Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Tunduma ni mji wa kipekee. Mapigo yake ni kama Kariakoo

Yule Jamaa pamoja Mpunga anaomiliki ila Bado ni mtu mungwana mnyenyekuvu msikivu Unamkuta yupo pale Dukani kwake anacheka na kutaniana na wateja wake , Huwezi zania ametoka Mbozi ndani ndani Maduka yake yote yameunganishwa na Mifumo ya kisasa piya Vituo vyake vya Mafuta vimeunganishwa kwenye mifumo mizuri ya kisasa kudhibiti Wafanyakazi wezi.
Hii Agro sio Mshani wewe??
 
Changamoto kubwa ya Mji wa Tunduma ni kukosa u uni kwenye eneo la Mipango miji, huu Mji uliathiriwa sana Siasa kwenye Issue za Mipango Miji Angalia Town Planer wamepeleka Huduma zote muhimu upande Moja wa Mji :- Wamepeleka Hospital ya Rufaa eneo la Mpemba, Wamepeleka parking ya Malori yanayosuburi kuvuka boarder Mpemba, Stand Ipo Mpemba, Uwanja wa Mpira upo Mpemba, Ofisi za Halimashauri na mkuu wa Wilaya zipi Mpemba. Na eneo Hilo la Mpemba Lina changamoto ya Foleni ya Malori makubwa , piya barabara ya Mpemba inamteremko hatari sana Kwa kupisha malori, magari madogo na Bajaji. Baadhi ya Huduma wangepeleka upande wa Sumbawanga Road kuanzia Njia panda ya Msongwa, Chipaka na Mizani ikangamo.. Leo Hii watu wanaoishi upande wa Msongwa Chipaka , Nyerere wanapatavShida sana kwenda Standi mpya Mpemba
ni kama Mbeya mjini tu. Tunduma pamejengwa hovyohovyo sana, has haya maeneo ya Chapwa kuelekea Mpemba. Wangeiga mpangili mzuri kama wa mji wa Sumbawanga ama Kasulu, mji ungependeza sana.
 
Zile deal za Black market upande wapili nyuma ya frame za Viatu ule upande unazalisha sana Madoni Kila mwezi kwenye deal za:-
Vipodozi.
Vitenge.
Mafuta ya Kula.
Sukari.
Sigara .
Mbegu za Mahindi / Zamsed.
Mafazeti used kutoka Zimbabwe, South Africa.
USD ;- zinatoka Congo na unazipata upande wapili, Pombe za Viroba, na Pombe za vichupa vidogo wanauza Bei ya Tshs 1000/= na Viroba vinaanzia 250-500 maeneo ya Black na Iboya.
Kuna matajiri wanspiga Hela kwenye Biashara ya kubadilisha Fedha, yeye ana Supply fedha Kwa Vijana jioni anarudishiwa na Faida , Hao wanaitwa wenye Visima , mtu ana Supply hata billioni Moja Kwa Vijana wake 30 wanaokwenda kutafuta Dolla Hadi Congo.
Kuna Wababe kwenye Biashara ya Mafuta ya Petroleum kupeleka upande wa Zambia Kuna Yule Msomali wa Petroafrica mwenye upara aliwakamata sana wa Zambia.
Kuna Yule Tajiri wa Valentine Bar ya Pale Boarder na Valentine night club Jamaa anajimbiza sana kaanzia kwenye Bar Hadi kushika soko la Viatu Hadi Kumiliki Kusoma pale Kisimani.
Yupo Dubai Tyre Jamaa anakimbiza sana kwenye biashara ya Tyre Sasa amehamia kwenye Mafuta Bei zake za Tyre ni kama Dar es salaam. Yupo yule Manyanya ameshika biashara za maduka balaa pale Boarder piya yeye ndie amehamia kwenye vituo vya Mafuta, Wapo Hawa Jamaa wa Olympic petroleum anauza Mafuta Kwa wholesale Kwa Bei ya Depot'.
Mjii wa Tunduma una Bank zaidi ya Sita, Petrol Station zaidi ya Hamsini, lodge na Bar zimetapaka Kila baada ya nyumba mbili or tatu,
UNGEKUWA UNAMSIFIA YESU KAMA HIVI UNGEFIKA MBALI SANA

