Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Tupia jina la mwalimu aliyekuwa mnoko shuleni/chuoni kwenu

Kitoko Mk*ndu alikuwa noma sanaaaa pamoja na mwenzie Mwl. Gamba Tarime Sec hiyoooo.

Huyu Gamba hata mimi nilipata habari zake ijapokuwa nilisoma Mara Sec. Nasikia huyu kidudu mtu alikuwa ni nuksi, balaa, mkosi!!!!!
 
Kilikuwa kinataka misifa kwa mademu, kilinitoa nisisome geograph, afu ati kinafundisha huku kimekaa juu ya meza, nilisusa somo lake lakini nilifaulu vizuri

Hahahahaha! Tena umenikumbusha mbali sana---wakati nasoma pale comb ya CBG, siku moja kukawa na test ya Geography--ilifanyikia kwenye darasa moja lililokuwa katikati ya yale madarsa mawili ya ghorofa. Wanafunzi wote tulipoingia ndani kiMgimwa kikafunga mlango na kutia kufuli ili wale waliochelewa wasiingie. Basi kulikuwa na mwanafunzi mmoja mlevi alikuwa ameenda Makanyagio kulewa. Aliporudi akakuta paper imeanza na mlango umefungwa. Jamaa akachana karatasi kwenye dafatari lake na kufanya paper akiwa amesimama nje ya darasa. Alikuwa akisoma maswali ubaoni kwa kuchungulia kupitia dirisha la kioo. Paper ilipoisha karatasi za majibu zikakusanywa na yule mwanafunzi mlevi naye akampa mwanafunzi mmoja kati ya wale wanafunzi tuliokuwemo ndani ya chumba cha mtihani akamkusanyia. Ikawa ngoma droo--jamaa kafanya paper akiwa amesimama nje ya darasa na bado kapasua. KiMgimwa na ukuda wake kikawa kimeshindwa na kulegea! Chezea Mkwawa Complex wewe!
 
Tarime sec mwaka 1987-1990 alikuwepo mwl anaitwa KAJOGOO WA NGARAMTONI. Hakuwa anajua vizuri somo la maths na physics. Halafu alikuwa mfupi. Sasa alikuwa anajiona inferior. Kutokana na hali hiyo alikuwa anatembeza stick class. Mwingine mwl RABARA na NYAMU. Mwingine GINSHULI ambae alikuwa mentally disturbed.
 
Kilikuwa kinataka misifa kwa mademu, kilinitoa nisisome geograph, afu ati kinafundisha huku kimekaa juu ya meza, nilisusa somo lake lakini nilifaulu vizuri

Ni kweli kabisa, kwa mademu kilikuwa hakikohoi. Halafu kilikuwa kinajifanya jiniasi--eti kinaingia darasani kufundisha Statistical Geography bila kuwa na daftari la kuangalizia! Kinavyopenda misifa kwa mademu, utakitaka?
 
Mwl Karuta, Buzuruga Primary Mwanza. Huyu mwalimu alikua mkali hadi wazazi walikua wanamgwaya
 
Umechanganya madesa, kashushula alikuwa wa pamba sec huyu ni wa mwanza sec
kwanza kashushua hata hakuwa mnoko
alikuwa mkali ili tusome shule za mjini ndo inatakiwa hivo la sivo
kila mwaka shule itakuwa ni 4 na 0 tu....

Baadae alihamia Mwanza sec...kwa upande wangu alikuwa mnoko
 
Namkumbuka mwalimu Kaselenge Kibaha sekondari kanionea sana
 
huyu hajapata kuwa mnoko katu,mkandawile mtu wa watu ,tumesoma tuition zake kwa bei ya bure kabisa
Mie hata sijawahi kumuona ila nasikia ni mwalimu mzuri sana wa Biology na Chemistry. Sasa hivi kajenga shule yake maeneo ya Gongolamboto inaitwa Mkandawire Sec School.
 
Katika shule/chuo hakosekani mwalimu msumbufu na ambaye huwafuatilia sana wanafunzi hata ktk mambo madogo madogo na kuwapa adhabu za ajabu ajabu.

Leo nataka tuwakumbuke walimu hawa pamoja na kujikumbusha vituko walivyowahi kuvifanya.

Mimi shuleni kwetu Mara Sekondari kulikuwa na mwalimu mmoja aliyeitwa Jigge. Basi siku moja kuna wanafunzi walitoroka kwenda mjini bila ruhusa. Na kibaya zaidi, walipokuwa huko mjini wakafanya fujo na kuharibu mali za wananchi. Taarifa zao zikafika shuleni. Ilikuwa jioni na kiza kilikuwa kimeanza kukolea. Mwalimu Jigge akapiga kengere. Wanafunzi wote tuliokuwepo shuleni tukakusanyika bwaloni na akaanza kuchuka roll call.

Ili kumkomesha mwalimu huyu, pamoja na kuwanusuru wale wanafunzi 'wahalifu' waliokuwa wamefanya tukio mjini, wanafunzi wakapanga kuzima umeme main switch na kumpopoa kwa mawe. Ghafla tu, umeme ulipozimika, mwalimu alichomoka kama mshale na kutokomea kizani. Wanafunzi walimtupia mawe lakini, kwa ile speed aliyochomoka, hakuna jiwe lililompata. Ana bahati sana.

duuh...unamkumbuka KIJUNGI..alikua mtukutu fulani hivi pale kigera
 
Kuna mwalimu mmoja alikuwa anaitwa Mtaturu huyu jamaa alikuwa hafai mwanzoni mwa miaka ya tisini Town primary school Tabora, na kwa walambo wengi wao watakuwa hawamsahau mwalimu Sikazwe alikuwa Discipline master wa Milambo secondary mwishoni mwa miaka ya tisini
 
Back
Top Bottom