Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Safi,Hatimaye majambazi ya nchi yajulikana, ni hatua nzuri kuelekea kurudi nyumbani,Haiwezekani mamlaka zinapiga chenga za uchunguzi mwaka wa tano huu

Kama wana nia ya dhati waanze na hizo taarifa,halafu akirudi akachukue gari yake

Nchi iliendeshwa kihuni sana na yule Jiwe alikuwa kiongozi wa hovyo mno ,Huyo balozi akamatwe haraka
 
Sasa Brother si arudi tu aifie nchi. Kapitia magumu, lakini ndio wito wake.
 
Tundu Lissu sio sawa na Watanzania wengine, huyu ni mtu aliyeshambaliwa kwa risasi 16 katika majengo wanayoishi viongozi wa serikali. Lazima kuwepo na namna tofauti ya kushughulika na ulinzi wake kwa kuzingatia waliomshambuliwa bado hawajakamatwa, wako huko mitaani.
Tundu Lissu aweke mezani ulinzi anaoutaka tuuelewe. Maana this is too much demanding.

Labda anataka awe protected kama Marais wastaafu maana apart of protection ya Rais na viongozi wengine wakuu, Watanzania wengine hatulindwi
 
Ni kweli kabisa, tena alirudi kipindi ambacho anayedai mtesi wake Magufuli alikuwa bado yuko hai na bado akiwa rais.

Kama hakuogopa kurudi awamu ya mtesi wake, anaogopa nini kurudi awamu ya aliyemwona kwa amani Nairobi na Ubelgiji?

Hivi mnaotaka arudi bila kuhakikishiwa usalama na wenye mamlaka yao mna agenda gani naye ndugu?
 

Mbona Lowassa yupo CCM na mtoto wake Ni mbunge, na upo comfortable. Kwa hivyo Lowassa kuja CDM ndio ihalallishe Lissu kupigwa risasi?.

Chadema Ni chama Cha siasa kinachotaka kuingia madarakani na mwanasiasa wa 2015 aliyeweza kuwa na nguvu alikuwa Ni Lowassa. Kwa Mara ya kwanza upinzani ulipata 40 percent ya kura zote pamoja na wizi uliofanyika. Chadema waliangalia political interests na sio CCM interests.

Kama Lowassa mbaya Sana mbona yupo CCM na mmekaa naye huko?. Acheni unafiki wa kuilaumu chadema inapofanya maamuzi magumu halafu baadae mnaitukana. Mbona aligombea Mbowe, Dr Slaa na Wala hamkuwachagua?. Wameleta Lowassa kelele zimekuwa nyingi.

Kama kupigwa risasi Lissu kwako unaona haina maana kwanini uwe na uchungu kwa CHADEMA kumpokea Lowassa Kama sio uongo na unafiki.
 
Nimeaikia audio clip ikitambaa ndani ya jamvi letu ambalo ndipo mahala pekee palipobakia hapa nchini kujieleza kwa uhuru.

Umefafanua vizuri kabisa kuwa ni kikosi kazi cha Tiss chini ya Modestus Kipilomba kilikupiga risasi na kilihusika kufanya mauaji ya watu mbalimbali hapa nchini.

Ni wakati wa wewe kurudi nchini ili ifunguliwe Criminal application ili kuomba mahakama kuu imsurutishe Dpp awafungulie kesi wahusika.

Hakuna aliye juu ya sheria hapa Tanzania.
 
Taifa lenye kujielewa haliwekezi kuua Raia wake, bali huwalinda kwa kila namna pasipo kujali tofauti zao.

Sasa Rais kinachomfanya ashindwe kumpa guarantee ya usalama wake ni nini kama kweli hawana nia ovu?

unachekesha sana!.
kuna kauli inasema msela na mshenzi namba moja ni serikali.
sasa huko ulaya uwaga usikii mambo kama haya kwa wanaharakati,wasema ukweli,wapingaji.
basi ni kusaidie ukasimulie hata wanao:
*uganda kaangalie
*rwanda,kenya,south africa
hizo nchi nimekupa za karibu tuje huko kwa putin ndo kabisa.

wewe acha ujinga kwa vile hayaja kukuta
 
Wakati anagombea Urais alikuwa na ulinzi maalum na kulikuwa na macho makali ya mabeberu kwake.
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana...
Kwa hiki alichokizungumza sasa hivi tayari ameshajiondolea uwezekano wa kurudi Tanzania, 'mark my words

Unatarajia watamwacha?

Rais anayemtaja kwamba awashughulikie kikosi kazi kilichohusika kumpiga risasi hapo ndipo panaitwa 'DEEP SEA WATER' Je, anaweza kuogelea kuwagusa kwa namna yoyote?

Amemchonganisha, akifanya kitendo chochote kitakachowagusa hao anaodhani ndio walimshambulia kuna nyama itararuliwa hadharani kuthibitisha na yeye aliishirki kikao na kubariki, hapo ndipo vumbi litatimka na kindumbwendumwe kuanza rasmi.
 
Kwani kuna mashindano ya nani ni nani kwenye katiba mpya? Mbona hata Mukandara, Zitto, Pole pole au hata wewe ungekuwa na uzalendo tungemwuunga mkono tu?
Atulie sasa watu wako kwenye jambo zito la kitaifa litakalo komesha hayo matendo aliyofanyiwa yeye na wengine.
 
Afungue yeye case au serekali kama ilivyo ada?

Hakuna aliye juu ya sheria nchini una hakika? Bashite unaonaje yeye?
 
Wewe huoni tayari goli lemehamishwa. Ndio maana nawaita hawa wakimbizi wa Kisiasa wa CDM they are a batch of fools.

Not batch of fools maana taarifa inatoka kwa reliable and credible sources. Waliwapa taarifa za ukweli kuhusu Magufuri na Magufuri kafariki. Leo wamempa taarifa za kikosi kazi kipindi Cha Magufuri huwezi kuconnect dots. Kwamba Kuna kundi ndani ya sysytem halifurahii shambulio la Lissu.

Kesho usishangae yule Kipilimba ana letwa nchini. Huwezi jua ya kesho. Maana Nani alidhani General Sabaya angekuwa na kesi ya uhujumu uchumi?. Anayempa taarifa Lissu yupo sahihi
 

Hapo ndio unaoona umetupoteza maboya? Unadhani sisi ni watoto au mafamba na hatujui ukweli anaouzungumza Lisu.
 
Ohooo! kusha kucha huku

Lakini mbona hao hao TISS ndo walimpa ulinzi kipindi cha uchaguzi

Au ndo yale mambo ya mchawi mpe mwana akulelee
TISS wanajiamuria vitu, kwanza nikikosi kilicho chini ya nani vile....?
 
Atulie sasa watu wako kwenye jambo zito la kitaifa litakalo komesha hayo matendo aliyofanyiwa yeye na wengine.

Kwani kutulia ndiyo kufanya je? Sasa hivi tunajua Kipilimba ni mshukiwa namba 1 kwenye kadhia ile.

Tunahitaji katiba iliyo wazi kwa watumishi wa umma watuhumiwa kama Kipilimba na wafuasi wake.
 
Lissu huwa anaongea anachoona kwake ni sahihi....

Na hakuna ulazima kiwe sahihi kwa wote pia
UKo sahihi sana, ila hili analoongea Sasa ni ukweli wa wazi, suala la kuwa sahihi kwa wote hilo utajua ww.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…