Hili la Wamachinga lisiangaliwe kwa upande mmoja wa shilingi, ukigeuza mwingine ni kuna MaDon kwa makusudi mazima ya kukwepa kodi wanaleta vijana kutoka vijijini wanawapa bidhaa waingie nazo mitaani kwa mgongo wa MACHINGA huku wao wakinufaika,

Machinga ana uwezo wa kununua hadi mzigo wa Milioni 5 huyo ni Machinga???

Bidhaa zao ni ghali kuliko za dukani, wasiopenda kutembea wanadhani wamenunua kwa rahisi kumbe kapigwa dabo na machinga,

Sipati kusema hiyo kuchafua jiji na lugha chafu,

Naipongeza sana Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mama yetu mpenzi SSH, kufanya maamuzi magumu ni jambo la kuumiza lakini litazoeleka,

Bado hawa Omba Omba wanaowatembeza watoto wadogo kwenye jua kali na wengine kuwanyima haki yao ya kusoma na kuwageuza mtaji, habari zao tunazo wanafadhiliwa na watu jioni wanapeleka hesabu.
 
Kwani haukumsikia mwendazake aliposema hata mkitaka kajengeni ikulu! Hii nchi ni yenu.
 
Kwa hiyo ni Bora kuwa na Meza ya Chakula ya Kioo halafu mnachokula Ugali wa Mtama na Matembele?

Tunaiga nini yaani kuwe na Maeneo ya NOBLES na Maeneo ya daraja DUNI au sio? Kuchafua Mji!

Kama ndani ya Wamachinga kuna watu wana Mitaji ya 5 Mil na zaidi,mbona hatujaona angalau hata pakifanyika ufuatiliaji wa nani ni yupi na anapata kiasi gani?

Kilichopo ni kufagia tu hakuna Cha mwenye Chungu au Sanduku moja ama Mzigo wa kubeba na Canter.

Tufahamu kuwa Machinga wasio na Uwezo mkubwa kihalali wapo zaidi ya 90%
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…