geraldincredible
JF-Expert Member
- Mar 26, 2017
- 2,035
- 7,223
Ww ndio maloto.....umesoma na aslay njia ya Muongo Ni fupi hahahahahah unaiba story za watu fb huko na insta unasema ww ndio maloto....maloto ndio wa kusoma na aslay shenz
Sent using Jamii Forums mobile app
KISA CHA ASLAY KUCHEZEA BAKORA
By Sangu J
Mimi nimesoma na Aslay Isihaka pale Tandika Sekondari lkn nilimpita darasa moja Mimi nikiwa form three yeye alikua form 2.
Sasa wakati Ngoma yake ya naenda kusema Kwa Mama inatamba full kupata interview kwenye media kama zote, alienda kwenye Kituo kimoja cha radio nadhani ni Clouds FM sasa alitamba Kwamba siku hizi Shule hachapwi wala Viongozi wa Shule hawampi fagio akafagie.
Basi Jumatatu yake baada ya kufika Shule akakutana na Kiongozi (Kiranja) mmoja alikua anaitwa Theodory Mwingira alisikia Yale mahojiano basi jamaa hiyo siku alichelewq kufika Yule mshkaji akampa adhabu akazoe takataka kwenye eneo lenye nyasi nyingi na afyeke.
Basi Dogo Kwa kuwa ni Star alijifanya anaingilia huku anatokea huku (Kiufupi anamkwepa) basi Yule Dogo akaenda kusema Kwa Mwalimu mmoja alikua anaitwa Likalambile anafundishq Mathematics Hatari na kama mnavyojua Walimu WA mathe wanakuaga wakali sana basi Aslay aliitwa na Yule Ticha alipigwa bakora mpaka aliamua kwenda kuruka ukuta wa Shule Kwa bakora za Yule mwalimu.
Ikawa bonge moja la Stori Shule nzima Aslay kachezea kichapo tena Yule Mwalimu alimpiga akimwambia Nenda kaseme kwa Mama.
Kupata Stori nyingine nicheki Instagram na Facebook sangujoseph
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app