Tena Mazengo sekondari na wakaacha machata yao mule.
Albert Mangwea - RIP
Moses Bushagama (MEZ B) - RIP
Haji Nura.
Athumani Kabongo (Dark Master)
Mangwea.
Jamaa mpole na mkimya sana. Alikuwa anapenda Basket Ball na alikuwa fundi wa ku dunk na ku score 3 points. UMISETA kitaifa Mwanza mwaka 2000 ndio alikuwa best Basket Baller na aliipa sifa kemkem Mazengo secondary hadi shule kupewa zawadi ya Computer achilia mbali zawadi zake.
Alikuwa si wa kuhudhuria sana class hasa alivyofika form III muda mwingi nje ya class akikariri mashairi. Nimewahi mshuhudia akikariri mashairi ya Vulindela (Brendah Fassie) huku anaehakikisha anaimba sahihi jamaa mmoja alikuwa anaitwa Jose by then alikuwa namba 1 goalkeeper wa Mazengo.
MEZ B.
Toz fulani na mtoto wa kishua enzi hizo. Anatembea kwa mwendo wa mdundo Alikuwa Day schooler. Alikuwa anapenda sana Basket Ball ila mkali wao alikuwa Mangwea. Mez B alikuwa hajionyeshi kama anaimba but alipoibukia hata sijui.
Haji Nura.
Anaenda Mazengo 1998 as one of the best student wa mkoa wa Shinyanga kwa waliomaliza la 7 1997. Alikuwa na akili sana class but muda mwingi aliwekeza kwenye muziki. Nakumbuka kuna siku tukiwa form II tulipishana nae maeneo ya History Block nikiwa naimba baadhi ya mashairi ya Do for love (2PAC) basi akawa amependa sana na kuniuliza ahhh kumbe wewe ni mdau but kiukweli sikuwa that deep. Of course jamaa alikuwa na kipaji maana katumbuiza sana kule Makole Club la Aziz enzi hizo. Nakumbuka alikuwa anaimba Wimbo fulani wa kuji introduce kuwa "nasoma mazengo, kidato cha tatu" ila hapa anaiga wimbo wa Sisqo wa Thong Song (Ukiusikiliza utaelewa). Jamaa alikuwa anaweza.
Dark Master.
Dah! Nikiwa form 1 yeye Form 4. Walikuwa wakorofi sana hasa kwenye room yao pale bweni la Mwenge. Yeye anakaa room number 1 up na mimi number 4 up. Waliosoma Mazengo hapa wananielewa vizuri. Siku moja ilikuwa jumamosi jamaa wamekula ugali na samaki mkavu then wamechafua room sana. Dark Master anakuja room kwetu ananiita wewe form 1 njoo hapa kufika room ananiambia safisha room iwe safi huku wamekula wao. Nikaanza kugoma jamaa akanikaba na kunibamiza dirishani ananiuliza unasafisha husafishi ilibidi nijitetee nasafisha ngoja nikachukue ufagio. Alivyoniruhusu ikabidi nitoke nje ya bweni maana mlango ulikuwa karibu na chumba chao. Jamaa ananifuatilia nimefika chini tayari nikamwambia naenda kwa head master (Enzi hizo Msasa anatisha hatari) kukusemea maana unanionea. Jamaa ilibidi aombe msamaha kwakuwa walikuwa wanamfahamu alivyo huyo Mkuu wa Shule.
Kwa ufupi jamaa alikuwa mkorofi kulingana na company yake maana walikuwa ni watu wa kitu cha Arusha.
Upande Mwingine.
Nimesoma na Nick Mbishi but mie nikiwa Bachelor yeye Diploma. Sina story za huyu dogo lakini alikuwa ni mtu wa kuimba mengi kuhusu chuo na kuhamasisha mambo mazuri hasa kwa wanafunzi.
Asanteni.
Sent using
Jamii Forums mobile app