Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Ni kweli hizi Ni kampeni, eidha wapeleke malalamiko time au wamkamate tu Kama Kuna jinai
 
lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Ni mazoea au ndio Sheria inasema hivyo?
 
Hivi 'mataga' haina umoja kama ilivyo kwa maneno; mazingira, dini, n.k?
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
 

Na inakuwaje barua confidential inapitia kwa mtu mwingine? Confidentiality ipo wapi hapo?
 
Wito wa "kishkaji" siyo wito wa kisheria, polisi ifuate sheria na Lissu atatii sheria!

Lissu hawezi kuacha mambo ya msingi afuate wito ambao haujazingatia sheria, huko ni kupotezeana muda!
Tena ni ujuha kutumia headed paper ya Jeshi la Polisi yenye nembo na kubandika neno confidential wakati barua inapitia kwa mtu mwingine hivyo kuondoa umaana wa confidential na content (maudhui) ya barua hayakidhi haja ya kisheria ya kumuita mtu Polisi.
 
Kubattle na Lissu inahitaji akili mingi, unfortunately so far wote wanaojaribu wanatumia 'nguvu 9 na akili 1', watafeli wote!!
 
lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Ambapo huyo mwanasheria utampata muda gani ilhali barua/wito haujakupa hiyo nafasi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…