Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo


Shukrani mkuu
 
Mkuu nikifika hapo na 1.5m naweza kujitafuta nikajipata?
Mkuu kama wewe ni mtu wa Mpira , jichanganye pale Kisimani wanapobadili, Fedha , Kuna kijiwe kipo pembeni ya duka la simu maarufu kama lauphone , Anza kijichanganya pale Kwa Story za Mpira , acha habari za Siasa , yupo Mnyakyusa Moja mfupi kwenye kile kijiwe ni mbishi sana, Ila Kuna watu poa sana pale , wapo Jamaa wawili ukifika Waulizie Mr Solo mshabiki sana Arsenal, na Mr Parti Mshabiki wa Man United, ukifika jitambilishe Kwa hao Jamaa wawili watakupa muongozo ni watu wazuri sana kwa Tunduma, Hao watakusadia,, Ila Kuna jamaa wengine pale Mnyamwanga Wwa Arsenal, Rashidi wa Man U, mgogo, Na Jamaa Moja kibongecwa Chelsea. Ila hakikisha unamuona Solo mwambie ni nomelekezwa na mtu wa Mpira
 
Oya hivi nikizama Hapo tunduma na piki piki, inaweza kunipa pesa Kwa namna ipi?

Alafu vipi kuhusu wachumba ?
Kuwa makini boda boda Yale mazingira ni hatari Kwageni kuendesha Usiku, ila Kuna vijiwe wamejisajili kabisa wanafanya kazi 24HRS maeneo ya Valentine, mjini valenyine night club, Sauna, Mpemba, Kwa Yusuph,
 
Mfano natoka hapo tunduma natumia usafiri gani kwenda nakonde
Tunduma ni upande wa Tanzania na Nakonde ni upande wa Zambia ni eneo ambalo limeingiliana Kuna sehemu nyumba zinakutana Kwa umbali mdogo, unaweza vuka boda Kwa miguu or ukatumia pikipiki, Kuna muingiliano sana , kuanzia Tazara via migombani, Black , maguruweni, Mwaka. Mwaloni, Iboya, ,Dampo, Hadi maeneo ya Chipaka misugu, kote Kuna muingiliano na upande wa zambia
 
Ila mbona nasikia uhalifu ni mwingi sana Tunduma unahisi sehemu gani zinaweza kuwa salama mfano ni guest za maeneo gani zinawezq kuwa salama kwa mgeni
 
Ila mbona nasikia uhalifu ni mwingi sana Tunduma unahisi sehemu gani zinaweza kuwa salama mfano ni guest za maeneo gani zinawezq kuwa salama kwa mgeni
Maeneo hatarishi ni maguruweni ma baadhi ya maeneo, hata miji mingine Kuna mitaa hatarishi, Guest na lodge nzuri zenye usalama, ni Kuanzia Nyati hotel, Valentine ya I oya jirani na Olympic Petrol Station maeneo soko la Iboya, Olympia lodge jirani na Soko la Mazao, na lodge za Mpemba napo papo vizuri, ogopa vichochoro vya maguruweni mida ya Usiku, sogea mida Usiku sana, Mkombozi, Sayuni, makaburini Kwa Usiku sana kunaweza kuwa hatari. Kama mgeni pale ukifika Valentine lodge ya Iboya , mwambie counter akukutanishe na Boss wao anakuwepo Yale maeneo kuanzia saa tatu or saa nne asubuhi or jioni anakukabidhisha Kwa boda boda or tax unakuwa huru sana, mtu Moja mzuri sana Hana makuu
 

Mkuu mimi ni shabiki lia lia wa chelsea na simba so nitajoin nao, Mungu akubariki mkuu, nitawatafuta watu hao nikifika.
 
Nashukuru kwa muongozo mkuu na pia bila shaka inawezekana kulala upande wa pili wa boda huko zambia
 
Hivi many manyanya mbona mchafu sana hafanani na utajiri wake au ni masharti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…