Tupe maoni, ushauri, dokezo: Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Wenye Makundi Maalum

Ahsante Sana kwa maswali yako mazuri.

Muda huu nitajibu hoja chache tu, maana ziko nyingi, zingine nitaendelea.

Kuhusu baba watoto kufungwa; kwa kifupi kabisa, kufungwa huwa ni hatua ya mwisho kabisa katika mnyororo wa kutafuta amani ya ustawi wa jamii na pale ambapo mahakama imejiridhisha kwa mujibu wa sheria kuwa, ndugu yetu huyu anazo hatia na hana la kujitetea au utetezi wake labda hauna mashiko.

Kuhusu ubora wa sheria; sheria za nchi yetu huandaliwa kwa utaratibu stahiki uliowekwa. Hivyo, iwapo inaonekana kuna kifungu kimepitwa na wakati, ni kutoa maoni tu utaratibu wa mapitio ufanyike.

Ahsante Sana kwa leo, nakutakia usiku mwema na baraka.
 
Ahsante Sana kwa muda wako na mchango wako. Nikupe pongezi nyingi kwa hatua hiyo uliyofanya kutoa msaada wa kijamii.

Ipo wizara mahsusi inaitwa ya Kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu. Hii inashughulika na maendeleo ya vijana, kule kuna program mbalimbali kwenye Kila halmashauri kwa ajili ya maendeleo ya vijana. Aidha, ziko program zingine kwenye halmashauri kuhusu maendeleo na afya kwa vijana balehe.

Kwenye programu hizo, kuna huduma za afya, unaishi, ujasiriamali, saikolojia na mambo mbalimbali.

Kwa elimu zaidi, fika halmashauri au ofisi za serikali kata, utapata maelezo ya afisa mahsusi anayeratibu eneo la vijana kulingana na changamoto ya kijana husika.

Shukrani
 
Uoni aibu kuwa na wizara ambayo sio Rafi Kwa huduma za walemavu wanaozea nyumbanihawsomi hat dras moja
 
Uoni aibu kuwa na wizara ambayo sio Rafi Kwa huduma za walemavu wanaozea nyumbanihawsomi hat dras moja
Hapa sidhani kama ni sahihi kumlaumu Mh. Waziri. Wizara Iko Dodoma sisi mtaani tunakoishi tunafanya nini kuhakikisha watoto wenye ulemavu wanakwenda kwenye shule zinazochukua watoto wenye uhitaji maalum!?
 
Heshima yako Mama! hongera na pole kwa majukumu uliyonayo. unajitahidi sana kupambania na kuitendea haki nafasi yako uliyopewa. hakika unastahili pongezi. Ila napenda kusema kuwa wizara hii inayohusisha wanawake inayo mambo mengi ya kushughulikia. lkn ili Tanzania yetu iwe na watu bora , amani na mafanikio yasiyokuwa na kikomo , yote yanaanzia kwa wanawake. kwa hiyo inabidi kwanza muongeze zaidi kampaini na movement za kuwahimiza wanawake wote Tanzania kuwa na hamu ya kuwa na watoto wasiokuwa na ulemavu na akili timamu.

Ili tuweze kuwa na taifa lenye kueleweka zaidi kwa baaadae. Haswa kutumia vidonge vya folic acid mara tu wanapohitaji kubeba mimba na kuendelea navyo mpaka miezi mitatu baada ya kujifungua. na kingine pia wanawake tuelewe na tutambue kuwa jukumu la kuhudumia familia si kwa baba tu, leo na kesho anaweza asiwepo. kwa hiyo tunapopanga kuzaa tuchague idadi ambayo tunajua hata mwenza akikwama maisha yanaweza kusogea , ili tupunguze idadi ya watoto wa mitaani.

Mwisho ni jukumu la wazazi wote wawili kuwajali na kuwapenda watoto wao, kwa hiyo upendo uanze mtoto akiwa bado mimba, mama kuzingatia dawa na kwenda clinic kucheck ultrasound kama mtoto ana kasoro yoyote.
 
Ushauri wenu kwenu fuatilieni kozi ya social work ipo chini ya wizara yenu, kuna mauza uza mengi sana kwenye hii kozi kwa upande wa cheti na diploma,
 
Mbunge aliyezungumza suala la kuwajujumlisha jinsia ya kiume yuko sawa kwa 100%
 
Ahsante Sana kwa.maoni yako. Hakika una hoja ya msingi
 
Mbunge aliyezungumza suala la kuwajujumlisha jinsia ya kiume yuko sawa kwa 100%
Wanaume tayari walishajumlishwa kwenye sera mpya ya taifa ya jinsia na maendeleo ya wanawake iliyozinduliwa tarehe 8 Machi, 2024, elimu kwa umma ilishaanza na elimu kwa wabunge. Turejee ukurasa wa 22 "male engagement". Shukrani.
 
