Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba


Ufungue kesi mahakama chatu mshitakiwa nyoka?
 
Kwa hiyo ingetokea Lissu amefariki kwenye lile shambulio Tanpol wasingetakiwa kuchunguza na kuwapeleka wahusika mahakamani kwa sababu kusingekuwa na Principal witness???

That’s a different thing altogether. Kufariki sio sawa na kukataa kuvipa ushirikiano vyombo vya uchunguzi.
 
Ufungue kesi mahakama chatu mshitakiwa nyoka?

Hivi ni visingizio ambavyo huwa havina mwisho. Hata Police wakifanya uchunguzi, utauliza swali linalofanana na hilo. Na vivyo hivyo DPP akifungua mashitaka!
 
 
It is nobody's business! Let him get what is her right¬
 
Ni sehemu ya kazi yao. Hata hivyo, mahakama inaweza kuyatupa hayo mapingamizi, kama Kubenea atawasilisha hoja zenye mashiko zaidi.

Mahakama unayoongelea ni kama hii tu ya Yoachim Tiganga, iliyowaona watuhumiwa na kesi ya kujibu muda mfupi kabla ya mlalamikaji kughairi?

Hivi mnatuona je ndugu?
 
Mahakama unayoongelea ni kama hii tu ya Yoachim Tiganga, iliyowaona watuhumiwa na kesi ya kujibu muda mfupi kabla ya mlalamikaji kughairi?

Hivi mnatuona je ndugu?

Kama hukulima shamba unaweza kusema ukame umeathiri vibaya mavuno yako? Lima kwanza…
 
Taifa lenye kujielewa haliwekezi kuua Raia wake, bali huwalinda kwa kila namna pasipo kujali tofauti zao.

Sasa Rais kinachomfanya ashindwe kumpa guarantee ya usalama wake ni nini kama kweli hawana nia ovu?

Kwani sisi raia nani ametupatia hiyo guarantee?
We njoo bongo tuishi
Mbona sisi tupo salama kabisa
 
Hivi ni visingizio ambavyo huwa havina mwisho. Hata Police wakifanya uchunguzi, utauliza swali linalofanana na hilo. Na vivyo hivyo DPP akifungua mashitaka!

Hakuna visingizio tuliona kesi ya Lipumba Na CUF, kwa mahakama hizi Za CCM ni kupoteza wakati
 
Hizi comedy za hivi elezaneni na kina Phillipo Bukililo huko
Inaonekana na wewe wakubali Lissu & Co ni comedians. You are very right. Kusema mtu anatibiwa ugonjwa wa kisaikolojia baadaye unasikia polisi anakuja kukuhoji unakimbia na mgonjwa wa kisaikolojia ni comedy. Sasa unaanza kufumbuka macho.
 
Inaonekana na wewe wakubali Lissu & Co ni comedians. You are very right. Kusema mtu anatibiwa ugonjwa wa kisaikolojia baadaye unasikia polisi anakuja kukuhoji unakimbia na mgonjwa wa kisaikolojia ni comedy. Sasa unaanza kufumbuka macho.

Usiniwekee maneno yako ndugu.

Lissu alikuwapo Nairobi kwa muda gani? Wangapi walifika Nairobi kumjulia hali? Lini waliohitaji kumhoji walizuiliwa kwenda kumhoji?

Lissu alifika huku kwa kampeni hata kufika central polisi Dodoma na Dar es salaam.

Wapi polisi walipohitaji kumhoji?

Aliko wameshindwa kumfikia? Hivi kwa kutuona je?

Ninakazia: comedy zenu bakini nazo na kina Phillipo Bukililo huko.
 
Hata raia wa kawaida anao uwezo wa kuendesha private prosecution, kama kuna ushahidi wa criminal act lakini DPP ameamua kupotezea. Huu utaratibu upo hata katika nchi zingine, zikiwemo zilizoendelea!

..lakini Sirro si amesema bado wanachunguza?
 

..okay.

..sasa hebu tueleze kama IGP Sirro aliomba kibali cha AG wa Kenya ili aweze kutuma askari kwenda kumhoji Lissu alipokuwa Nairobi.

..Pia tueleze kama Lissu alipewa taarifa rasmi na IGP ya ujio wa askari hao halafu yeye na dereva wakaamua kutoroka kwenda Ubelgiji.

..Lakini vilevile IGP Sirro aliwahi kusema " Lissu akija tutampata.." ili kumhoji kilichotokea. Sasa Lissu alikuwepo muda gani hapa Tanzania? Kwanini jeshi la Polisi halikumhoji?

..Upo ushahidi wa Lissu kufika ofisini kwa RPC wa Dodoma. Upo ushahidi wa RPC wa Pwani kumzuia barabarani siku nzima. Upo ushahidi wa Lissu kukamatwa na kupelekwa Central police kwa mahojiano. Katika mazingira hayo Polisi hawawezi tena kudai kwamba uchunguzi umeshindikana kwasababu ya Lissu kutokuwepo nchini.

..Lakini pia kuna ushahidi mzito zaidi ambao Polisi wanao. Kwa mfano, ushahidi wa kuondolewa walinzi eneo la tukio siku ambayo Lissu alishambuliwa.

..Pia kuna ushahidi wa CCTV cameras toka eneo la tukio ambao Polisi wenyewe walidai wamechukua vifaa hivyo.

..Sasa kati ya CCTV, Lissu, na dereva, unadhani nani ameona tukio lile vizuri zaidi?

..Kati ya aliyeondoa walinzi, Lissu, na dereva, nani anawafahamu vizuri zaidi waliopanga tukio lile?

..Aliyetoa maelekezo walinzi waondolewe siku aliyoshambuliwa Tundu Lissu alikuwa na lengo gani? Je, inahitaji miaka zaidi ya minne kumtambua?

Cc Erythrocyte , Pascal Mayalla
 
hili nililianzishia uzi humu,
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…