Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

lissu anatafuta sababu ya kukamatwa au kuzuiwa kuendelea na kampeni kwa nguvu zote lakini alipolalia yeye wenzie ndipo walipoamkia wanampuuza tu hawamkamati na kampeniaendelee mpaka pumzi itakapomkatikia aache mwenyewe asubiri kuapishwa kwa jpm yaani sasa hivi hata akienda kumfinya jpm hakamatwi anaachwa tu tumeshamjua janja yake
Acha ujinga Yaani Polisi kwenda kumpiga mabomu ni lisu aliwaomba kwenda sasa atafuta sababu kivipi?
 
Wote tumeshasikia kwenye TV kwamba IGP kaamuru Tundu Lissu aende kuripoti kituo cha polisi Moshi. IGP ambaye ndiye top alisisitiza kwamba hiyo ni amri toka kwa IGP. Hiyo ni taarifa ya habari.

Masaa mawili baada ya taarifa ya habari ikasambaa mitandaoni barua ya kumwita Tundu Lissu akahojiwe kwa matamshi yake kwenye shughuli zake za kampeni.

Saa moja baadaye Tundu Lissu amejibu kwenye Twitter yake kwamba wito wa polisi siyo barua ya kirafiki, wito ni amri ya kisheria inayopaswa kueleza kosa unaloitiwa. Kwamba barua yenyewe ameandikiwa mwenyekiti wa CHADEMA na siyo yeye Tundu Lissu na haijaeleza kosa.

Hivyo yeye kama Tundu Lissu ataendelea kesho (leo) na ratiba yake ya mkutano na mabalozi.

Kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa kwani makosa ya kampeni, kama kweli yapo au kauli kwa mgombea yeyote hayashughulikiwi na polisi.

Nimesema kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa. Lakini kuna tetesi kwamba hata polisi wenyewe wanajua wamechemka. Wote wanajua sheria inayotawala ni ya uchaguzi na siyo makosa ya jinai.

Pamoja na kujua hayo yote bado mkakati wa kumkamata Tundu Lissu uko palepale na atakamatwa.

Wakishamkamata hawatamfanyia jambo lolote baya ila watakuwa wameshapata kipimo kwamba ukmuonea Tundu Lissu mwaka huu kitatokea nini hapa nchini na jumuiya ya kimataifa itafanya nini.

Maana kiukweli wote hatujajua ukimgusa Tundu Lissu kinatokea nini.

Tusubiri hadi saa 10 jioni tuone yanayokuja
Umetafakari vizuri sana. Ila mie najiuliza. Tuliona mtanange wa Lissu vs Mkurugenzi NEC kuhusu wito. Ikaonekana wito wa Mkurugenzi una mapungufu. Lissu akapangua wito huo. Lakini hata wito wa IGP nao una mapungufu pia. Wote pia wanaonekana kujawa na jazba. Nadhani miito yote miwili haitokani hasa na maamuzi ya Taasisi hizo mbili, Polisi na NEC. Nadhani inatokana na "natamani ningekuwa IGP" na "natamani ningekuwa mkurugenzi wa NEC". Pia "pumbavu" toka kwa Magufuli.
Hasira kali za Magufuli zinaonekana kwenye hotuba yake ya Tunduma.

Naamini hayo mapungufu ya wito ni ya makusudi ili kumridhisha JPM.
 
Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.

Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.
Inambanaje na washa surrender? 😂
 
Kwa hiyo kauli za Lissu ni mbaya ila za kalio anasema mkichagua wa vyama vingine haleti maji ni nzuri?
Nchi kwa double standard inashangaza sana, hawa polisi hivi wote ni form four failure? au wote brainwashed tu? Sometimes tukiitwa monkeys tunajifanya na hasira ila tabia hizi ni za nyani

Wote tumeshasikia kwenye TV kwamba IGP kaamuru Tundu Lissu aende kuripoti kituo cha polisi Moshi. IGP ambaye ndiye top alisisitiza kwamba hiyo ni amri toka kwa IGP. Hiyo ni taarifa ya habari.

Masaa mawili baada ya taarifa ya habari ikasambaa mitandaoni barua ya kumwita Tundu Lissu akahojiwe kwa matamshi yake kwenye shughuli zake za kampeni.

Saa moja baadaye Tundu Lissu amejibu kwenye Twitter yake kwamba wito wa polisi siyo barua ya kirafiki, wito ni amri ya kisheria inayopaswa kueleza kosa unaloitiwa. Kwamba barua yenyewe ameandikiwa mwenyekiti wa CHADEMA na siyo yeye Tundu Lissu na haijaeleza kosa.

Hivyo yeye kama Tundu Lissu ataendelea kesho (leo) na ratiba yake ya mkutano na mabalozi.

Kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa kwani makosa ya kampeni, kama kweli yapo au kauli kwa mgombea yeyote hayashughulikiwi na polisi.

