Mpaji Mungu
JF-Expert Member
- Apr 24, 2023
- 17,613
- 56,787
Madam mahari fuso mbili za ng'ombe zipo standby sema suuu nilete
Karibu sana.Nzuri sana love, ndiyo chakula rahisi na cha haraka nikipendacho 🥰
Hapo unaweka 1 badala ya 3. Hata mimi sipendi mayai yawe mengi kwenye chapati za maji.Wengi nimegundua hawazipendi kutokana na kupikiwa na mayai.
Binafsi mimi huwa si mpenzi wa mayai ila yakipikiwa kwenye chakula nakula.
Sawa siku ya kupika chapati za kawaida niambie,tupike wote natamani sana kujifunzaLeo Jumapili niliamka nikiwa nina hamu sana ya kula chapati za maji.
Ila leo nikasema kwa kuwa nina muda wa kukaa jikoni, ngoja leo nijikumbushe enzi zangu.
Mahitaji na viambaupishi:
-Unga wa ngano nusu
-Mayai ya kuku 3
-Maziwa ya maji nusu kikombe
-Tui la nazi kikombe kimoja
-machicha ya nazi kijiko kidogo kimoja
-Unga wa sembe kijiko kimoja kikubwa ( hii husaidia chapati kuwa crunch)
-maji ya vanilla kijiko kidogo cha chai
-manjano (si lazima)
-pilipili hoho kipande
-karoti kipande
-kitunguu maji kimoja kizima
-sukari vijiko 2½ vikubwa
-chumvi kiasi upendacho
-Maji vijiko 3 vikubwa
-hamira kidunchu sana (napenda chapati ijae kidooogo)
Maandalizi:
Nilichukua bakuli na kutia unga wa ngano, wa sembe, hamira, sukari, chumvi na yale machicha ya nazi.
Kisha nikatia nazi na tui kisha nikaanza kukoroga.
Baada ya mchanganyiko kuwa tayari, nikatia vanilla, hoho, karoti, kitunguu na mayai.
Nikauacha upumue.
Baada ya kupumua nikatia manjano kwa mbali sana na maji vijiko 3.
Kisha nikauacha uchanganyike vyema.
Huwa napenda sana kutumia margarine (si ya maji) katika kupikia.
Nikajipikia zangu hapa.
View attachment 3317754
Upande wa juu
View attachment 3317761
Upande wa chini
View attachment 3317762
Hapa zikiwa tayari
View attachment 3317765
Hapa nikajitengea zangu na kuanza kula
Nilikula zangu chapati za maji pamoja na chai ya maziwa na kiporo cha maini cha jana.
Karibuni
View attachment 3317766
Msishangae kuona naweka viambaupishi vingi, nimepika sana kwenye hotels na vijimgahawa ndio maana hio asili bado ninayo.
Cc:
Mwachiluwi
Hiyo kawaida kabisa, unajikuta hata mpikaji umo, unasema ngoja nionje kama ziko sawa. Unajikuta umeshakula hata 4 🤭🤭🤭🤭Karibu sana.
Ni mlo wa haraka kwa asubuhi.
Sema kwenye kuzipika unaweza jikuta zote zinaishia jikoni kabla ya kufika mezani 😅😅
Maaana naona zinachukua muda kupika
ukila nne jua wewe ni mroho na mrafi...😂Hiyo kawaida kabisa, unajikuta hata mpikaji umo, unasema ngoja nionje kama ziko sawa. Unajikuta umeshakula hata 4 🤭🤭🤭🤭
Kwenye maziwa huwa natumia ya maji, kuna siku nikajaribu ya unga yanashika zaidi na utamu unausikia wa maziwa zaidi.
Ndio inawezekana pia.Hapo unaweka 1 badala ya 3. Hata mimi sipendi mayai yawe mengi kwenye chapati za maji.
Sawa.Sawa siku ya kupika chapati za kawaida niambie,tupike wote natamani sana kujifunza
Hapo nashushia na juice au maji ndiyo nimeahakula tena. Huwa tamu sana na laini.ukila nne jua wewe ni mroho na mrafi...😂
Sasa baby hili pishi hujawahi kunipikia niambie utanipikia lini mpenzi wangu wa huba..?Hapo nashushia na juice au maji ndiyo nimeahakula tena. Huwa tamu sana na laini.
Sasa madame chapati unaweka hamira si unavimbiwa hata ukila moja tu20 mtu mmoja?😲😳😲😳
Acha zako aisee.
Mimi 3 tu niko hoi kabisa + chai na kiporo
Kweli tumetofautiana.
Yaani hizi tu jikoni ukisema uonje sijui chumvi na sukari, ushakula 4 kabisa🤭Hiyo kawaida kabisa, unajikuta hata mpikaji umo, unasema ngoja nionje kama ziko sawa. Unajikuta umeshakula hata 4 🤭🤭🤭🤭
Kwenye maziwa huwa natumia ya maji, kuna siku nikajaribu ya unga yanashika zaidi na utamu unausikia wa maziwa zaidi.
Next weekend nitakupikia usijali. Au nitazifata Dom kwa dada mkubwa Madame B maana zake ni zaidi vikorombwezo vingi, nimejifunza vitu vipya.Sasa baby hili pishi hujawahi kunipikia niambie utanipikia lini mpenzi wangu wa huba..?