Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Uchaguzi 2020 Tundu Lissu: Wito wa Polisi siyo barua ya kirafiki, Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi

Lissu anatafuta sababu ya kushindwa
kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu,maelezo utayakuta polisi,na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote
Sasa mbona hawakuimuita kwa Simu bali walimuita kwa PRESS CONFERENCE sasa aende wapi KIlimanjaro au DAR? bado tu hujona kuwa mmetumia akili ndogo saana kumfanyia figisufigisu? hivi CCM hamna brains za kufanya "siasa"?
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.
kwa sheria ipi hio ?
au ndio tumezoea kuburuzana ?

nimepigiwa simu na polisi niende kituoni kuuliza kosa akaniambia eti nitajua nikifika...

huu ni mwezi wa tatu sijawahi kukanyaga kituoni na nilimuambia kama ana uwezo anisake mpaka anikamate mwenyewe ila kwenda kituoni mwenyewe asahau.

sipendagi ujinga
 
Nahisi Sirro anakosa raha Sana ya kuwa IGP.

Mchakamchaka mwanzo mwisho,akigeuka huku Jiwe anamshurutisha akigeuka kule Lissu anamuhenyesha.

Safi sana Mh Lissu lazima wawe na nidhamu ya kazi hao vibaraka wa Jiwe![emoji16][emoji16]
 
Tundu Lissu katika Ukurasa wake wa Twitter, ameweka Barua ya Polisi na kuandika Maneno haya "Wito wa polisi sio barua ya kirafiki, ni amri ya kisheria. Wito huo unatakiwa kueleza kosa la mtuhumiwa. Barua hii haielezi kosa ninaloitiwa na imepelekwa kwa Mwenyekiti wa chama. Huu sio wito wa polisi kwa mujibu wa sheria. Nitaendelea na ratiba yangu ya kikao na mabalozi kesho."

IGP Sirro amtaka Tundu Lissu kuripoti kituo cha polisi Moshi mkoani Kilimanjaro

Polisi wa CCM hawafanyi kazi kwa mjibu wa Sheria wao wakati wanawapiga mabomu chadema waliitwa wapi kutoa Maelezo ya unyama ule?
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.
No!Ni mambo ya aibu na ya ajabu,ni serekali ya aibu!Angalia hii barua imekuwa addressed kwa nani?Hata mtoto wa chekechea hawezi kufanya kosa kama hili!Sasa unategemea katika mazingira kama haya Lissu akuchekee?
432098.jpg
 
Lissu anatafuta sababu ya kushindwa, kisheria polisi wanaweza kukuita hata kwa simu, maelezo utayakuta polisi na utapewa haki ya kusikilizwa ukiwa na mwanasheria wako au mtu yoyote.
Sababu ipi ya kushindwa? Wito wa uonevu kwa matakwa ya ccm una uhusiano gani na kushindwa?
 
Kwani kuitwa polisi hadi uwe umetenda kosa🤤🤤🤤 huyu jamaa kama tukiigeuza sheria kuwa kiingereza basi alichokalili yeye ni Yes,No,Giive me water basi Tundu ni mweupe sana kwenye sheria hata mikataba ya kimataifa alisema tuiache vile vile hatuna namna ila wanaojua sheria wakaingia vitani na wakashinda poor you mpigania ushoga.

MAGUFULI4LIFE.
 
Huo huo mstari mkumbushe na jiwe kuwa wananchi wa tunduma hawastahili kufokewa wa kupangiwa mtu wa kumchagua hivyo achunge ndimi yake
Halafu anadai apeleki maendeleo Tunduma huku anakusanya kodi zao.Huo ni utapeli Kama hawezi peleka maendeleo pia aache kukusanya kodi!
 
Barua yenyew ina dosari Polisi wetu bana 😂 😂 😂
View attachment 1587708
Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.

Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.
 
Heheheee.... Ukweli ni kwamba, hiyo ni sawa sawa na barua ya harusi tu!

Wito au barua ya polisi LAZIMA ieleze KOSA ANALOITIWA KWALO ikiambatana na "statement of probable cause" kuhusu kosa hilo!