Nimesema kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa. Lakini kuna tetesi kwamba hata polisi wenyewe wanajua wamechemka. Wote wanajua sheria inayotawala ni ya uchaguzi na siyo makosa ya jinai.

Pamoja na kujua hayo yote bado mkakati wa kumkamata Tundu Lissu uko palepale na atakamatwa.

Wakishamkamata hawatamfanyia jambo lolote baya ila watakuwa wameshapata kipimo kwamba ukmuonea Tundu Lissu mwaka huu kitatokea nini hapa nchini na jumuiya ya kimataifa itafanya nini.

Maana kiukweli wote hatujajua ukimgusa Tundu Lissu kinatokea nini.

Tusubiri hadi saa 10 jioni tuone yanayokuja
Lissu kashavunja mkeka police washa sitisha wito
 
lissu anatafuta sababu ya kukamatwa au kuzuiwa kuendelea na kampeni kwa nguvu zote lakini alipolalia yeye wenzie ndipo walipoamkia wanampuuza tu hawamkamati na kampeniaendelee mpaka pumzi itakapomkatikia aache mwenyewe asubiri kuapishwa kwa jpm yaani sasa hivi hata akienda kumfinya jpm hakamatwi anaachwa tu tumeshamjua janja yake
Kwa hiyo yeye ndie alijiandikia barua au police?
Police hawakufuata taratibu kwenye kuandika barua na kumwita..? Halaf unasema lissu anatafuta sababu.. how? Grow up man..
 
mtashangaa sana mwaka huu mitego yake yote hanasi mtu subirini jpm aapishwe ndo mtajua
 
Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.

Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.
Watanzania wengi wanaonewa kisa hawajui sheria. Nitakupa mfano mdogo.

Katika zoezi la kuondoa wafanyakazi kwa hoja ya vyeti feki, kuna wengi ambao walikuwa na mikopo ya taasisi mbalimbali za kifedha. Pia wengi huwa wanapunguzwa huko makazini, au hata kutimuliwa.

Wengi hufuatwa na mabenki hayo na kudaiwa kulipa madeni yao. Mabenki pia husaidiana na waajiri katika kumbana mtanzania huyu. Wachache husimama kidete na kuwakumbusha kwamba kwa kuwa mdhamini wa deni ni mwajiri, na yeye hayuko kazini, basi wawasiliane na mwajiri.

Sasa wewe inaonekana hujui sheria. Watanzania huogopa sana polisi. Ndio maana polisi hujifanyia watakavyo. Tundu Lissu ni mwanasheria, tena ni wakili wa courtroom. Hawa wanapambana na polisi kila leo, tofauti na wanasheria wa makampuni.

Ndio maana kule Nyamongo, wananchi wengi walibambikizwa kesi mpaka za mauaji, Lissu aliwatoa magerezani watu 400 bila kuwatoza fedha. Acha kupotosha watu
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.
utaitwa siku moja na wenzenu watu wasiojulikana ukiendelea kua na akiri za kipumbavu...eti na kwa simu....utajuwaje wana impersonate police officers ...kada mjinga kweri wewe
 
Watanzania wengi wanaonewa kisa hawajui sheria. Nitakupa mfano mdogo.

Katika zoezi la kuondoa wafanyakazi kwa hoja ya vyeti feki, kuna wengi ambao walikuwa na mikopo ya taasisi mbalimbali za kifedha. Pia wengi huwa wanapunguzwa huko makazini, au hata kutimuliwa.

Wengi hufuatwa na mabenki hayo na kudaiwa kulipa madeni yao. Mabenki pia husaidiana na waajiri katika kumbana mtanzania huyu. Wachache husimama kidete na kuwakumbusha kwamba kwa kuwa mdhamini wa deni ni mwajiri, na yeye hayuko kazini, basi wawasiliane na mwajiri.

Sasa wewe inaonekana hujui sheria. Watanzania huogopa sana polisi. Ndio maana polisi hujifanyia watakavyo. Tundu Lissu ni mwanasheria, tena ni wakili wa courtroom. Hawa wanapambana na polisi kila leo, tofauti na wanasheria wa makampuni.

Ndio maana kule Nyamongo, wananchi wengi walibambikizwa kesi mpaka za mauaji, Lissu aliwatoa magerezani watu 400 bila kuwatoza fedha. Acha kupotosha watu
Sijaelewa Mikopo, Vyeti, na kukataa wito wa polisi vinauhusiano gani
 
Kabudi no waziri wa mambo ya nje ndie bosi wa mabalozi wote aweza ongea nao anytime
Wewe mwanamke acha utani, yani Kabudi awe bosi wa balozi wa Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa.

Tatizo lako wewe waga reasoning ni ndogo sana. Wewe unaweza kuwa bosi wa wazazi wako.!!
 
Back
Top Bottom