Leo Jumapili niliamka nikiwa nina hamu sana ya kula chapati za maji.
Ila leo nikasema kwa kuwa nina muda wa kukaa jikoni, ngoja leo nijikumbushe enzi zangu.
Mahitaji na viambaupishi:
-Unga wa ngano nusu
-Mayai ya kuku 3
-Maziwa ya maji nusu kikombe
-Tui la nazi kikombe kimoja
-machicha ya nazi kijiko kidogo kimoja
-Unga wa sembe kijiko kimoja kikubwa ( hii husaidia chapati kuwa crunch)
-maji ya vanilla kijiko kidogo cha chai
-manjano (si lazima)
-pilipili hoho kipande
-karoti kipande
-kitunguu maji kimoja kizima
-sukari vijiko 2½ vikubwa
-chumvi kiasi upendacho
-Maji vijiko 3 vikubwa
-hamira kidunchu sana (napenda chapati ijae kidooogo)
Maandalizi:
Nilichukua bakuli na kutia unga wa ngano, wa sembe, hamira, sukari, chumvi na yale machicha ya nazi.
Kisha nikatia nazi na tui kisha nikaanza kukoroga.
Baada ya mchanganyiko kuwa tayari, nikatia vanilla, hoho, karoti, kitunguu na mayai.
Nikauacha upumue.
Baada ya kupumua nikatia manjano kwa mbali sana na maji vijiko 3.
Kisha nikauacha uchanganyike vyema.
Huwa napenda sana kutumia margarine (si ya maji) katika kupikia.
Nikajipikia zangu hapa.
View attachment 3317754
Upande wa juu
View attachment 3317761
Upande wa chini
View attachment 3317762
Hapa zikiwa tayari
View attachment 3317765
Hapa nikajitengea zangu na kuanza kula
Nilikula zangu chapati za maji pamoja na chai ya maziwa na kiporo cha maini cha jana.
Karibuni
View attachment 3317766
Msishangae kuona naweka viambaupishi vingi, nimepika sana kwenye hotels na vijimgahawa ndio maana hio asili bado ninayo.
Cc:
Mwachiluwi