Tuombe Mungu sana watoto wetu wasijekuwa kama mwijaku maana huku alipofikia inasikitisha

Hapana mkuu sijamfuatilia sana, sema hizi ambazo nimeziona ni anajidharirisha yeye kwa lengo la kupata pesa SASA ni bora anayejidhalilisha yeye kuliko anayewadharirisha wengine kwa manufaa binafsi.
Kudhalilika ni kubaya iwe wewe mwenyewe au kwa kufanyiwa na mtu mwingine.
Na psychology says : ni afadhali kuzalilishwa na mtu au Watu wengine jamii inaweza kukuelewa Pengine umeonewa lakini kujidhalilisha mwenyewe ni kutoitendea haki nafsi yako mwenyewe .
Ni kujikatili nafsi yako mwenyewe ni Sawa na kujiua mwenyewe ambao ni ukatili wa hali ya juu sana.
Inaweza kueleweka kukataliwa na watu wengine lakini sio kujikataa mwenyewe nafsi yako.
 
Na mimi nashangazwa mno na comments za hivyo huku aisee.
Kumbe wapo wengi wenyevakili kama yake jamaa.
Wanasema ukitaka kumjua mtu Mwambie aongee au aandike ndipo utajua yaliyomo moyoni na kichwani nwake.
Ndipo utajua hapa pana mtu au hapana.
Vijana wengi sahv wanataka mafanikio...wako tayari kuuza hata utu wao

Ova
 
Mafanikio kwa kujitoa utu wako ?
Kwani maana ya mafanikio ni nini labda ?!
Kuwa na material things pekee ?
Tafuta kujua zaidi aisee.
Heshima na utu ndio mafanikio ya kwanza kwa binadamu mengine yanafuata.
Tafsiri ya utu haiwezi kulingana kati ya jamii na jamii, mtu na mtu ndio maana Mimi na wewe tonafautiana kwenye huu mtazamo . Kwa maana ndogo tu utu ni kufanya matendo ya kibinadamu.(akili) Mwijaku ana shahada ya sanaa, anachofanya ni sehemu ya kile alichosomea na ubunifu wake unamlipa! Kwa nini uhisi yeye anajiondoa utu wake?

Tukisema Kila kitu tukiangalie kwa undani kwa mitazamo yetu tunapata tafsiri iliyo potofu au kukibeza/ kuona sio sahihi. Mwisho wa siku unapata stress....take it easy bro! Enjoy life
 
Ni ajabu mtu kujaji maisha ya mtu ambaye huwezi ata kumsaidia chochote, kila mtu ana maisha yake na njia yake katika utafutaji, kulikoni ufuatilie maisha ya mtu ambaye hata akikwama huwezi kumsaidia chochote? Ikitokea leo mwijaku akasema aache kufanya hvo halafu umuchangie hela, cha ajabu ata hutatoa chochote mkuu, hvo ishi unavyopenda ww kuishi pia muache na yeye aishi anavyopenda yy kuishi syo uvyopenda ww mkuu, kla mtu na maisha yake na familia yake na kifo chake
 
Ukinisoma vizuri utaona nimeongea kitu neutral sio kwa sababu nafurahia nachokiona Ila ndio uhalisia.

Siku hizi upuuzi ndio unapigiwa promo kwa sababu ni rahisi kuuza kwenye mitandao ya kijamii. Mbaya zaidi hao hao social media influencers wanaokuza majina katika upuuzi ndio wanapewa channels za kupata pesa kama media careers and endorsements

Hata hiyo crown media inaonekana ina unafuu kwa sababu wanachukua sana influencers wa twitter ambao hawana controversies sana Ila sio kwamba wana uwezo mkubwa.

Kwa sasa watu wanajali numbers watazozipata kirahisi kuliko kuumiza kichwa. Mwisho wa siku tuanona tunayoyaona
 

Hao watendaji wenye brains wengi wamekaa kimya ili kulinda positions zao na wengine wakiweka mbele ujasiri. Wanapigwa pesa wananyamaza.

