Basi unaambiwa kwamba kuna mwalimu anaitwa Bachubila. Jina la utani tulikuwa tunamuita Ruba. Huyu ticha alikuwa hacheki na mtu yeyote yule. Tangu nianze fomu wani mpaka namaliza fomu foo sikuwahi kumuona akicheka. Usiombe ukutane na Ruba hujachomekea shati, hujahudhuria assembly au ukiwa umetoroka shule--utajuta kuzaliwa!
Kuna siku alinitaka niokote makombo ya chakula nimpelekee alishie kuku wake, nikamdis. Siku 1 alinivizia nikiwa natoka DH akanizaba konzi kidogo nizimie! Kisha alinipa adhabu ambayo niliifanya wiki nzima bila ku-attend class. Nilikomaje!
Sasa huyu bwana kiingereza chake kilikuwa na matege. Siku 1 kuna mwanafunzi wa fomu tuu alimpiga mwanafunzi wa fomu wani mbele yake, Ruba akadakia: 'WHY YOU BEAT FORM ONE IN MY FRONT?'. Hapa alikuwa na maana kwamba: 'KWANINI UNAMPIGA FOMU WANI MBELE YANGU?'. Bora hata alipokuwa hajui kiingereza, angekijua angekuwa mnoko zaidi. Kwa kweli mwalimu huyu alikuwa mtata sana, hakuna mwanafunzi shuleni kwetu Mara Sekondari asiyemfahamu huyu ticha mnoko.