Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Nilichoka hapo Tunduma baada ya kukuta vijana wamepanga hela mikononi kama milioni kumi kumi hivi wanabadilisha na dollar au kwacha ya Zambia. Hawana wasiwasi na maisha yanaenda tu, nilipowauluza wazawa wakasema hayo ndiyo maisha yao, kwa kweli sijawahi shuhudia sehemu nyingine yeyote ile hali. Inaonyesha mzunguko wa hela ni mkubwa sana hapo mjini Tunduma
Hata Namanga upande wa Kenya kuna wasomali wanabadili fedha ila wao angalau wana vibanda kama vya m-pesa sio hadharani kama Tunduma.
 
Huu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.

Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.

Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
ni kwa vile inapakana na nchi nzuri ya Zambia
 
Sidhani kama Kariakoo Kwa volume ya biashara inaifikia Tunduma,najua mtabisha ila tukija kwenye figures ndio utashangaa.

Mkoa wa Songwe ni WA 6 Kwa mapato makubwa(TRA) Tanzania na 90% ya mapato hutoka forodha ya Tunduma zaidi ya Bil.150

Kariakoo ni bil.40 😂😂
hizi statistics umezitoa mchambawima au wapi...
 
ni kwa vile inapakana na nchi nzuri ya Zambia
Wewe mfuasi wa Mbowe usijidanganye. Zambia haina uzuri wowote. Hii ni barabara kuu ya Nakonde - Kapiri Mposhi ilivyo kwa sasa. Mashimo kama yote. Ukiamka asubuhi nenda ofisi ya CCM iliyopo karibu ukashukuru kwa ilani nzuri ya uchaguzi iliyosambaza lami nchi nzima.
IMG-20230822-WA0012.jpeg
 
Huu uzi ilikuwa niuandike muda mrefu kwa mambo niliyojionea kwenye mji wa Tunduma. Kwa ambao hajawahi fika Tunduma wanaweza kudhani ni ka-mji kadogo ambacho kipokipo tu. Kwa sisi wa Arusha tulikuwa tunaamini Namanga ndo mji mkubwa zaidi wa mpakani kwa Tanzania kumbe kuna Tunduma.

Kinachonifanya niandike ni biashara kubwa iliyoko Tunduma. Ule mji wa mpakani kwa mjasiriamali mdogo ni sehemu sahihi ya kwenda kusoma ramani. Uchangamfu wake unaendana sana na Kkoo tofauti ikiwa ni ukubwa tu. Ila wafanyabiashara wa nguo Tunduma wanawezaje kuuza nguo za jumla kwa bei sawa na ya Kariakoo? Baadhi ya wafanyabiashara huuza bei chini hata kuliko Kariakoo. Kimahesabu imekaaje hii? Hata vitu vingine jamaa wako fair.

Kimsingi Tunduma ni boda kubwa zaido bongo yenye fursa nyingi sana.
Tunduma ni mji mkubwa wa mpakan lakin hauna deal kubwa za mpakan kama mpaka x. Ngoja niishie hapo.
 
Hiyo Tunduma yote hadi Mpika upande wa Zambia ndo kulivyo.
Ndio siwezi ishi kwenye kimji Cha hivyo hivyo.

Miji yote Iko covered na Vegetation hata Dodoma imeishinda.
 
Sasa si Bora hapo katikati ya Chapwa na Tunduma walau pamepangwa ila huko kwingine ni mabanda ya hovyo hovyo Bora liende.Walau Sumbawanga road ndio nimeona wanajitahidi kupanga Mji japo ushamba Sasa wa kujenga nyumba za kufanana ndio umezidi 😂😀

Wote wanakomaa na pitched roof,wanashindana kench kupaa Juu,ujinga.

Mwisho Huwa sipendi kuishi Miji ya hivyo ni Miji ya watu wasio soma ila Wana hela Sasa wanakosa aspects ya utaalamu/shule kwenye mambo Yao mengi.
Tafuta hela kwa bidii kikawaida mtu akiwa na pesa huyo moja kwa moja ameshastaarabika hawezi kufanya mambo ya ajabu ajabu...kusoma unakosema ni kama kabudi,lipumba,mdee,bulaya nk?
 
Back
Top Bottom