Ahsante Sana kwa maoni. Kwa upana zaidi tafadhali sms kwenye 0765345777, ningependa kuelewa zaidi. Shukrani
Heshima yako mkuu, naomba kufichua uovu na pia kufahamishwa njia za kupita ili kupata haki, iko hivi

Kuna binti aliolewa na akapata mimba ndani ya mwaka mmoja, bahati mbaya wakati wa ujauzito mume akawa anamtolea matusi mabaya yasiyoandikika hapa, imefika mpaka kumwita malaya na shutuma nyingi zaidi ya hizo,na ushahidi upo wa maandishi, sauti na hata video.

Sasa binti akalea mimba mwenyewe kwa wazazi wake bila ya msaada wa mume, na akajifungua salama bila ya msaada wa mume na akatunza mtoto mwenyewe bila ya msaada wa mume, na baada ya miezi miwili ya kujifungua akapewa talaka na mpaka sasa mtoto ana miaka miwili kamili mama kupitia wazazi wake analea mtoto mwenyewe.
Sasa tatizo limeanza kujitokeza baada ya baba kuja kudai mtoto na kutoa matusi ya nguoni na kashfa za umalaya zikiendelea wakati huyu si mkewe tena,

Sasa naomba kujuzwa,je wapi huyu binti apeleke malalamiko yake?
Msaada tafadhali
Natanguliza shukrani sana
Asante
 
Najua kuna maoni kama haya huko chini. Ila yangu ni kwamba, badilini kwanza jina la wizara. Kwamba wanawake wana jinsia yao? Kwamba wanaume hawahusiki na hii wizara? Baada ya hapo ndio nitatoa maoni yangu
 
Mimi nauliza kuhusu ajira za watoto, unakuta kabinti ka miaka 13 mpaka 14 ni ka "housegirl" sehemu, hiyo ni haki kweli au kuna sheria inawalinda wanaoajiri hao watoto?
 
Najua kuna maoni kama haya huko chini. Ila yangu ni kwamba, badilini kwanza jina la wizara. Kwamba wanawake wana jinsia yao? Kwamba wanaume hawahusiki na hii wizara? Baada ya hapo ndio nitatoa maoni yangu
Salaam. Ahsante kwa muda wako na maoni yako. Wizara hii ni ya Jinsia zote. Ndiyo maana sera mpya ya jinsia ya Mwaka 2023 ukurasa wa 22 unaongelea wanaume (male engagement). Ndiyo maana watoto wote chini ya miaka 18 inahusu jinsia zote. Labda useme umekwama wapi na ukakosa huduma gani tafadhali?
 
Kwanza pole nyingi kwa Binti huyu. Pia, huyu Binti kama ana mawasiliano mpe namba yangu ya simu anitumie ujumbe nitamuongoza akikwama.

Utaratibu rasmi ni, aende Dawati la jinsia polisi aandikishe maelezo. Pale atapewa mtaalamu wa ustawi wa jamii atasikiliza shauri hili na kuliongoza kwenye utaratibu.

Upo msaada wa kisheria pia, akihitaji atapewa.
Ahsante Sana

Niwie radhi kuchelewa kujibu, mambo huwa wakati mwingine yanakuwa mengi.
 
Mimi nauliza kuhusu ajira za watoto, unakuta kabinti ka miaka 13 mpaka 14 ni ka "housegirl" sehemu, hiyo ni haki kweli au kuna sheria inawalinda wanaoajiri hao watoto?
Tena juzi hapa tumekamata wanandoa kule goba kwa kutumikisha mtoto. Ni kosa kisheria. Taarifa zinatakiwa kutolewa Dawati la Watoto kituo cha Polisi. Pale pia Yuko afisa ustawi wa jamii.
 
Uoni aibu kuwa na wizara ambayo sio Rafi Kwa huduma za walemavu wanaozea nyumbanihawsomi hat dras moja
Iko wizara ingine inayohusika na wenye ulemavu inaitwa, wizara ya Kazi, ajira, vijana na wenye ulemavu.

Nikadhani unaijua.
 
Mbunge aliyezungumza suala la kuwajujumlisha jinsia ya kiume yuko sawa kwa 100%
Sera ya Jinsia ya Mwaka 2023 tuliyozindua 8 Machi 2024 ukurasa wa 22 walishajumuishwa. Vyama vya wanaume vimesajiliwa, watoto wote wa kike na kiume chini ya miaka 18 wako wizarani miaka yote. Madawati ya ulinzi wa watoto shule za Msingi na sekondari, madawati ya Jinsia Polisi na vyuoni, yote yanahudumia wanaume na wanawake ..

Changamoto: ukiacha watoto, wanaume watu wazima hawajitokezi. Ila inbox baadhi wanatumaga ujumbe tunawaunganisha na huduma, pia kupitia rais wa Chama cha wanaume na mwenyekiti wa Chama cha wanaume Wazee.

Tuendelee kutoa maoni tafadhali. Shukrani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…