Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Tupe stori za msanii uliesoma au kujuana nae kabla ya umaarufu

Wimbo wa "ghetto langu"" humo ndani ndio kuna hicho kipande.
"masela kibao wanapenda kuja na mademu zao!nia yao!waje kuwa**pa nao!wakifika ndan wanaishia kuduwaa mwishowe muda ukifika wanaishia kuduwaa wanatambaa!kesho yake demu anakuja pekee!eti anazuga anamtafuta mchizi wake!nikimulekeaza kwake amfate anadai eti amechoka anataka kidogo apumzke!akifka ndan haishi kukusifiaa hata mchiz wake anaanza kumkandia!haipit muda ameshanikumbatia oooh!ndo kisa cha kugombana na evance aliponikuta ghetto na mdogo wake nancy!nambia manebo haya uliyaskia wapiiiiiiii!
 
Mwl Banana anapiga stick nae yule alitokea Nyanza primary akaletwa Mirongo kwa matahira. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Mwanza ilikuwa Ni aibu saana kusoma Mirongo sababu kulikuwa na shule ya walemavu wa akili mixer na wenye utimamu wa akili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu acha kupotosha bhana, hicho kitengo cha walemavu wa akil kilkua knajtegemea had walimu wao walkua tofauti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa nasubiri kuskia aliyesoma na Pfunk majani naona bilaaa aisee kuna wengine hawajasoma bongo aisee..
Sidhani kama watakuwepo humu, P funk kasoma IST pale ada zao hadi milioni 60 kwa mwaka, Modewji nae alisoma hapo, Chuo alisomea huko uholanzi fani ya utayarishaji wa mziki ndio mana ngoma zake zilikuwa na kiwango cha juu
 
Kwanza kabisa nimesoma na Edward Nyerere wenyewe walikua wanamuita Chief Rocka enzi zile wana kundi lao wanajiita The Rockaz (Abbot a.k.a Quick Roca, Moracka, Dau Roca). Mshkji alikua mtu poa sana wala hakua na makuu. Alikua amenizidi kidato kimoja,
Then at the same school tulikua pia na jamaa mmoja wa kuitwa Jimmy Jeezy, jamaa ni producer mmoja mkali sana sema tu aliamua kuachana na uproducer ila ndio aliyoproduce Ngoma ya mateso ya country boy na lina.
Cliff mitindo na Ben Pol nilikutana nao chuo ifm. Wote walisomaga school Aza boys na mwanang mmoja wakuitwa bwana Cow. Enzi hizo Ben pol anaishi vingunguti anakuja kuangusha ghetto kwetu maeneo ya Hindu Mandal pale tunapika nguna tunagonga wote usiku tunategea mida ikienda tunasogea posta mpya pale Kuna wamaza wanapika misosi mnakaa kwenye mabenchi mnagonga au siku mawe yakiwa fresh mnaenda kule kisutu Chef's pride mida ambayo wahindi wameshaenda kula wameshiba hivyo misosi inabaki kibwena mnaenda kula bufee kwa hela ndogo tu maana wahindi hua hawakubali kumwaga chakula.
Sanchoka nae tumekaa nae jengo moja enzi za ifm pale maeneo ya nbc club kabla sijahamia Hindu Mandal, tulikuaga tunamuita buggati.
Abdul Mohammed naye nilikujuana nae ifm enzi hizo yuko clouds anatangaza sports extra na nakumbuka nilikuaga nampiga pindi la Qm. Kabla hajasepa zake na kwenda BBC. Aisee list ni wengi ila wachache sana ambao tunakeep nao intouch

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mlisoma makongo hampo humu!!!
Umenikumbusha mkuu, pale wakati nipo olevo nawaona kina marehemu amina chifupa (alikua na mdogo wake wakuitwa Rehema pini moja matata form 3), daz baba,makamua, salma jabir (aliletwa na kipingu kutoka zenj kwaajili ya kipaj chake cha b/ball), hasheem thabeet pale kantini alikua akisimama anavuka hadi lile paa la kantini kwa urefu wake. Pawasa nafkiri aliishia form 5 pale hakuendelea. Ila wengi waliosoma pale mwisho wa siku matokeo yao wali-differentiate constant

[emoji851][emoji81][emoji23][emoji28][emoji3][emoji16][emoji74][emoji86][emoji85][emoji204][emoji205][emoji38][emoji2][emoji1787][emoji1]

Mkuu umeniacha hoi hapo kwenye differentiate constant. Means walikula zero zao saaafi kabisa.
 
