Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Jeshi la polisi limejaa vilaza, ndiyo maana hutumia nguvu zaidi sababu akili hawana.
Kwa maoni yangu ocd angalau aanzie diploma, RPC aanzie na degree, Igp angalau masters.watoa amri wote jeshi la polis wawe na elimu, nikimfikiria yule aliyetoa amri ya kupiga mabomu msafara wa salumu mwalimu ananiacha hoi.
 
Nilishauri humu narudia tena, tundu lisu aachwe aropoke apendavyo maana hiyo ni sehemu ya tiba kwake kwa yaliyomkuta.

Kingine Lisu hawezi kuwa rais popote duniani kwahiyo aachwe afanye atakalo maana 28 oktoba hii tutamfundisha adabu
 
Kuigomea polisi kufanya uchunguzi ni kinyume cha sheria; sasa sijui yeye ni mwanasheria gani. Wakati mwingine polisi wanaweza kutaka kukuhoji wewe kama shahidi kuhusu mtumhumiwa mwingine tofauti kabisa ambaye wanaweza kuwa na taarifa zake zaidi. Ni afadhali angejibu tu kuwa sasa hivi ratiba yake iko tight sana anaomba akutane na polisi katika muda mwingine siyo sasa kuliko kuweka jou hilo la kukaidi, kwani tayari ameshaweka ushahidi unaoweza kutumika dhidi yake; ndiyo maana nina mashaka sana na busara za Lissu pamoja na uanasheria wake. Hiyo kisheria ni kuizuia polizi kufanya kazi zake ammbalo ni kosa. Raia kuhojiwa na polisi ni sehemu ya majukukumu ya polisi kabla hawajamchukulia mtu hatua; yeye Lissu anaogopa nini kuhojiwa kama anajua yuko clean?
Polis wangeweza hata kuongea naye kwa simu kwanza, kama wasingeelewana ndipo angepewa wito wa kwenda kituoni.kwa barua ile nimeona shida ya jeshi la polis..
 
Nilishauri humu narudia tena, tundu lisu aachwe aropoke apendavyo maana hiyo ni sehemu ya tiba kwake kwa yaliyomkuta.

Kingine Lisu hawezi kuwa rais popote duniani kwahiyo aachwe afanye atakalo maana 28 oktoba hii tutamfundisha adabu
Angalau umejitaidi kutoa maoni yako vizuri, polis wetu wanadhani kila kitu in cha kuita MTU kituoni.hili ni tatizo.
 
Nilishauri humu narudia tena, tundu lisu aachwe aropoke apendavyo maana hiyo ni sehemu ya tiba kwake kwa yaliyomkuta.

Kingine Lisu hawezi kuwa rais popote duniani kwahiyo aachwe afanye atakalo maana 28 oktoba hii tutamfundisha adabu
Serekali ya CCM inahangaika na Lissu kwa sababu ni serekali iliyokosa maarifa,ni serekali dhaifu,imejaa woga na kutokujiamini.Serekali ya namna hii ni serekali iliyokosa kibali cha wananchi kuendelea kukaa madarakani
 
Mimi siyo mwanasheria wala mwanasiasa, lakini nina foundation nzuri sana kuhusu sheria kwa vile ninaishi mazingira ambayo ujuzi wa sheria ni wa muhimu sana. Kwa mfano polisi akikuwashia taa za rangi barabarani huwezi kukimbia ukidai kuwa hujaambiwa kosa lako; ukikimbia unakuwa umetenda kosa, na anaweza kukurushia risasa au kutafuta polisi wengine wakuzingire na hata kuangusha gari lako mtaloni kwani wakti huo tayari unakuwa ni mhalifu hata kama sababu waliyokuwa wanataka kukuuliza haikuwa inahusianiana na makosa yako binafsi. Simama umsikilize kwa nini kakuwashia taa za rangi, baada ya hapo ndipo uulizea uhalali wake kukusimamisha.

Polisi siyo mahakama, hawahukumu bali kazi yao ni kutafuta ushahidi, na raia anakuwa anavunja sheria kuwazuia polisi kutafuta ushahidi huo. Ukishashaingiza mambo ya sheria kwenye siasa basi unakuwa unapoteza watu wako, na pia kuvuruga jamii. hakuna uhusiano wowote kati ya sheria na siasa kwenye jamii timamu.
Tatizo polis wanapenda ingilia kila jambo, pia polis wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria.
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Ndio maana mnatekwa tekwa na kupotezwa mazwazwa nyie
Utaendaje sehemu kichwa kichwa.
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
mataga andikeni upya upya barua ya wito acheni kulia-lia kama kuku maji.
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro
View attachment 1587622
View attachment 1587514
Police hawako serious barua gani iyo hakuna ata aliyesomaga communication skills chuoni
 
Kwa maoni yangu ocd angalau aanzie diploma, RPC aanzie na degree, Igp angalau masters.watoa amri wote jeshi la polis wawe na elimu, nikimfikiria yule aliyetoa amri ya kupiga mabomu msafara wa salumu mwalimu ananiacha hoi.
Yes ni wazo jema kabisa, lakini kwa kuanzia hili jeshi ilipaswa lifumuliwe kutoka kwenye Police force kwenda kwenye Police service.

Kwa muundo wa sasa lazima warecruit watu 'wajinga' ambao kazi yao ni kupokea na kutekeleza amri maamuzi wanafanya wengine.

Sifa ya majeshi yetu kwa sasa ni kuwa na physical fitness tu ndio maana 'hawawapimi' afya ya akili japo wanawakabidhi silaha na moja ya sharti la kumiliki silaha ni kuwa na akili timamu.
 
Back
Top Bottom