Huwezi tu kuita mtu kienyeji enyeji! Angalau sio kwenye nchi tunayoiita "Jamuhuri" (sijui hata kama unaelewa maana ya Jamuhuri wewe mataga?)

Vinginevyo hiyo itakuwa ni Jamuhuri ya kihuni tu kama mapolisi watakuwa wanajiendesha kama genge la walevi.

Polisi hawako juu ya sheria. Wafuate hizo procedures waache kujidekeza!
Hujuu kitu, kuitwa polisi au ofisi yoyote ya kiusalama sio lazima uwe umetenda kosa na haimaanishi kuwa umetenda kosa unachotakiwa ni kuitika wito kwakuwa umeitwa na vyombo vya usalama vya nchi yako Tena vilivyopo kisheria. Ila kama wewe ni teja mla unga unaweza kujishtukia kidogo.

MAGUFULI4LIFE.
 
Police hawako serious barua gani iyo hakuna ata aliyesomaga communication skills chuoni

Guys, nilishasema kuwa Polisi ni watu wenye uelewa duni sana! Sifa ya kujiunga na Polisi ni Form 4 failure wenye 0 na Division 4 au 3 mahututi.
Ukiwa mwajiriwa wa Jeshi la Polisi huhitaji kufikiri zaidi ya KUPOKEA AMRI iwe nzuri au mbaya!!
JITU linaambiwa KAMATA, PIGA BOMU, PIGA RISASI linatekeleza amuri hata Kama siyo halali.
Mapolisi wote duniani wako hivo ndo maana tunaona yanayotokea Marekani kwa mauaji ya watu weusi k.m. George Floyd na msemo wa..." I CAN'T BREATH"....!!
Polisi ni tatizo katika Jamii wasipo dhibitiwa na sheria Bora za nji.
 
Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.

Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.

Utopolo++++++😁😁😁
 
Aisee kama sote tungekuwa kama Lissu, Nchi hii ingekuwa mbali sana

Kama wote mngekuwa hivyo nchi isingetawaliwa.

Lissu anasahau kuwa ni mgombea Urais, hivyo anapaswa kuonesha mfano wa kuheshimu mamlaka ili naye aje kuheshimika! Akumbuke pia ni kiongozi wa chama kinachodai utawala wa sheria!

Tusubiri kuona kama Lissu, mwanasheria, aliyewahi kuwa mbunge (kutunga sheria), na Rais wa Chama cha Mawakili Tanzania (TLS) ataendelea kukaidi wito wa Jeshi la Polisi na kuonesha ubabe hadharani.

Busara, hekima na utii ndio humtofautisha binadamu na mnyama. Yumkini Lissu ana agenda yake. Kwa vyovyote vile Polisi wasisite kumchukulia hatua.
 
Makosa hayo ya kiuandishi sio utetezi kabisa kisheria, Tundu anajua hilo na hiyo barua kupelekwa kwa Mwenyekiti wa Chama chake kwake sidhani kama ni utetezi anapaswa atambue kuwa Chama ni Cha mwenyekiti na Chama hicho ndio kimemdhamini yeye kuwa Mgombea wa Urais na hata alipofika Tume aliwasilisha barua ya Utambulisho kutoka kwa Chama ambayo Katibu wa Chama ndio alimtambulisha Tume. Hivyo Polisi kumtaarifu Mwenyekiti juu ya hilo ni sahihi kabisa kuwa mtu wako anahitajika. Na anahitajika kuhojiwa kutokana na matamshi na kauli zake alizozitoa.

Tundu anachofanya ni kuchelewesha tu lakini bado sheria inambana.
Sheria zipi zitambamba?Hizi hizi anazovunja Magufuli na hafanyiwi lolote?
 
Isjui kilichokuwa kichwani mwa polisi katika kuandika barua hiyo kwa Mwenyeketi, ila ninadhani kuwa hawakutaka kuathri kampeini za CHADEMA wakati Lissu akiwa anahojiwa na polisi: ni uungwana tu kuhakikisha mwenyekeiti anaweka mtu wa kuendesha kampeini za Lissu wakati hayupo kwenye majukwaa.
Mtu wa kuendelea na kampeni kama mbadala wa lisu? Dah! Umesoma hata sheria za uchaguzi ndugu?
 
Back
Top Bottom