"masela kibao wanapenda kuja na mademu zao!nia yao!waje kuwa**pa nao!wakifika ndan wanaishia kuduwaa mwishowe muda ukifika wanaishia kuduwaa wanatambaa!kesho yake demu anakuja pekee!eti anazuga anamtafuta mchizi wake!nikimulekeaza kwake amfate anadai eti amechoka anataka kidogo apumzke!akifka ndan haishi kukusifiaa hata mchiz wake anaanza kumkandia!haipit muda ameshanikumbatia oooh!ndo kisa cha kugombana na evance aliponikuta ghetto na mdogo wake nancy!nambia manebo haya uliyaskia wapiiiiiiii!
Aisee ..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaani kuanzia Chekechea, Shule ya Msingi, shule ya sekondari, shule ya Adance mpaka chuo sijawahi soma na msanii kweli ?

[emoji23]nimecheka sanaaa
ila haupo peke yako, mimi nimesoma na underground mmoja anajiita azzy wizzy huko Ahlulbayt islamic seminary,japaa ana talent ila tatizo muziki anaoimba ni wa kigumu

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
[emoji851][emoji81][emoji23][emoji28][emoji3][emoji16][emoji74][emoji86][emoji85][emoji204][emoji205][emoji38][emoji2][emoji1787][emoji1]

Mkuu umeniacha hoi hapo kwenye differentiate constant. Means walikula zero zao saaafi kabisa.
[emoji23][emoji23][emoji23] ndio mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma na wasanii ila bado si maarufu sana. Mmoja wapo ni yule mmasai wa mahanjamu ya star tv. Alikuwa cha sita mimi nikiwa cha tano kipindi tupo longido a level. Alikuwa room mate. Japokuwa kiukweli tulikuwa hatupatani flani hivi sababu alikuwa hapendi kubishiwa anapokuwa anatoa stori zake, sasa mimi nilikuwa nabisha sana, so akawa ananiona kama myeyusho hivi😀😀😀. Kuna wakati alitaka kunizingua ila nikavimba kugumu japo nilikuwa najua akiamua kunipiga angenikung'uta kwelikweli😀😀😀😀😀😀. Ila jamaa ana kipaji cha comedy cha hali ya juu, alikuwa akikaa kupiga story zake basi watu wanajaa nyomi full kucheka. Huwa naangalia mahanjamu nasikitika sana, hayuko katika ile level ninayomfahamu. Nadhani akitafuta namna bora atakuwa bonge la comedian halafu pia anaimba na kuchana na matalent mengine kibao.

Mwingine naye hapohapo longido naye alikuwa roommate. Anaitwa gaudence sikuhizi naye anajiita masai. Yeye alikuwa anakung'uta kinanda balaa. Siku hizi niproducer ndiye aliyeprocuce ngoma mpya ya bonga aliyekuwa producer wa harmonize.

Na wakati nikiwa NIT nilikuja kusikia kuwa s2kizy alikuwa anasoma pale japo kwa muda huo alikuwa kashaacha chuo.
 
jamaa alikua na uchanaji flani hivi kama hataki miongoni mwa ngoma zake ni cheza hardcore, shida tu ft makabei(lebo ya kijani jamaa alikua anajua sana r&b) na ile moja baghdad akaiba chorus

siku moja kulikua na sherehe hapohapo azania sasa ikafanyika rehersal kwaajili ya kupata wasanii watakaoperform, miongoni mwa walioshiriki walikua ni makabei(simba mwinyi) na tapa square kwa azania na kule benjamini alikuja sheta ila mwisho wa picha tapa alitemwa sasa tulipokua tunarudi home mimi, makabei, tapa na masela wengine tapa akawa analalamika kwa kusema "wale majaji waseng* hawajui mziki yani wananiacha mimi nnaekubalika na maproducer wakubwa wanamkubali mlamba lips yule sheta" me nikaishia kucheka tu

amsr.
Daah so sad... alikuwa mwanangu san tapa square! Alikuwa na nyimbo yak moja inaitwa 'sambona' bonge moja la ngoma..RIP kwake daah ndo nmejua leo asee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom