Ama kweli:
KNOWLEDGE IS POWER.
Kama haya ndiyo matusi tunayoambiwa na kina Makonda, basi iko shida mahali bila shaka.
Yaani ukweli kwa hawa ndugu zetu, kwao ni matusi.
=============
Tukirudi kwenye mada kumhusu huyu mwamba.
Kwamba, haina shaka kuwa anaijua historia ya Tanganyika na Tanzania kila anapokwenda.
Amejaa ufahamu na maarifa ya kutosha. Watu wa namna hii hawafungwi wala hawadanganyiki. Wajinga na wasio na ufahamu ndio huonewa na kunyanyaswa.
Mtu hachoki kumsikiliza Tundu Lissu anapotoa elimu ya uraia kwa watu.
Anatumia lugha rahisi yenye "authority" na ya kueleweka na kila mtu wa ulewa wowote kwa urahisi kabisa.
View attachment 2975995
Kwa ufupi yaliyomo ktk video:
Hapa anaongelea ma - Rais wezi wanaolindwa na mfumo mbovu wa kikatiba ya mwaka 1977.
Anauliza wananchi swali hili linalogonga akili zao sawasawa, kwamba; "
Hivi mkiwa na Rais mwizi mnawezaje kupona?"
Anasema, Rais akiwa kinga ya kutoshitakiwa kwa matendo maovu kama wizi, hata hawa huku chini mawaziri, wabunge, ma - RCs, DCs, Wakurugenzi nk nao watakuwa wezi vilevile.
Anaendelea kusema kuwa, katiba ikiondoa kinga ya Rais tu kutokuwa mwizi, hawa wengine wote huku chini hawatakuwa na wizi wa kimfumo kama ilivyo sasa.
Anawapandia mbegu ya ujasiri watu wa Babati mpaka wanamfurahia.
Amwongolea pia
Herman Sarwatt aliyewahi kuwa mbunge binafsi asiye na chama, machachari wa jimbo la Mbulu miaka ya 1960 - 1965 chini ya chama kimoja - TANU.
Huyu (Herman Sarwatt) alipambana na mwenzake Dodo kuwania ubunge jimbo la Mbulu wote kwa tiketi ya TANU.
Kwa sababu ya misimamo mikali ya kutopenda uchawa, TANU ya Nyerere ilikata jina la Herman Sarwatt. Kuona hivyo, Herman Sarwatt hakukata tamaa. Wakati huo katiba ilikuwa inaruhusu mtu kusimama kama mgombea binafsi.
Herman Srwatt akagombea kama mgombea binafsi na kushinda.
Nyerere alienda Mbulu kumpigia kampeni Dodo na TANU. Hakuweza kumsaidia. Dodo na TANU yake na kwa msaada wa Nyerere alibwagwa chini na Herman Sarwatt.
Kwa uzuri zaidi hebu tazama na sikiliza mwenyewe kwa umakini video clip hii upate ufahamu.