Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Tundu Lissu: Walionipiga risasi ni Kikosi Kazi cha Ofisi ya Rais chini ya Mkuu wa TISS, Balozi Kipilimba

Wanaumkebehi Lissu ni wendawazimu...huyu mtu alitaka kuuliwa na mwili wake umeumizwa. Amekuja kushiriki uchaguzi kila chombo cha habari kilipigwa marufuku kutangaza habari zake. Alitaka kuuliwa akakimbilia ubalozi wa Ujerumani ameondoka chini ya usimamizi wa mataifa ya nje, sasa hapa analalamika kuhusu hao watu waliotaka kumdhuru kuna mbuzi mawe humu zinakebehi. Huyo Mama Samia mwenyewe pamoja na kwenda kumtembelea Nairobi mbona alishindwa kusimamia alivyotaka kuuliwa tena. Magufuli alikuwa na kikosi katili sana.
 
Kati ya jambo la hovyo Sana ambalo the state wamefanya hadi leo ni kuruhusu nchi itawaliwe na chama kimoja KWA MUDA mrefu Sana!!!Tusimlaumu jpm !jpm alipewa jukumu la kulinda chama ambacho kilishapoteza mvuto ndio màana ilikuwa ni lazima atumie nyenzo haramu kama POLISI na Tiss kwenye siasa za kibabe!!!chanzo chake ndio hayo mauaji hayo na marisasi!!!!The state ingejiandaa KWA KUANDAA chama mbadala tangu mwaka 2010 Baada ya uchaguzi wa kikwete ule!!hata kama si Chadema Basi hata NCCR MAGEUZI TU!!HATA TLP AU CUF Wangeandaa mtu mzalendo hata huyo jpm akagombee HUKO na kushinda asingeua wala kutwaa Sana Sana angepambana na mafisadi tu!!!MIMI NITAENDELEA KUWALAUMU THE STATE KWA UZEMBE WAO NA KUKOSA MAONO YA KESHO!!!MARAISI WA CCM WANATUMIA NGUVU NYINGI KUPAMBANA NA UPINZANI ILI KULINDA CHAMA KULIKO KUPAMBANA NA MAENDELEO!!!NA HII ITAKUJA KULETA MACHAFUKO HUKO MBELENI NA TAIFA LITAPATA WAASI NA TUTAGAWANYIKA KWA UZEMBE WETU SISI WENYEWE!!
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Kipilimba "Mchungaji" wa kondoo!

Huyo jamaa alivyokaa kaa kimwonekano, haishangazi kama aliyasimamia haya.

Taratibu yote yataeleweka, na inafaa wahusika wafikishwe mbele ya sheria.
 
Kutaja mfumo wa utendaji juu ya tukio lile ni ushujaa wa Hali ya juu.Lisu ni raia Mwaminifu kwa nchi yake.Mpaka yanamfika yale hakufikia hata robo ya kuwa mtu aliyekua anahatarisha amani ya nchi..kwanini watu washindwe kusmamia ukweli? MAMLAKA ilifeli totali kulinda hyu Mtu na hichi ndicho ameamua kukifanya leo, ataje angalau liwe findisho kwa Mamlaka na watu fulani.
Rais wa nchi huapa kulinda Raia wa nchi yake na hili ndilo jukumu kuu.Sasa kwanini tukio lile Serikali haikuwahi kustushwa kabsaa.Sasa leo kawapa pa kuanzia. WAFANYE UCHUNGUZI ili YEYOTE ALIEHUSIKA awajibishwe ili Mamlaka iwe safi.Siasa ni nguvu ya hoja si upanga wala bunduki.
 
Hajaweka wazi nini haswa hoja yake. Ni kama mtu mwenye wasiwasi usiokwisha kwa vigezo vya mwanzoni mwa maongezi haya.

Inaweza kuwa ni muendelezo wa siasa za mitandaoni, hataki kutoka midomoni mwa watu kirahisi hivyo inambidi aongee hata kama anachokiongea ukikipima hakina undani sana.
Magufuli alikuwa muovu sana
 
Mh. Tundu Lissu awataja waliohusika kumshambulia.

