Tundu Lissu: Wakati mnajadili kujiuzulu kwa Spika Ndugai, mwenzenu He's laughing all the way to the Bank. Anaondoka akiwa tajiri

Tundu Lissu: Wakati mnajadili kujiuzulu kwa Spika Ndugai, mwenzenu He's laughing all the way to the Bank. Anaondoka akiwa tajiri

The Palm Tree

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
7,951
Reaction score
12,541
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Watumishi wa Kisiasa [Political Service Benefit Act] iliyotungwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Hayati Benjamin W. Mkapa, mstaafu huyu wa "kujiuzuru kwa kulazimishwa" yuko entitled kupata mafao yafuatayo;

1. Kiinua Mgongo [Gratuity] cha 50% ya pesa zote alizowahi kulipwa kama mshahara wakati wote akiwa Spika [2015 - January, 2022]...

2. Malipo ya pensheni 80% ya mshahara wa Spika kwa wakati huo/wa sasa...

3. Winding up Allowance: Ambayo ni malipo ya mkupuo ya mishahara yake ya miaka miwili [miezi 24] - February 2022 hadi February 2024..!

4. Gari mpya [brand new] moja ya chaguo lake [obviously itakuwa Toyota Land Cruiser V8]....

5. Personal Driver: Huyu ni mwajiriwa wa serikali na atakuwa analipwa na serikali maisha yake yote hadi boss atakapokufa...

6. Lita 70 za mafuta ya gari kila wiki sawa na lita 280 kila mwezi: Hii ni kwa ajili ya Gari yake aliyonunuliwa na serikali...

7. Fedha taslimu 40% ya thamani ya bei ya mafuta anayopata kila mwezi i.e Lita 280: Hii inaitwa vehicle maintenance allowance kila mwezi...

8. Diplomatic Passport for him & his Spouse: Kwa maisha yao yote hadi watakapokufa...

9. Atapewa/kujengewa nyumba ya thamani ya chaguo lake....!

NOTE:
1. Sheria hii inawataja hawa "Viongozi walio katika Utumishi wa kisiasa" kuwa ni: Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, mawaziri, makatibu wakuu, manaibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya nk

2. Kinachowatofautisha hawa wote ni AINA na VIWANGO vya mafao [benefits]. Wanaofaidika na kulundikiwa mafao mazuri na ya kufuru zaidi ni Rais, VP, PM, Mawaziri...

3. TUNDU LISSU alimaliza kutoa maelezo ya elimu na ufafanuzi wake akijibu swali hili kwa wasikiliizaji na wachangiaji wa mjadala huo kwa kusema...

"....Wakati nyie mkishangilia na kulumbana mitandao oh amejiuzuru, mwenzenu IS LAUGHING ALL THE WAY TO THE BANK . Hili lijamaa limeondoka lakini likiwa litajiri kwelikweli...!!"

Akauliza, mnadhani ni kwanini CCM wanang'ang'ani madaraka, hawataki kuondoka madarakani kwa njia za Amani hata kutupiga risasi sisi wengine (yeye TL)...?

Alijijibu kwa kusema: Ni kwa sababu hii....ULAJI..!!
 
Matumizi ya lugha ya Lissu yanaongeza hatred miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania, kwa mtazamo wangu hata kama alifanyiwa ubaya lakini akiendeleza ubaya huo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko alichofanyiwa yeye matokeo yake ni yapi?

Napenda kumuona Lissu akijiweka zaidi kwenye personality ya kiongozi wa Chadema, aache matumizi ya maneno kama "lin'gombe" kwa binadamu wengine haya yanakishushia hadhi chama, achague maneno.

Anayo brain ya kutengeneza hoja zenye ushawishi, na anajua namna ya kufikisha ujumbe wake kwa walengwa kwa mpangilio mzuri wa maandiko yake na matumizi ya alama, vyote vikiongezwa na elimu yake, aitumie hii silaha kubwa zaidi na nzuri zaidi.

Maneno haya ya hovyo atuachie mashabiki huku mitaani na mitandaoni, lakini kwa level yake sipendelei, ikitokea kesho akiwa mwenyekiti akaendeleza hii tabia atakifanya chama kionekane cha waropokaji.
 
Matumizi ya lugha ya Lissu yanaongeza hatred miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania, kwa mtazamo wangu hata kama alifanyiwa ubaya lakini akiendeleza ubaya huo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko alichofanyiwa yeye matokeo yake ni yapi...
Ndio baba yako, kaka yako au ww mwenyew in reality umeshindiliwa bullets za kutosha ili ufe. Then kibinadam kbs ni ngumu sana kutoumia kila ukikumbuka. Sometimes huez mlaumu kwa madhira aliyopitia still hata hakuna aliejali kuchukua hatua, Tafakari mkuu!!!
 
Matumizi ya lugha ya Lissu yanaongeza hatred miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania, kwa mtazamo wangu hata kama alifanyiwa ubaya lakini akiendeleza ubaya huo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko alichofanyiwa yeye matokeo yake ni yapi...
Unaposema Kesho Akiwa mwenyekiti unataka kuhalalisha nini?
 
Matumizi ya lugha ya Lissu yanaongeza hatred miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania, kwa mtazamo wangu hata kama alifanyiwa ubaya lakini akiendeleza ubaya huo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko alichofanyiwa yeye matokeo yake ni yapi...

Ifike mahala hata ninyi wanachama muyaelewe hayo maneno kwamba yanafaa kutumika ili kutia msisitizo wa hoja maana hata hao ambao wako against na nyie kuna wakati wanatumia maneno kama hayo hayo.

Sikiliza ule wimbo wa CCM mbele kwa mbele kuna maneno kama “waache waandamane wajinga wale” nikusema jambo ambalo kikatiba linajulikana watu timamu wakilifanya ni wajinga?

Mimi naona yupo sawa asimtukane tu mtu matusi ya nguoni.
 
Hii CCM ni Sawa na shetani mweusi .sielewi Kwa nini alipwe % ya mshahara badala ya contribution alofanya yeye na mwajiri wake wakati wa service yake .katiba mpya ni muhimu aisee
 
Matumizi ya lugha ya Lissu yanaongeza hatred miongoni mwa wanasiasa wa Tanzania, kwa mtazamo wangu hata kama alifanyiwa ubaya lakini akiendeleza ubaya huo hata kama kwa kiwango kidogo kuliko alichofanyiwa yeye matokeo yake ni yapi...
Petty issues
 
Kwa mujibu wa Sheria ya Mafao ya Watumishi wa Kisiasa [Political Service Benefit Act] iliyotungwa wakati wa serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Hayati Benjamin W. Mkapa, mstaafu huyu wa "kujiuzuru kwa kulazimishwa" yuko entitled kupata mafao yafuatayo...
Kweli linaondoka likiwa Tajiri. Lakini lingeondoka Tajiri zaidi kama lingeondoka 2025. Kama ni kupoteza bado limepoteza na limeondoka kwa aibu.... Hiyo Siyo nusu Shari ni Shari kamili.

Sidhani kama kulikuwa na uwezekano wa kumfukuza na kumkosesha hayo maslahi unless wamfukuze chama halafu wamnyime maslahi yake kama walivyomfanyia Mrema.
 
Hayo mafao kwa aliyelazimishwa kustaafu tu au hata wale wanaostaafu kwa mujibu wa sheria???

Vipi na wale wanaotumbuliwa na wanyewe wanapata mafao kama hayo??
 
Back
Top Bottom