Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Tundu Lissu: Tunasikia taarifa watu wanakufa kwa Corona lakini haisemwi wazi. Serikali imerekebisha Sheria inayozuia kupeana taarifa

Mkuu Hawa jamaa mzee marehemu Mkapa aliwaita malofa na wapumbavu kwani alikosea hapana hakukosea hawa kweli ni malofa haswaa.
Usisahau kuwa BM kipindi cha hivi karibuni alitoa mapendekezo ya tume huru ya Uchaguzi yenye kutoa ushirikiano wa wazi wa kuhesabu kura kwa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
 
Kama we hujafa kwa corona basi haipo nchini

Huko ni kuwacheza shere na kuwadhihaki waliokufa au kufiwa na ndugu au jamaa kwenye janga hili.

Kauli yako ni yenye kuashiria dharau kwao ambapo kwa hakika ni ujinga uliopitiliza. Samahani lakini sikuweza kupata namna nyingine ya kukuelezea zaidi ya hiyo.

Pole lakini.
 
Muda mfupi mh Tundu Lissu atakuwa mbashara kuanzia saa 8: 00 mchana,Vituo vitakavyokuwa live Ni @standardKenya na @KTNNews, hii Ni kwamjibu wa Tumaini Makene

======
Mwandishi: Ulikuwaje mchakato wa kupona ulikuwaje?

Lissu: Asante kwa kushiriki kwenye kipindi chenu na kuongea na wananchi wa Kenya kuhusu mambo ya Tanzania, Nimekaa miezi minne Nairobi, nilipata huduma nzuri sana za kiafya kutoka kwa madaktari wa Kenya, nina damu nyingi ya wakenya inatembea kwenye mishapa yangu ya damu, nawashukuru watu wa Kenya kwa kuniangalia kwa miezi minne na baadae nikaenda Ubelgiji kutibiwa kwa miezi 11.

Mwandishi: Ulipoteza kiti chako bungeni wakati uko kwenye matibabu, ilikuwa halali kisiasa au kisheria?

Lissu: Wanasema sikuwepo bungeni lakini kila mtu anajua sikuwepo bungeni kwa sababu ya jaribio la mauaji September 2017. Wale waliojaribu kuniua kwa bunduki waliposhindwa ndio wakaamua kunipokonya siti yangu bungeni. Haikubaliki kibinadamu na kisheria labda kisiasa kwenye hesabu zao za siasa.

Mwandishi: Upinzani bado haujaungana kukikabili chama tawala cha CCM, kuna uwezekano wowote upinzani kuongea kwenye sauti moja?

Lissu: Nafikiri kwa upinzani umemaanisha chama changu cha CHADEMA na ACT- WAzalendo(Lissu amekatika). Tunafanyia kazi hilo, kuna baadhi ya mambo ya kisheria yanatakiwa kufanyiwa kazi na mitego ya kisheria.(Lissu amekatika).

Mwandishi: Tanzania imekuwa haitoi namba rasmi za Corona toka April 19, wapiga kura wakienda kupiga kura, tunawezaje kuwalinda wakati wa mchakato wa upigaji kura, kitu gani kitakuwa tofauti kwenye mchakato ambacho kitawalinda?

Lissu: Hili ni suala ambalo linatufikirisha, tuko katikati ya gonjwa la mlipuko lakini serikali yetu imesema wazi kwa dunia kwamba hakuna corona hivyo Rais aliposema hakuna shida wananchi wamefata, watu hawaachi nafasi baina ya mtu na mtu, litakuwa tatizo kubwa kutoka sasa mpaka uchaguzi mkuu. Napenda kuwaomba wananchi wa Tanzania kuamika silika zao na wafanye maamuzi yao hasa kutokana na Rais kutolikubali hili gonjwa.

Nawaomba wananchi wapeane nafasi, wavae barakoa, wanawe mikono na kufanya vyote ambavyo wataalam wamewaelekeza kuepuka maambukizi ya korona.

Mwandishi: Tukiongelea Covid19, unaweza kutupa picha gani kutoka nchini kwako?

Ni picha inayohuzunisha, tunasikia taarifa watu wanakufa kwa corona lakini haviongelewi wazi, serikali imerekebisha sheria ya mitandao inayozuia kupeana taarifa kuhusu huu ugonjwa, ukisema unavunja sheria na unaweza kufungwa. Wananchi wafanye maamuzi yao na wasisikilize ushauri mbaya wa watu kutoka serikali kwamba hamna tatizo, corona inaua na ipo Tanzania.