Tundu Lissu amesema Walionipiga risasi ni Kikosi kazi kilichopo chini ya Rais kikisimasimaiwa na Mkuu wa TISS Kipilimba. Kikosi kazi kimeua watanzania wengi sana.

Kimeua watu wengi sana, Kilijumuisha watu wa Usalam wa taifa, Watu wa Jeshi la Wananchi, Jeshi la Polisi. Kinaitwa kikosi kazi cha kupambana na Ugaidi na madawa ya kulevya.

Watu wote waliouawa Maeneo ya Mkuranga, Kibiti Kilwa Rufiji zaidi ya watu 400. Wale waliokuwa wanatupwa mtoni maiti zinaokotwa kwenye beach, wote ni Wahanga wa Kikosi hicho.

Ndio waliomteka Ben Saanane, Azory Gwanda Mdude, Mo Dewji. Yote yalitekelezwa na hicho kikosi kazi hichi chiini ya Kipilimba ammbaye sasa ni Balozi.

Mpaka hapa harudi tena tanzania maana vita ndio kaitangaza upya
 
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀😂😂😂
Serikali imeshindwa kuwakamata hao wahuni waliotaka kuvuruga nchi mpaka Lissu arudi nchini sio?!
 
Huyu bwana ni mlalamikaji wa kiwango cha PHD. Kama Rais kafunga safari mpaka Belgium na akataka waonane, ni lazima nia yake iwe ni njema.

Akumbuke kuwa rais ni taasisi yenye watu wengi nyuma wenye majukumu mbalimbali. Hivyo aondoe wasiwasi aliokuwa nao.

Kufariki kwa JPM kumaifanya taasisi ya urais iwe na mabadiliko makubwa. Aondoe shaka.
Sasa wewe nawe unalalamikia nini; ulishapigwa risasi hata moja ukabaki salama ili utueleze ulijisikiaje?
 
Ohooo! kusha kucha huku

Lakini mbona hao hao TISS ndo walimpa ulinzi kipindi cha uchaguzi

Au ndo yale mambo ya mchawi mpe mwana akulelee
Ukisikiliza clip, anasema baadaye walimfuata ili wamuue. Noma sana
 
Ohooo! kusha kucha huku

Lakini mbona hao hao TISS ndo walimpa ulinzi kipindi cha uchaguzi

Au ndo yale mambo ya mchawi mpe mwana akulelee
Jamaa wanasema alilindwa na akina khalfan bwire na akina adamoo makomandoo wa mbowe
 
Hili na mimi ndio nilikua nataka kulisema haya yote anazuga tu pesa ya ukimbizi ya bure keshaiona tamu kuliko kurudi bongo. Asiwasingizie watu ubaya kikosi cha kujumuisha TISS, JWTZ na polisi kingemtaka kisingetumia risasi 36 na atoke mzima. Hao jamaa wa kazi risasi mbili tu angekua sasa hivi jina lake linatanguliwa na marehemu. waliompiga risasi hawajui anabahatisha ila watakua ni wahuni tu waliotaka kuivuruga nchi. Lisu anatafuta scapegoat ya kutorudi bongo mjanja sana huyu wakili msomi😀😀😀😀[emoji23][emoji23][emoji23]
Miunguni wao ni wewe kwenye kikosi kazi hicho hebu tuuleze mlitaka kutoa lisu ili faida yake nini .komenti sana ujinga na roho mbaya yako ipo siku yaja
 
Anata apate kauli thabiti kwamba atakuwa salama akirejea nchini.

Atafute huo uhakika kwa Mungu aliye muokoa mara ya kwanza. Huyu TL anamjua Mungu kweli na ni dini gani? Pamoja na ule muujiza Mkuu ulioponya maisha yake bado anatafuta uhakika wa uhai na usalama wake kwa wanadamu? Labda nina wasiwasi jamaa ni muunini wa dini ya stanisim
 
Back
Top Bottom