Labda ujifanye umesahau. Wakati Lissu akiwa Nairobi na akawa ameanza kufanya mahojiano na vyombo mbali mbali vya habari IGP Sirro alitamka kuwa atapeleka vijana wake Nairobi kwenda kumhoji ili shauri liweze kuendelea. Wa kwanza ku-react alikuwa mgonjwa Lissu akidai kuwa polisi wa Tanzania hawana uwezo wa kumhoji akiwa Kenys labda wapate kibali cha mwanasheria mkuu wa Kenya. Sasa kwa nini Lissu afikiri kuwa IGP wa Tanzania hafahamu taratibu??? Cha kushangaza zaidi ni kuwa baada ya hili tamko la IGP Sirro, ilichukua muda mfupi sana Lissu na dereva wake wakahamia Ubeljiji. Inabidi ujivue ufahamu sana ili uone kuwa matukio hayo ya Lissu ni ya kawaida. Dereva aliyekuwa anatibiwa kisaikolojia Nairobi mara anahamishwa ghafla na mgonjwa Lissu kwenda Ubeljiji!!!!
..okay.
..sasa hebu tueleze kama IGP Sirro aliomba kibali cha AG wa Kenya ili aweze kutuma askari kwenda kumhoji Lissu alipokuwa Nairobi.
..Pia tueleze kama Lissu alipewa taarifa rasmi na IGP ya ujio wa askari hao halafu yeye na dereva wakaamua kutoroka kwenda Ubelgiji.
..Lakini vilevile IGP Sirro aliwahi kusema " Lissu akija tutampata.." ili kumhoji kilichotokea. Sasa Lissu alikuwepo muda gani hapa Tanzania? Kwanini jeshi la Polisi halikumhoji?
..Upo ushahidi wa Lissu kufika ofisini kwa RPC wa Dodoma. Upo ushahidi wa RPC wa Pwani kumzuia barabarani siku nzima. Upo ushahidi wa Lissu kukamatwa na kupelekwa Central police kwa mahojiano. Katika mazingira hayo Polisi hawawezi tena kudai kwamba uchunguzi umeshindikana kwasababu ya Lissu kutokuwepo nchini.
..Lakini pia kuna ushahidi mzito zaidi ambao Polisi wanao. Kwa mfano, ushahidi wa kuondolewa walinzi eneo la tukio siku ambayo Lissu alishambuliwa.
..Pia kuna ushahidi wa CCTV cameras toka eneo la tukio ambao Polisi wenyewe walidai wamechukua vifaa hivyo.
..Sasa kati ya CCTV, Lissu, na dereva, unadhani nani ameona tukio lile vizuri zaidi?
..Kati ya aliyeondoa walinzi, Lissu, na dereva, nani anawafahamu vizuri zaidi waliopanga tukio lile?
..Aliyetoa maelekezo walinzi waondolewe siku aliyoshambuliwa Tundu Lissu alikuwa na lengo gani? Je, inahitaji miaka zaidi ya minne kumtambua?
Cc
Erythrocyte ,
Pascal Mayalla