Mkuu hizo ni silaha za ccm, sasa hutakiwi kuzitoa mapema ili wabuni 'mbinu' mpya.
Hakuna cha mtandao wa kujenga hapo, ni elimu ya siku 3 tu kwa mawakala wanaiva.
Mawakala wapo kibao na kuna mbinu kadha wa kadha za kudhibiti wakala asinunuliwe sema hapo Lissu hawezi kuweka wazi ni siri hiyo. Lissu kwa mfano amekuwa akitumia mawakala ambao ni std vii tu lakini ccm hawajawahi muibia hata kura moja.
Sio jambo kubwa au gumu kulitekeleza, na kila mgombea ubunge wa Chadema na viongozi wanaelewa cha kufanya sio kwamba Lissu ndio ataenda nchi nzima. Kwa hiyo muda bado unatosha sana.