Watanzania wengi wanaonewa kisa hawajui sheria. Nitakupa mfano mdogo.
Katika zoezi la kuondoa wafanyakazi kwa hoja ya vyeti feki, kuna wengi ambao walikuwa na mikopo ya taasisi mbalimbali za kifedha. Pia wengi huwa wanapunguzwa huko makazini, au hata kutimuliwa.
Wengi hufuatwa na mabenki hayo na kudaiwa kulipa madeni yao. Mabenki pia husaidiana na waajiri katika kumbana mtanzania huyu. Wachache husimama kidete na kuwakumbusha kwamba kwa kuwa mdhamini wa deni ni mwajiri, na yeye hayuko kazini, basi wawasiliane na mwajiri.
Sasa wewe inaonekana hujui sheria. Watanzania huogopa sana polisi. Ndio maana polisi hujifanyia watakavyo. Tundu Lissu ni mwanasheria, tena ni wakili wa courtroom. Hawa wanapambana na polisi kila leo, tofauti na wanasheria wa makampuni.
Ndio maana kule Nyamongo, wananchi wengi walibambikizwa kesi mpaka za mauaji, Lissu aliwatoa magerezani watu 400 bila kuwatoza fedha. Acha kupotosha watu