Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kilikuwa kinataka misifa kwa mademu, kilinitoa nisisome geograph, afu ati kinafundisha huku kimekaa juu ya meza, nilisusa somo lake lakini nilifaulu vizuri
Kilikuwa kinataka misifa kwa mademu, kilinitoa nisisome geograph, afu ati kinafundisha huku kimekaa juu ya meza, nilisusa somo lake lakini nilifaulu vizuri
Umechanganya madesa, kashushula alikuwa wa pamba sec huyu ni wa mwanza sec
kwanza kashushua hata hakuwa mnoko
alikuwa mkali ili tusome shule za mjini ndo inatakiwa hivo la sivo
kila mwaka shule itakuwa ni 4 na 0 tu....
Baadae alihamia Mwanza sec...kwa upande wangu alikuwa mnoko
Jamen kashushula kahamia lini mwanza sec?
si unamuongelea yule maza alikuwa headmistress wa pamba sec?
Hajawahi kuwa mwasec huyo maza hizo shule zote mi nimesomaeee yule aliyekuawa mweupe hivi...
Hajawahi kuwa mwasec huyo maza hizo shule zote mi nimesoma
Basi Bundala wa Mwanza sec
Mie hata sijawahi kumuona ila nasikia ni mwalimu mzuri sana wa Biology na Chemistry. Sasa hivi kajenga shule yake maeneo ya Gongolamboto inaitwa Mkandawire Sec School.
Mama kikwete mbuyuni primary 1998....
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.
Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.
Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi. Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.
Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.