Wote tumeshasikia kwenye TV kwamba IGP kaamuru Tundu Lissu aende kuripoti kituo cha polisi Moshi. IGP ambaye ndiye top alisisitiza kwamba hiyo ni amri toka kwa IGP. Hiyo ni taarifa ya habari.
Masaa mawili baada ya taarifa ya habari ikasambaa mitandaoni barua ya kumwita Tundu Lissu akahojiwe kwa matamshi yake kwenye shughuli zake za kampeni.
Saa moja baadaye Tundu Lissu amejibu kwenye Twitter yake kwamba wito wa polisi siyo barua ya kirafiki, wito ni amri ya kisheria inayopaswa kueleza kosa unaloitiwa. Kwamba barua yenyewe ameandikiwa mwenyekiti wa CHADEMA na siyo yeye Tundu Lissu na haijaeleza kosa.
Hivyo yeye kama Tundu Lissu ataendelea kesho (leo) na ratiba yake ya mkutano na mabalozi.
Kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa kwani makosa ya kampeni, kama kweli yapo au kauli kwa mgombea yeyote hayashughulikiwi na polisi.
Nimesema kimsingi ngoma ilitakiwa iishie hapa. Lakini kuna tetesi kwamba hata polisi wenyewe wanajua wamechemka. Wote wanajua sheria inayotawala ni ya uchaguzi na siyo makosa ya jinai.
Pamoja na kujua hayo yote bado mkakati wa kumkamata Tundu Lissu uko palepale na atakamatwa.
Wakishamkamata hawatamfanyia jambo lolote baya ila watakuwa wameshapata kipimo kwamba ukmuonea Tundu Lissu mwaka huu kitatokea nini hapa nchini na jumuiya ya kimataifa itafanya nini.
Maana kiukweli wote hatujajua ukimgusa Tundu Lissu kinatokea nini.
Tusubiri hadi saa 10 jioni tuone yanayokuja