Tundu Lissu: Ukiwa na Rais mwizi mnawezaje kuwa salama? Katiba bora ni kuzuia Marais wezi

Tundu Lissu: Ukiwa na Rais mwizi mnawezaje kuwa salama? Katiba bora ni kuzuia Marais wezi

narudia tena,
there is nothing, mercenaries and puppets can do in this country against very able and united Tanzanians Patriots 🐒
Mkuu naamini ndo umeanza kujifunza kiingereza. Inaonekana unakipenda bahati mbaya chenyewe kinakukataa.
 
Kwa uungwana mkubwa raisi wetu aliruhusu mikutano ya hadhara na maandamano kwa vyama vya siasa nchini ili viweze kujijenga.

Lakini masharti ya ruhusa hiyo ilikuwa vyama hivyo vikafanye siasa za kiustaarabu. Hili alilisisitiza sana mheshimiwa raisi. Lakini kwa masikitiko makubwa Tundu Lissu amelipuuza agizo hili muhimu la raisi na kuendelea na siasa zake za uchochezi, ubaguzi, maudhi, matusi etc. Mwenyekiti wake Mh. Mbowe yeye kalizingatia sharti hilo vizuri na anafanya siasa za kistaarabu na za kuheshimiana, akijenga hoja zake kwa ustadi mkubwa bila kuudhi mtu ye yote. ACT wazalendo na CUF nao wanafanya siasa za kistaarabu kwa ustadi mkubwa.

Sasa kipi kifanyike kumunyoosha Tundu Lisu kumrudisha kwenye mstali sahihi? Akiachwa hivyo ataivuruga nchi na kuleta machafuko kama yale ya Sudani na kwingineko tunayoyaona. Demokrasia haina maana hiyo. Tunajua watoto wake wako Amerika (wana uraia wa Marekani) na mke wake yuko Ubeligiji. Akikinukisha hapa yeye haraka atakwenda Amerika au Ubelgiji, sisi atatuacha tukiumizana.
Nikumbushe: ccm inaungwa mkono zaidi na ......
Wapinzani (Chadema) wanaungwa mkono zaidi na .....
 
there is no where mercenaries and puppets can be given a chance to represent their masters in our land Mama Tanzania.

no way 🐒
Mamluki unaowasema ndo hao waliopo madarakani wanaoza Hadi malango ya nchi kama vile bandari na yaweza kuwa unatete huu upumbav kisa shemeji Yako ni katibu tarafa wa ccm huko Ikwingwifu
 
Mamluki unaowasema ndo hao waliopo madarakani wanaoza Hadi malango ya nchi kama vile bandari na yaweza kuwa unatete huu upumbav kisa shemeji Yako ni katibu tarafa wa ccm huko Ikwingwifu
mihemko ni hatari kwa afya ya akili na moyo wako,
kua muungwana tu kwenye mambo haya utaelewa na kuyafahamu vizuri 🐒

mtanzania yeyote ana haki ya kutoa maoni na mtazamo dhidi mambo mbalimbali kadiri anavyoona inafaa....

lakini mtanzania yeyote mwenye sifa na vigezo stahiki anastahili kua kiongozi iwe wa kata, kijiji ama vinginevyo bila kujali chama chake cha kisiasa 🐒

na kwahivyo,
nikuhakikishie tu kwamba,
mamluki na vibaraka wa mabwenyenye ambao umeungana nao, wanadhibitika kirahisi sana kama vile kudhibiti kundi kubwa sana la nyumbu, bila tashwishwi yoyote 🐒
 
Katiba ni Sheria na kama Sheria hata zilizopo zinapindishwa basi ndio hivyo.... utawapeleka Mahakamani lakini mwisho wa siku ndio hivyo....

