Safi sana wakenya watampigia kura!

Nasikia pia hata wale wazungu milion 80 mliosema wamemfollow baada ya kuhojiwa hard talk nao watampigia kura,!
Kwani kuhojiwa na TV ya Kenya ndio kupigiwa kura na Wakenya?
Mbona uwezo wako unazidi kuwa upoloto?
Mahojiano ya Kenya yameonwa na maelfu ya Watanzania na wamejuwa kile ambacho TV station za TZ wanaogopa kwa kukosa Uhuru.
Kitakachotokea tena mahojiano hayo yatasambaa kwenye mitandao ya kijamii na WhatsApp na kila MTU ataona maswali ambayo hakuna mwandishi awezaye kuuliza hapa na hakuna mwanasiasa anaweza kujibu pia zaidi ya Lissu.
 
Back
Top Bottom