Hii nchi haina nafuu kuanzia juu hadi chini maana watu wenye substance wanawekwa kando kwa sababu wanatoa challenge kuliko hawa ambao wanaweza kujizima data. Unachowaambia ndicho wanachokisema
 
Ukweli mkuu tunatofautiana upeo, kwa hoja zako hatutofautiani na misimamo yangu lakini tutambue kuwa hatuwezi kufanana wapo ambao wanajali pesa kuliko utu wao mfano huyo jamaa anayezungumziwa hapa.

Kwangu mimi ni heri nikose pesa lakini sio kuuza utu wangu, maana naamini shida ni sehemu ya maisha ila shida haziwezi kunitesa, sasa hapo ndipo nitatofautiana mimi na huyo jamaa lakini haimaanishi mimi ni bora kuliko yeye, ni uwezo tu wa kutafsiri mafanikio ndo tumepishana.

Hivyo ni lazima tuelewe kuwa hatuwezi kufanana. Kupitia muda atakuja kujifunza kama sio yeye basi kupitia kizazi chake.
 
Da, unasikitisha sana. Mawazo yako yalikuwa yana nafasi kipindi cha Victorian huko UK. Tuache binadamu wafanye chochote kwa sababu tu wakikwama hatuwezi kuwasaidia?
 
Mkuu taifa linaongozwa na watu wasiotaka wajenga hoja, wauliza maswali na wala wapiga zumari wanafurahia majibu yasiyojibu maswali wala hoja.
Vijana taifa hili wataendelea kuwa machawa, maslay queen n.k kwa sababu kazi hizo ndizo sasa zenye fedha. Wasomi kwa sasa hawatakiwi na ukipata nafasi ukataka kutumia usomi wako mfumo unakutema. Ili uendelee kusurvive usomi unautupa pembeni unakuwa kama wao.
Never underestimate the power of stupid/evil people in large numbers
 
Njaa ni mbaya sana...... mwachen afanye mm ningepTa nafasi ya uchawa aaah pesa mbele,

Njaa inauma
hii ina maana huwezi kuwa chawa otherwise ungeshakuwa chawa kwa kuanza kujipendekeza tu from nowhere. Anza kwa kujirekodi unakata mauno ukiwa umevaa tshirt ya mama na kofia ya chama ukisifu na kuabudu.... Utatrend watu wakianza kushare video yako wakikundia jinsi gani unajidhalilisha na ambavyo huna akili.
 

Kama ukisoma Sanaa unakuwa vile basi hapana aisee.
No mind transformation
Kwa hiyo walosoma Sanaa wote wako na behavior kama yake kwenye jamii ?

Education is not a piece of paper (certificate ). Yaani cheti.
Education must be reflected through behavior in the society.
Ndipo tutajua kuna msomi au mfano wa msomi ?!
 
Kwani mwijaku na babalevo uchawa wameuanza lini ?

Mimi kukatika siwezi aseeh, nashindwa mno

Kama una kibarua Cha kufagia au kupanda maua hapo home nipe,

siwezi for sure πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwani mwijaku na babalevo uchawa wameuanza lini ?

Mimi kukatika siwezi aseeh, nashindwa mno

Kama una kibarua Cha kufagia au kupanda maua hapo home nipe,

siwezi for sure πŸ˜‚πŸ˜‚

uchawa wa namna ya mwijaku unataka moyo. Sema now kila mtu chawa tu hata AY sikutegemea nikasikia wao wanajiita Samia Kings.
Vijana now ni pesa na nahisi kuna pesa ndiyo maana kila mtu now anajifanya ana mahaba sana na CCM.
Unajua tunawakandia ila watanzania wanawasilikiliza wao kuliko wale tunaosema wana hekima na wasomi. Ukimpa msomi akutangazie jambo watanzania wachache watafuatilia kuliko ukimpa mwijaku.
 
Upo sahihi kabisa ndugu
 
When ignorance is bliss to be wise is foolish
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…