Sent from my A37fw using JamiiForums mobile app
 
Sijui ulifika lini Sumbawanga mkuu Petrol station zipo zaidi ya hizo unazosema wewe

Usipende kuiongelea Sumbawanga uliyofika wewe miaka ya 90 mkuu
Saizi Kuna Ujenzi wa petrol station Mpya 3,mwaka Jana pia petrol station Mpya 3 zilifunguliwa.

Hao wamezoea story za kusimuliwa hawasafiri.Mwisho.kusema Tunduma Ina petrol station zaidi ya 50 ni uongo wa mchana kweupe,zilizopo hazizidi hata 30 na Hadi juzi sijaona ujenzi wa service station yeyote hapo Tunduma.
 
Kkoo kweli ni kubwa ila hapa tunashangaa mji mdogo Tunduma kuwa na mambo yanayokimbizana na Kkoo
Sidhani kama Kariakoo Kwa volume ya biashara inaifikia Tunduma,najua mtabisha ila tukija kwenye figures ndio utashangaa.

Mkoa wa Songwe ni WA 6 Kwa mapato makubwa(TRA) Tanzania na 90% ya mapato hutoka forodha ya Tunduma zaidi ya Bil.150

Kariakoo ni bil.40 😂😂
 
ni kama Mbeya mjini tu. Tunduma pamejengwa hovyohovyo sana, has haya maeneo ya Chapwa kuelekea Mpemba. Wangeiga mpangili mzuri kama wa mji wa Sumbawanga ama Kasulu, mji ungependeza sana.
Sasa si Bora hapo katikati ya Chapwa na Tunduma walau pamepangwa ila huko kwingine ni mabanda ya hovyo hovyo Bora liende.Walau Sumbawanga road ndio nimeona wanajitahidi kupanga Mji japo ushamba Sasa wa kujenga nyumba za kufanana ndio umezidi 😂😀

Wote wanakomaa na pitched roof,wanashindana kench kupaa Juu,ujinga.

Mwisho Huwa sipendi kuishi Miji ya hivyo ni Miji ya watu wasio soma ila Wana hela Sasa wanakosa aspects ya utaalamu/shule kwenye mambo Yao mengi.
 
Nakuunga mkono 100%. Kwa Tanzania napakubali Sumbawanga na Tanga kwa mpangilio. Halafu yote ni miji inayosifika kwa ushirikina
Ila wahamiaji kutoka.mbeya/Songwe wameanza kuharibu Mji wa Sumbawanga kama walivyofanya huko kwao.

Maana wafipa walishazoea kuishi Kwa order na kuachiana nafasi Barabara za mitaa nk na ni Karibu Mkoa mzima eg Namanyere.

Ila Sasa hao ndugu zetu wa huko Mbeya wanataka kuharibu Mji maana Huwa sio wastaarabu kiasi kwamba kama Sehemu Bado haijapimwa na Serikali itageuka kuwa squatter wakikaa wao.
 
Tunduma ukienda kwa ajiri ya starehe mkuu apakufai ila kwa mtu anae jitafta ni Bora kwenda tunduma kuliko kwenda dar.

Mimi naona ukishindwa kuishi Tunduma wewe sehemu zote uwezi kuishi

Pale vitu ni Bei ndogo Sana sio msosi sio pakulala ukiwa Tunduma unapata advantage kubwa ya vitu vikipanda upande wa bongo unafuata upande wa zambia.

Mpaka mabando pale ukiwa na laini ya zambia unatumia vizuri tu maana mtandao unashika vizuri tu,unaweza pata GB2 kwa 10kwacha ambayo kwa kibongo ni kama 1350 tu.
Kuishi kwenye kimji ambacho hakina planning (squatter)ndio sifa ,Tunduma ingekuwa impangiliwa kama tanga au Dodoma ingevutia watu wengi sana
 
Back
Top Bottom