Kinachohitajika ni utamaduni wa wananchi kuchukia wizi na kuona ufisadi sio jambo jema as of now mtu akiiba ukishangaa jamii inakuona una wivu...., Siasa imekuwa ni sehemu ya kuchuma, wezi / wizi ndio ujanja wakati zamani ilikuwa ni aibu...
 
wakweli huwa wanapigwa sana vita Duniani !
Sijui ni kwanini !!!!

tangu zama na zama iko vile 🙄😱🙄
 
Mercenaries (mamluki wa mabeberu) ni wale waliokwisha kuuza na kugawa rasrimali asili zetu zote Watanganganyika kwa wageni wa mataifa ya nje kwa mikataba ya kichifu - Magungo kama vile wajinga ambao hawajawahi kwenda shule kabisa.

Hawa si wengine bali ni CCM wote ukiwemo wewe Tlaatlaah walio tayari kuuza nchi hii, utu wao na ndugu zao kwa mabeberu wa Ulaya na Uarabuni kwa sababu ya tamaa ya fedha na kutaka kujaza matumbo yao tu.

Na kwa sababu ya kutojua kwako au kwa makusudi tu kwa sababu unanufaika ktk namna fulani, basi kutwa nzima unawatetea na kulamba viatu vya mercenaries hawa Ili mradi ulipwe ujira kidogo.

Acha kulamba viatu vya kina Samia wewe. Jiunge na wapigania uhuru wenzako toka kwa mkoloni mweusi - CCM ili tutengeneze mfumo bora wa kikatiba na kisheria wa kutuwezesha kujitawala kwa haki na kugawana keki ya taifa hili kwa usawa.

Otherwise, kama unajiweka mbali na wanaopinga mfumo huu wa utawala kandamizi, usio haki, maana yake unajipa mwenyewe tiketi ya kuwa mlamba viatu vya kina Samia Suluhu Hassan na wenzake walio kwenye prestigious political positions za chako chako.!

Amka Tlaatlaah.

Huo ubunge unaoutafuta kwa kujidhalilisha na kulamba viatu vya bwana zako hao, unaweza kuupata kirahisi bila gharama ya kuuza utu wako kwa kina Paul Makonda wahalifu walioshindikana iwapo tutafanikiwa kuweka mazingira na mfumo bora wa uchaguzi na mgawanyo wa rasrimali zetu.
Duh 🙄 !
Hatar sana 🙏🙏 !
 
Ndio maana CCM wanamuogopa sana Tundu Lissu.

Hawangependa kabisa kumuona anasimama kugombea kiti cha Rais na mtu wao yeyote watakayemweka.

Na wakirogwa wamweke huyu mama, atachanwachanwa mpaka watamhurumia!
hizo ni ndoto za mchana huwezi kushindana na mtu anayeshika dola hata awe anapendwa kaisi gani mama anamchana mchana kweupeee watu wanarudi ikulu anabaki analalama tu huko kama mtu aliyefumaniwa akioga nje lisu hana lolote ni maneno matupu
 
Ama kweli: KNOWLEDGE IS POWER.

Kama haya ndiyo matusi tunayoambiwa na kina Makonda, basi iko shida mahali bila shaka.

Yaani ukweli kwa hawa ndugu zetu, kwao ni matusi.

=============

Tukirudi kwenye mada kumhusu huyu mwamba.

Kwamba, haina shaka kuwa anaijua historia ya Tanganyika na Tanzania kila anapokwenda.

Amejaa ufahamu na maarifa ya kutosha. Watu wa namna hii hawafungwi wala hawadanganyiki. Wajinga na wasio na ufahamu ndio huonewa na kunyanyaswa.

Mtu hachoki kumsikiliza Tundu Lissu anapotoa elimu ya uraia kwa watu.

Anatumia lugha rahisi yenye "authority" na ya kueleweka na kila mtu wa ulewa wowote kwa urahisi kabisa.

View attachment 2975995
Kwa ufupi yaliyomo ktk video:

Hapa anaongelea ma - Rais wezi wanaolindwa na mfumo mbovu wa kikatiba ya mwaka 1977.