Mwandishi: Unaongeleaje haki za binadamu?

Lissu: Rekodi ya haki za binadabu Tanzania ni janga, hii miaka mitano tumeona historia mbaya zaidi katika historia yetu yote.(Lissu amekatika)


Kungekuwa na korona wangerundikana hivyo kama panya wakati wanampokea na kwenye vikao vyao?
 
Usisahau kuwa BM kipindi cha hivi karibuni alitoa mapendekezo ya tume huru ya Uchaguzi yenye kutoa ushirikiano wa wazi wa kuhesabu kura kwa vyama vya upinzani nchini Tanzania.
Lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba aliwaita ni malofa na wapumbavu.

Naamini matendo yenu yalimsukuma kuwaita hivyo.
 
Ilipaswa wampeleke kutibiwa tatizo la kisaikolojia badala ya kumpa nafasi ya Urais.

Hapo alipo anataka kila mtu apigwe risasi Kama yeye, ndio maana hachungi kauli zake, anataka kuona machafuko, kuona watu wakiumia ndio itakua faraja yake.
ukimtafakari sana unaona kabisa waliompitisha na unajiuliza waliompisha hawakulijua hili...?
 
Hata kama corona bado ipo hakutakiwa kukiri wazi. Hii kauli itampa wakati mgumu kwenye kampeni. Atafanyaje kampeni kama kuna corona? Halafu anatakiwa asome upepo, watanzania kwa sasa wanafurahia maisha ya kuishi bila hofu ya corona. Watu hatupendi kuvaa mibarakoa hivyo kutuambia bado corona ipo ni kutukosesha furaha. Nashauri aachane kabisa na habari za korona zitamshushia umaarufu.
 
TL yuko sahihi! Lini serikali ilitoa taarifa kuwa Hakuna corona!!? Nilini serikali ilieleza kuwa hakuna wangonjwa kabisa na hakuna watu wanaokufa kwa corona. Ikiwa JPM alisema Corana tuendelea kuishi nayo maana ni ugonjwa kama magonjwa mengine ulitaka TL aseme Hakuna Corona??

TL yuko sahihi.
 
Lakini hiyo haiondoi ukweli kwamba aliwaita ni malofa na wapumbavu.

Naamini matendo yenu yalimsukuma kuwaita hivyo.
"matendo yenu"??!!

Jaribu kutafiti kuwa aliwaita wapinzani hivyo lini na hiki nilichokisema alikifanya lini.

Kama aliwaita majina hayo hapo kabla lakini baadaye akaja kutaka maridhiano nao hasa katika masuala ya Uchaguzi, wewe unapata fundisho gani hapo?
 
Kaharibu balaa, ajirekebishe, tusemane humu ndani ila tukitoka hapa tuwaseme wao. Shuubat, tumekusamehe usirudie tena, ukirudia tutaamini kuwa hujapona[emoji31][emoji51][emoji51][emoji51]
 
TL yuko sahihi! Lini serikali ilitoa taarifa kuwa Hakuna corona!!? Nilini serikali ilieleza kuwa hakuna wangonjwa kabisa na hakuna watu wanaokufa kwa corona. Ikiwa JPM alisema Corana tuendelea kuishi nayo maana ni ugonjwa kama magonjwa mengine ulitaka TL aseme Hakuna Corona??

TL yuko sahihi.
Mnashindana kutangaza so what? Watu kibao wanakufa kwa malaria, tb, HIV nk mbona hamtangazi! Acheni kushikiwa akili na watu
 
Kuna mtu anasema amenunua ndege kwa keshi na haoni mtanzania mwingine anaweza kufanya hivyo,Sasa sijui kesho corona ikimchukua ndo utakuwa mwisho wa nchi hii? Kwa kweli kuwa uyaone
Hakuna mwingine. Ndio ukweli wenyewe.
 
Halafu usishangae akarudia, mimi nasema kama ana sera tupo tayari kumsikiliza humu ndani ila akijichanganya tunamdiss, ni mimi mwananchi mwenye msimamo mkali linapokuja swala la nchi yangu.
 
Back
Top Bottom