chinchilla coat
JF-Expert Member
- May 16, 2016
- 5,107
- 10,969
Kipindi hicho WaTanzania hawakua waoga na waliungana na Nyerere, leo hii unaona wa Tanzania kama hao?Elimu ya kuunga-unga ndiyo inaimaliza Tanzania. Unajua au umewahi kusoma historia yoyote ya ukombozi? Unadhani kina Nyerere wangekuwa wana mawazo mgando na ya kioga namna hii uhuru ungepatikana?
Tundu Lissu hakuwa mwoga, alipingana na Magufuli kwa hoja, kilichonkuta unakifahamu, Watanzania walionyesha reaction gani?
Uchaguzi wa S/Mitaa ulifanywa kihuni kabisa hadharani hadi CCM wengi wanakiri, Wa Tanzania walifanya nini? Uchaguzi Mkuu hivyo hivyo, je kulikuwa na reaction gani?
Kama yote hayo yalitokea hakukua na reaction yoyote, Mbowe akiendelea kukaa gerezani kutakuwa na reaction gani ya maana?