Anauliza wananchi swali hili linalogonga akili zao sawasawa, kwamba; "Hivi mkiwa na Rais mwizi mnawezaje kupona?"

Anasema, Rais akiwa kinga ya kutoshitakiwa kwa matendo maovu kama wizi, hata hawa huku chini mawaziri, wabunge, ma - RCs, DCs, Wakurugenzi nk nao watakuwa wezi vilevile.

Anaendelea kusema kuwa, katiba ikiondoa kinga ya Rais tu kutokuwa mwizi, hawa wengine wote huku chini hawatakuwa na wizi wa kimfumo kama ilivyo sasa.

Anawapandia mbegu ya ujasiri watu wa Babati mpaka wanamfurahia.

Amwongolea pia Herman Sarwatt aliyewahi kuwa mbunge binafsi asiye na chama, machachari wa jimbo la Mbulu miaka ya 1960 - 1965 chini ya chama kimoja - TANU.

Huyu (Herman Sarwatt) alipambana na mwenzake Dodo kuwania ubunge jimbo la Mbulu wote kwa tiketi ya TANU.

Kwa sababu ya misimamo mikali ya kutopenda uchawa, TANU ya Nyerere ilikata jina la Herman Sarwatt. Kuona hivyo, Herman Sarwatt hakukata tamaa. Wakati huo katiba ilikuwa inaruhusu mtu kusimama kama mgombea binafsi.

Herman Srwatt akagombea kama mgombea binafsi na kushinda.

Nyerere alienda Mbulu kumpigia kampeni Dodo na TANU. Hakuweza kumsaidia. Dodo na TANU yake na kwa msaada wa Nyerere alibwagwa chini na Herman Sarwatt.

Kwa uzuri zaidi hebu tazama na sikiliza mwenyewe kwa umakini video clip hii upate ufahamu.
Huyu jamaa ni akili kubwa.......hawa ndio tunawaita visionary leader ambao taifa letu linawahitaji kwa udi na uvumba.
 
Mercenaries (mamluki wa mabeberu) ni wale waliokwisha kuuza na kugawa rasrimali asili zetu zote Watanganganyika kwa wageni wa mataifa ya nje kwa mikataba ya kichifu - Magungo kama vile wajinga ambao hawajawahi kwenda shule kabisa.

Hawa si wengine bali ni CCM wote ukiwemo wewe Tlaatlaah walio tayari kuuza nchi hii, utu wao na ndugu zao kwa mabeberu wa Ulaya na Uarabuni kwa sababu ya tamaa ya fedha na kutaka kujaza matumbo yao tu.

Na kwa sababu ya kutojua kwako au kwa makusudi tu kwa sababu unanufaika ktk namna fulani, basi kutwa nzima unawatetea na kulamba viatu vya mercenaries hawa Ili mradi ulipwe ujira kidogo.

Acha kulamba viatu vya kina Samia wewe. Jiunge na wapigania uhuru wenzako toka kwa mkoloni mweusi - CCM ili tutengeneze mfumo bora wa kikatiba na kisheria wa kutuwezesha kujitawala kwa haki na kugawana keki ya taifa hili kwa usawa.

Otherwise, kama unajiweka mbali na wanaopinga mfumo huu wa utawala kandamizi, usio haki, maana yake unajipa mwenyewe tiketi ya kuwa mlamba viatu vya kina Samia Suluhu Hassan na wenzake walio kwenye prestigious political positions za chako chako.!

Amka Tlaatlaah.

Huo ubunge unaoutafuta kwa kujidhalilisha na kulamba viatu vya bwana zako hao, unaweza kuupata kirahisi bila gharama ya kuuza utu wako kwa kina Paul Makonda wahalifu walioshindikana iwapo tutafanikiwa kuweka mazingira na mfumo bora wa uchaguzi na mgawanyo wa rasrimali zetu.
Umemjibu kwa ufasaha na ustadi mkubwa sana......kazi kwake
 
Back
Top Bottom